Na
PETER MMBAGA
+255 656 859 045.
Kuna mwalimu wangu kwa jina la Emmanuel Maqway, nina sababu za mimi
kujivunia tafakuri hii aliwahi kutusisitizia kiujumla wanafunzi wake kuwa
usipokuwa mwanaminifu kwa vitu vidogo vidogo
hata vikubwa ni tatizo, sasa katika vitu vidogo wamefanikiwa, uwezo, utekelezaji na wana misimamo ya aina yake!
Nimemkumbuka Delilah kwenye Biblia, wasomaji biblia mtanielewa
hapa zaidi, kipindi mamia ya mijianaume ya kifilisti iliposhindwa kupambana na Samson, ikamtumia mwanamke kumwangusha mwamba. Fikiria mwanamke
mmoja tu!
Kisa cha kanisa la
Anglikana kuanzishwa, ilikuwaje?Mwaka 1527,
Mfalme Henry VIII wa Uingereza aliwaza penzi la Anne Boleyn aliyekuwa msaidizi wa mkewe Catherine wa Aragon na kutaka
kumuoa, kanisa Katoliki likaweka
pingamizi kwakuwa talaka haruhusiwi, Henry VIII akaona dola kubwa ya Uingereza
haiwezi ingiliwa na dola ya Roma, akajitoa
rasmi ndani ya ukatoliki na kuupiga marufuku Uingereza. Mfalme Henry VIII akampa
mkewe talaka na akawa kiongozi mkuu wa kanisa la Anglikana. Twende taratibu utanielewa, nguvu ya mwanamama hiyo!
Hata dola ya Israeli kugawanyika
kusini na kaskazini moja ya sababu ni
matokeo ya mfalme Suleimani
kuwa na “masuria” ubavuni mwake walitokea Misri waliomletea miungu ya
Baali kipindi cha malkia wa Sheba akamuasi Mungu
wa kweli! “Masuria” hao?
Maajabu ya wanawake ni
wavumilivu, jasiri, na uwezo wa hali ya juu sana ila ni watu wa kupenda ushauri, kujaliwa na kusikilizwa, usiyafanye yote
hayo na usiombe achoke, akasirike na
yamfike, utajuta! Utajua yeye ni
mwanamke, kiumbe chenye nguvu!
Dunia ina mambo ila
wanadamu wana mambo ya ajabu, na ukistaajabu ya Musa, utayaona ya firauni,
haitii shaka unapoona kuhusu
kisichotarajiwa kabisa lakini kuna wanaojua kabisa kitatukia. Twende taratibu,
utanielewa!
Kuna jamaa anaitwa Pablo Reyes pale Marekani kashajijengea
umaarufu kwa alichokiandika desemba mwaka jana kupitia ukurasa wake wa facebook, kuwa mwaka 2016 tulioko sasa, kuna vifo vya watu
maarufu duniani kama mpiganaji wa
mtaani, Kimbo Slice, mwanamuziki
mwingereza Prince, mwanandondi Muhammad Ali, Gorilla, na nchi ya
Marekani itashuhudia mauaji ya kinyama(mfano mdogo, polisi na watu weusi),
vyote hivyo vimeshatokea. Utabiri umetimia!
Kwa maelezo yake
kilichobaki ni kifo cha Donald Trump,
mgombea urais Marekani kupitia chama cha Republican
na mwanamama Hillary Clinton,
mgombea kupitia chama cha Democratic
kuwa rais wa kwanza mwanamke nchini
Marekani, utabiri wake utatimia?
Mgombea urais Marekani kwa chama cha Democratic, Mama Hillary Clinton. |
Unajua Wamarekani kesho
Jumanne ya novemba 8, wanaamua nani awe
Rais?, na Pablo alipotaja mwanamama kuiongoza Marekani, ndipo jicho
lilipojikita, hapohapo Washington D.C, jirani ni shirika la fedha duniani(IMF) kuna mwanamama mwenye misimamo yake wa kifaransa anaitwa Christine Lagarde anakwenda kwenye muhula wa pili wa miaka mitano baada ya kuongoza taasisi
hiyo yenye nguvu duniani toka 2011, masharti magumu yaliyobadilisha siasa za
dunia ya tatu yaliletwa nao!
Bosi wa IMF, Mama Christine Lagarde. |
Malkia wa Uingereza, Elizabeth II anaongoza “sakata” akimpa nguvu ya kiutendaji, Theresa May ambaye kaikamata nafasi ya
Waziri Mkuu hivi karibuni , pale Ujerumani yalikwishatimia kwa kansela Angela Merkel, Anasubiri kwa
hamu kwakuwa wamepata nguvu ya pamoja na anagombea kwa msimu mwingine wa nne
huku chama chake cha CDU(Christian
Democratic Union) kikishika nafasi ya tatu nyuma ya chama cha Demokrasia ya kijamii(SDP) na Alternative fur Deutschland(AfD) kwenye chaguzi za majimbo, waandamaji kumsakama
wakitaka aachie ngazi kwa kuruhusu wahamiaji mwaka 2015 nchini Ujerumani tena siku ya kumbukumbu ya miaka 26 ya muungano wa Ujerumani “Germany
Unity Day” mapema Oktoba 3, mwaka huu ila hajapata kigugumizi na vyama vyote
vitamsapoti mwakani 2017 kwenye
uchaguzi. Kutilia mkazo hasa ndani ya EU
(Umoja wa Ulaya) kuwa na sauti ya
mamuzi kutosikiliza sauti ya nchi moja kutokana na ukubwa. Moja kwa moja mfano ni Uingereza, “mzizi” wa yeye mpka kuja
kujitoa EU. “Aliona haiwezekani nchi ndogo kama Ugiriki anaisaidia bajeti yake
halafu wawe na maamuzi sawa” nawaza hivyo, Ukifuatilia kwa undani wanahusika pia
kinamama.
Mahakama ya kiuhalifu ya kimataifa (ICC) ina mwanamama Mgambia, mwendesha
mashtaka mkuu(The Hague), anaitwa Fatou
Bensounda ni mkakamavu mwenye maamuzi ya kijasiri asingewekwa pale, kuna kitu cha ziada anacho kuanzia
alipoiongoza wizara ya Sheria Gambia kabla ya kuteuliwa mwaka 2012.
Mwendesha Mashtaka ICC, Mama Fatou Bensounda. |
Umoja wa Mataifa(UN) daah! “wamechana mkeka” kwa mwanamama kurithi
nafasi ya Ban Ki-Moon, mreno Antonio Gueterrez kachukua, japo changamoto aliiona ukiangalia nafasi ya wagombea 12, nane
walikuwa ni wanawake wa shoka na “nilibet” kinamama watang’ara kama Christiana Figueres, Irina Bokova, au Hellen
Clark na baadhi yao wapo kwenye “ukubwa” wa mashirika ndani ya UN, bado
tutaona “impact” yao.
Unajua ubongo wangu
unawaza nini? kwenye zama zakwenye “fifty-fifty”
haya maswala ya kutafuta usawa na haki kwenye mfumo dume ndiyo sauti hizi
nyororo utapokwenda kufurahia hotuba na maamuzi zao! Ndio utazifurahia, Taratibu
utanielewa!
Harakati za kuzuzururisha
akili mataifani kwa tafakuri na Wabasi wangu, tunaoamini kwenye falsafa za Ubasi, Amani akadai “Msuguano
hatarishi wenye harufu ya chechendani ya miaka kumi inaweza tokea kupitia hili
kwani kina Putin na wenzake kupinga sera za kihafidhina watazidi kubisha ila
hisia zitawapanda kwa wao kuona sauti nyororo zinawapelekesha”, kati ya wale
nane mmoja angechukua, “anyway” UN
wamechana mkeka!
“Pia sauti nyororo
zitaona zinapingwa sana nazo zitaingiza hisia kuonyesha dunia maamuzi yao yalivyo ili heshima
ionekane”.
“Eti msuguano hatarishi ndio utatokea? Hasa kwenye miaka kumi, wakati
wengi wa hawa viongozi watatawala kwa vipindi visivyozidi vinne?” Akajibu mbasi
mwingine kwa jina la Mlang’a.
Wakati tafakuri
ikiendelea mara kuna bajaj ikapita na
bonge la mziki “me and you na, perfect
combo, eeh na perfect combo….”
“Perfect Combo”, ndio ameimba mwanarapu Joh
Makini wimbo aliomshirikisha Mnigeria Chidinma,
nikawaambia wabasi wangu kuwa kweli hii itakuwa “Perfect Combo” kwakuwa maamuzi, misimamo, dukuduku,
matarajio yao yanaelekea kwenye mrengo mmoja wa kusaidia kizazi cha kinadada
kwa kuwatia nguvu ya kujiamini kutoyumbishwa na misimamo ya mfumo dume
iliyokwepo, na hata ukisikiliza kwa umakini hotuba zao wanavyojielezea na hasa usawa
wa kijinsia na haki unavyojielekeza kuna mabadiliko watafanya, tena makubwa ya
kimapinduzi.
Ni suala sio la kipuuzi
au kupepesa macho kuukataa ukweli, bado wanaume na hata baadhi ya wanawake tunaamini
nguvu ya hoja kuhusu mfumo dume, waaminio biblia wanaamini
mstari usemayo “……..kweli itakuweka huru”, wengi wanatetea kwenye umma kinafiki
wakikutana sirini mfumo dume ndio hoja, Twende taratibu, nadhani unaanza kunielewa!
Kinamama hawa wanaunganisha “nguvu” ya pamoja ukizingatia nchi na taasisi wanazotoka
nazo zina “nguvu” za kuitawala dunia kwa masharti yao itakavyo, wana mamlaka
kubwa, wataalamu wa kutosha, na uchumi mkubwa ambao ndio “silaha” ya kuteka
dunia ya tatu, japo sio nchi zote zinaweza kutingishwa!
Kweli sio nchi zote zinaweza kutingishwa? Hapa ndipo kwenye ule msuguano hatarishi utakao
leta cheche mbasi wangu aliounena, na nisiuopenda kuuona ila, unaweza kutokea.
Je, misimamo ya mataifa na taasisi zao kwenye kutoa maamuzi na
kuingilia mataifa inapingwa na imeathiri vipi dunia hasa mataifa yasiyo na udini na huu unaoitwa ubeberu? Hapa namuwaza sosholisti Vladimir Putin wa Urusi, Kim Jong-un wa Korea Kaskazini na Xi Jinping wa China. Kwanini msuguano utakuwa mkubwa sana na kupelekea msuguano
hatarishi wenye cheche?
Sauti nyororo kutoa “speech”
nzito kutoakana na mataifa na taasisi nzito, na ndipo napata kigugumizi kwa
kuwaona wapingaji hawa kutoka mataifa haya yanayokataa kwa uwazi ubeberu nawazungumzia Korea Kaskazini, China, Cuba na Urusi. Mnanielewa sio?
Je, Waarabu hasa Mashariki ya kati na misimamo yao ya kidini na utamaduni wao,
kwenye hii ‘fifty-fifty” na “order”
ya sauti nyororo wataelewa, kwakuwa tu,
kule kwao hata gari kinamama hawaruhusiwi kuendesha!
Na nguvu ya utekelezaji
wa sera zao wanaweza kuzipenyeza kwa namna yoyote ile hata kwa nguvu, angalia
Uganda kusitishiwa misaada kisa kupinga sheria za ndoa ya jinsia moja, misaada
wamekata!
Sio hatuwezi kusimama
bila wao, ila mifumo ilishazoea hiyo hali hivyo lazima mkatae huku
haijasitishwa, hapo sitaki kupagusia kwakuwa sio “engo” husika. Akili haipo
sawa“ UN wamechana mkeka”. Sio “kesi”, kwanini?
Maamuzi ya dunia yanategemea
sana haya mataifa na taasisi hizi, kumbuka suala la demokrasia na mfumo wa
vyama vingi kwenye dunia ya tatu
uliletwa na shirika la fedha duniani (IMF)
kupitia mpango waliouita “Structural
Adjustment Programme”, zaidi Marekani ndiye mama wa sauti za kutaka mambo
yaende atakavyo, siasa ya dunia kaikalia na anaijua, nchi na taasisi zenye nguvu kimaamuzi na utekelezaji duniani
zina watu hawa, kwenye nafasi ya wanawake wenye nguvu duniani sita bora Miss Lagarde, Angel Merkel na Hillary
Clinton wamo.
Sasa sidhani kama hawa
wapingaji wa sera za mabeberu, watarudisha kuni nyuma kutochochea moto, upande
wa pili ukiweka mkaa! Mnanielewa sio?
Sio kitu cha kushangaza kwenye mifumo yenye
mizizi ya kidini, kikabila, kijamii na mazoea vilikuwa vinapinga na havioni
nafasi ya mwanamke kwenye mambo makubwa, jiulize ile presha ya kupinga itaongezeka
au kupungua kwa asilimia ngapi?
Sitamani kuzidi kuziona ghiliba za nchi wanachama wa ubeberu
zilivyo na ushirikiano toka muda mrefu. Tangu enzi za vita ya pili ya dunia,
Marekani na Uingereza huku taasisi ya IMF na UN zote zipo Marekani na zaidi
yule mwanamama kiongozi wa IMF ni mfaransa, sapoti kubwa inaongezeka!
Mnanielewa sasa? maslahi
na maamuzi nguvu ya kura “veto”
ndani ya UN, na hasa ndani ya baraza la usalama ambapo China na Urusi wapo ila
Marekani, Uingereza na Ufaransa nao ni
memba wa kudumu na jinsi nchi hizi zilivyo na ukaribu watazidi kulekeza
nguvu kwenye maslahi yao kidunia na upande wa pili ni dhahiri hawatokaa kimya.
Ninapoangalia nguvu ya
sauti nyororo ipenyayo masikioni bila kutumia nguvu, ila maneno yapenyanyo
yanaweza kuwa na zuri au baya, ukicheza tu huponyoki. Ila masoshalisti na wenye
“imani kali” watapindua unyororo wa sauti hiyo, na sauti hizi“zitajiongeza” kwa
kutumia hisia, nini kitatokea? Msuguano hatarishi!
Bado natafakari baada
ya miaka nane mpaka kumi ya vipindi vya sauti hizi nyororo karibu zote
zikiachia ngazi. Dunia itaingia kwenye hatua kuelekea historia, kwa wale “Standpoints
feminists” wanayoiamini, japo UN wametuchania mkeka mimi na Wabasi
wangu katika fikra pana, mwanafalsafa E.Maqway
na ndugu Amani.
“End will justifies the meaning” Waingereza husema!