Sunday 4 September 2016

TAIFA STARS HAINA REKODI DHIDI DHIDI YA SUPER EAGLE

Taifa Stars imeshindwa kuvimba ili kuitafuta rekodi iliyowekwa na Wanaigeria katika mechi nane za kimataifa walizokutana.
Mchezo wa jana uliochezwa uwanja wa Akwa Ibom huko Nigeria, ulikuwa wa mwisho  wa kundi G katika hatua za kufuzu AFCON 2017 huko Gabon dhidi ya Super Eagles, mchezo ulikwisha huku mshambuliaji kijana  wa Man City, Kelechi Iheanacho akitupia dakika ya 77.
Kwa goli hilo ndoto za Taifa Stars iliyokuwa ikiongozwa na nahodha wake Mbwana Samatta anayekipiga klabu ya Genk ya huko Ubelgiji ziliishia kuambulia historia ya sare ya mechi tatu na kufungwa mechi tano(ya jana ikiwemo) hivyo hakuna  "ubabe" wowote kwa Taifa Stars dhidi ya Super Eagle iliyoongozwa na kiungo mkongwe Mikel Obi na mshambuliaji machachari Ahmed Mussa. 

Mafarao wa Misri ni kati ya waliopenya ndani ya kundi la G.

No comments:

Post a Comment