Bwana Ali Bongo |
Rais wa Gabon
Bwana Ali Bongo
Ondimba anataraji kuapishwa leo usiku wa jumanne kushika hatamu ya
uongozi wa nchi
hiyo ya Afrika
magharibi kwa muhula
wa pili baada
ya kumshinda mpinzani
wake Bwana Jean
Ping kufuatia uamuzi wa
mahakama ya kikatiba
nchini humo kutupilia
mbali shauri la
upinzani la kutaka
kura zihesabiwe upya
jumamosi iliyopita.
Jumuiya
ya kimataifa imelaani uamuzi huo wa mahakama
kwa kushindwa kufanya
kazi kwa uhuru
na usawa ambapo
akijibu tuhuma hizo
rais wa Gabon
Bwana Ali Bongo
Ondimba alikuwa na
machache ya kusema ‘’Jumuiya ya
kimataifa haikuja kupiga
kura hapa bali
watu wa Gabon
ndio waliofanya hivyo
nami nawajibika kwa
ajili yao’’
Taarifa
kutoka ndani ya
ofisi ya rais
nchini humo inadai
kuwa hafla ya
kuapishwa kwa Bwana
Ali Bongo itafanyika
jumanne hii mjini
Libreville nchini humo
lakini haijaweka wazi
ni muda gani
hasa tukio hilo
litafanyika.
No comments:
Post a Comment