![]() |
Rais wa Zambia, Edgar Lungu |
Katika uamuzi wa wengi ,jopo la
majaji katika mahakama hiyo ya kikatiba liliamua kwamba mda wa mwisho uliowekwa
kusikiliza kesi hiyo ulikuwa umekwisha.
Bwana Lungu alihifadhi kiti chake
baada ya kujipatia zaidi ya asilimia 50 ya kura katika uchaguzi huo uliofanyika
tarehe 11 mwezi Agosti.
![]() |
mgombea wa UPDP, Hakainde Hichilema |
Chama cha UPND cha mpinzani wake
Hakainde Hichilema kilipinga matokeo hayo na kuwasilisha ombi la kuyapinga
mnamo tarehe 19 mwezi Agosti.
Sheria
inasema kuwa mahakama ya kikatiba ina siku 14 kusikiliza kesi hiyo.
Mwandishi wa BBC nchini
humo anasema kuwa muda huo ulikumbwa na mabishano na ilipofika siku ya Ijumaa
mawakili wa bwana Hichilema waliondoka katika mahakama wakidai ukosefu wa muda.
Mahakama hiyo iliendelea
mapema leo na kutangaza uamuzi huo.
Chanzo:BBC
Swahili
No comments:
Post a Comment