Friday 16 September 2016

NUKUU KUNTU: MISIMAMO YENYE TIJA IKO VIPI?


"Katika siasa, kuwa na misimamo yenye tija ni msingi mkuu. Nyimwa kila kitu lakini usinyimwe misimamo katika masuala ya msingi. Na kwa hiyo, katika ndoa, biashara, shughuli yoyote, taaluma na maisha ya kila siku, msimamo ni nguzo yako kuu! Unapokuwa na misimamo yenye tija inahitajika tu wenzako waijue na waiheshimu, huna haja kutumia nguvu kubwa sana kuionesha. Usiogope kuwa na msimamo wenye tija kwenye kila jambo la msingi".                                                                                                   

Julius S. Mtatiro, kiongozi  mwandamizi wa chama cha CUF na mchambuzi wa masuala ya kisiasa.

FUNNY FACT:SMARTPHONE INAPOLETA HESHIMA NYUMBANI

Kwa wale washikaji na masista duu ambao wazazi wao wakali sana na hawasikilizwi, hasa DINGILII, FUNNY FACT ni kuwa muda pekee ambao unaweza kumzoea, kumpa masharti, kumbishia, kumuonya na kumshauri akakusikiliza  ni pale unapomfundisha kutumia vifaa vya teknolojia hasa simu za SMARTPHONE!
Wanakuwaga wapole sana kama wamemwagiwa maji vile!

Binti akimfundisha mzazi wake kutumia simu


FUNNY FACT: KWENDA DARASANI KUNA FAIDA


Mbwa koko wawili walikuwa wanasaka chakula kwenye jalala, mara ikapita Land Rover ya FFU na ndani yake kuna mbwa wa polisi. Mbwa koko mmoja akaangalia kwa uchungu kisha akamwambia mwenzie, 'Unaona wenzetu waliosoma, wale wanaenda kazini.

SOMO: Elimu ina nafasi kwenye maisha ya mtu hasa ukiitumia vyema.







TRUMP AANZA KUAMINI KUWA OBAMA KAZALIWA MAREKANI



Hilo limetokea  baada ya Donald Trump kuanza kuamini Obama amezaliwa Marekani ambapo mgombea huyo kwa mara nyingine alisisitiza kwamba hayuko tayari kuamini kwamba Bw Obama alizaliwa Marekani. Akihojiwa na gazeti la Washington Post, Bw Trumo alikataa kusema Bw Obama alizaliwa Marekani na badala yake akasema hangejibu swali hilo.
Ofisi ya kampeni ya mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump imetoa taarifa ikisema sasa anaamini Rais Obama alizaliwa nchini Marekani.
Trump huchukuliwa mwanzilishi wa kundi lijulikanalo kama "birther movement", ambalo huamini Rais Barack Obama hakuzaliwa katika jimbo la Hawaii, na kwa hivyo hakufaa kuhudumu kama rais wa Marekani.
Anasema taarifa hiyo iliyotiwa saini na mshauri mkuu wa Trump, Jason Miller hata hivyo si kwamba anakubali makosa.
Badala yake, Miller aliweka lawama kwa Hillary Clinton na kundi lake la kampeni la mwaka 2008, ambapo Bi Clinton alikuwa anashindania tiketi ya chama cha Democratic na  Obama.
Hakuna ushahidi wa kumhusisha Bi Clinton na kundi la Birther. Akijibu, Bi Clinton alisema kupitia Twitter kwamba mrithi wa Rais Obama "hawezi kuwa mtu aliyeongoza kundi la ubaguzi wa rangi la Birther".
Wanaopinga kwamba Obama alizaliwa Marekani wamekuwa wakisema alizaliwa Kenya (babake Obama alikuwa Mkenya).
Taarifa katika magazeti kadha ya Marekani zinaashiria uvumi huo ulienezwa mwaka 2008 na wafuasi sugu wa Bi Clinton ilipoanza kudhihirika kwamba mwanamke huyo hangeshinda uteuzi wa chama cha Democratic.
Madai hayo baadaye yalifufuliwa na wafuasi wa mgombea wa Republican John McCain alipoanza kuachwa nyuma na Obama kwenye kura za maoni, tovuti ya Fact Check imeripoti.
Obama
Trump alianza kujihusisha na suala hilo kabla ya uchaguzi mkuu wa 2012.
Aprili 2011,  Trump alimtaka Obama kuonyesha hadharani cheti chake cha kuzaliwa, wito ambao uliungwa mkono na wanasiasa wengi wa Republican akiwemo aliyekuwa gavana wa Alaska Sarah Palin.
Mwaka 2012 mgombea wa wakati huo wa Republican Mitt Romney alirejelea madai hayo kwenye mkutano wa kampeni Agosti mwaka huo.


Chanzo:BBC Swahili

TEKNOLOJIA INAVYOKWENDA NA WAKATI KWA UJIO WA 'APPLE LIGHTNING'

Kampuni ya Apple imeshaingiza aina ya simu zake mpya iPhone7 kwenye matangazo ya biashara na zimeanzwa kuuzwa  septemba 16, 2016.
Huku kampuni hiyo ikiwa imethibitisha aina hiyo mpya simu haitakuwa na tundu la kawaida la kifaa cha kusikilizia sauti yaani "headphone", ila itatumia vishikizi " adapter" vilivyobatizwa jina la kiteknolojiia la 'Apple Lighting' japo kampuni ya Moto Z na vifaa vya LeEco  ya huko China ilizindua 'earphone'  bila kisikizia sauti mapema mwaka huu hivyo kutangulia kwa ugunduzi.
Sasa ipo hivi, nikujuze?
Kampuni ya Apple imekuwa na "falsafa" ya kuacha mapema teknolojia wanayodhani imepitwa na wakati.
Hivyo kwa kukujali msomaji wangu nakuletea miongoni mwa orodha ya teknolojia zilizopitwa na wakati kwenye sekta hii ya mawasiliano  na vifaa hamisha data tukielekea kwenye teknolojia mpya:

Floppy Disk drive(1998), Dial up modem(2005), CD/DVD drive(2008), 30-pin connector(2012) na USB 3 ports(2015).