Bwana Trump(kushoto) akimsalimu Bi. Hillary mapema leo |
Wagombea
urais wa marekani, Bi Hillary Clinton
wa chama cha
Democratics na Bwana
Donald Trump wa
Republican wamechuana vikali
katika mdahalo uliofanyika
mjini New York
nchini humo usiku
wa kuamkia jumanne
ambapo katika
mdahalo huo masuala
ya sera za
ulipaji kodi, ajira
na uchumi yamechukua
nafasi kubwa huku
wagombea hao wakitupiana
maswali ya hapa
na pale.
Akiongea
kwa bashasha na
tabasamu Bi Hilary
Clinton wa Democratic
alimtaka Bwana Donald
Trump kuweka wazi
taarifa zake za
ulipaji kodi ili
kuwathibitishia wamarekani kuwa
atachangia kuinua uchumi
wa taifa hilo
na kuwalipa vizuri
watumishi wa umma,
mambo yalikuwa hivi, ’Tupo
na Bwana Trump
jukwaani jioni ya
leo tukijadili mambo
yanayolikumba taifa letu, ninyi
mnapaswa kutupima kwamba
ni nani kati
yetu anafaa kuwa
rais wa Marekani
lakini naamini mimi nitashinda kwa kura
yako Novemba nane’’
Kwa
upande wake mgombea
wa chama cha
Republican Bwana Donald
Trump amemjibu Bi
Hillrary Clinton wa
Democratic kwa kumtaka
aweke wazi jumbe
za barua pepe
zaidi ya 33,000
za serikali alizozitumia
kupitia anuani yake
binafsi wakati mwanamama huyo
akiwa waziri wa
mambo ya nchi
za nje wa Marekani na
hapa Bwana Trump
anasema “Tunahitaji
kuboresha uhusiano mzuri
ndani ya jamii
nchini hapa, ninasema
uhusiano mzuri nikiwa
na maana kuwa
kumbukumbu za hivi
karibuni zinathibisha kudorora
kwa uhusiano kati
ya polisi na
raia na wanaoathirika
zaidi ni wamarekani
weusi wenye asili
ya Afrika”.
Uchaguzi
wa rais nchini
marekani unataraji kufanyika
Novemba 8 mwaka
huu 2016 ambapo
hivi sasa kampeni
za ushindani kati
ya wagombea hao
wawili zimepamba moto
huku kura za
maoni zikionyesha kuwa
uungwaji mkono wa
Bwana Donald Trump
wa Republican na
ule wa Bi
Hillary Clinton wa
Democratic umekaribiana kwa
viwango kikubwa.
No comments:
Post a Comment