Monday 5 September 2016

POGBA HAKWENDA MAN U KUCHEZA TU, KUNA BIASHARA TAYARI IMESHANUFAISHA WATU!

Mourinho(kushoto) na Pogba
Ilionekana biashara kichaa kwa  kocha Arsene Wenger wa  "The Gunners" akasema haiwezi tokea yeye kufanya kitu kama hicho kwenye ulimwengu wa soka. Ndiyo kuna biashara ya ziada nyuma zaidi ya Jose Mourinho kutaka huduma ya uwanjani Man U. Si bure kufanya vile, kuna watu waliwaza.
Wadhamini wa Man U, Adidas na Chevrolet pamoja na wengineo wana siri zao, siri?
Sasa ndivyo biashara imeshafanyika, Agosti 9, Paul Pogba kiungo mfaransa alivunja rekodi ya kuwa mshambuliaji bora duniani kwa kusajiliwa kwa pauni milioni 100, balaa ni kuwa wiki tatu za mwanzo pesa imerudi kwa kuuza jezi pekee, pauni milioni 200 Man U washazitia mfukoni na wanamalizia deni lao kwa Juve  taratibu.
Achana hiyo mwenzake aliyesajiliwa toka PSG, Zlatan Ibrahimovic wiki ya kwanza tu kwenye mauzo ya jumla Man U walilamba pauni milioni 76. Zlatani akasema jezi yake itauza kurudisha hela walizomnunulia Pogba!
Unajua mawazo yao(Adidas na Chevrolet) ? Kibiashara tu kwenye mitandao ya kijamii kabla na baada ya kumsajili walisharudisha hela, cheki lile liubunifu #POGBACK si snapchat, tweeter, Instagram, blogs, websites, na facebook. Dunia ya kidigitali!  Unajua soka la sasa linaangalia nini?
Mchezaji ataingiza shilingi ngapi kwenye mauzo ya jezi, matangazo ya televisheni na mchezaji ana mvuto?
Mikataba ya udhamini  klabu itapata, unadhani Man U ni "wajinga" kupelekea kukosa karibu  dola milioni 100 kila mwaka toka kwa Adidas. Adidas walitaka kijana mwenye "mvuto" kuwepo kwenye picha za matangazo. Sababu moja nzito! Magari ya Chevrolet yalikuwa hayauzi sana UK na Ulaya, ishu kubwa ya kwanza waliyofanikiwa ilikuwa ni kumshusha Pogba kwenye uwanja wa mazoezi wa AON(AON Training Centre) ndani ya ndinga ya kifahari  kali mpya ya Chevrolet Camaro(new model). Utamaduni wa zamani ulizoeleka kumtangaza mchezaji kupitia "press conference", sasa kuna ishu ya ziada za kufanya matangazo ya biashara zingine, mambo yanabadilika.  Kwasasa biashara ya Chevrolet imeanza kukua vyema Uaya, sababu kwenzi nayo hiyo!
Pogba akiwa ndani ya Chevrolet Camaro akiingia uwanja wa mazoezi wa AON siku akitambulishwa

Kwa uchache huo, Pogba anavyo vyote. Nani asimununue japo sio mkali kivile, enzi za kina Andre Pirlo huyu Pogba ana uwezo gani? kibaya zaidi kilichomkimbiza toka Man U  2012 kwenda Juve ni "jitu"  likiwa uwanjani ila sura ya upole, kiungo Paul Scholes, unadhani Sir Alex Ferguson hakuwa na akili.
Zaidi usajili wake hatujaujadili sana kwakuwa ni "kijana mweusi", ubaguzi wote kwenye michezo tena Uingereza kupenda vyao, lakini akachukuliwa kwa bei hiyo!
Unajua kinachotokea mwaka huu wa fedha, Man U watapata faida zaidi  ya dola milioni 665 kwa mwaka 2015/2016 ukiweka pembeni na  pesa walizomsajili Pogba ambazo pauni milioni 100 na " kiasi" fulani ziada ni sawa na  "turnover" ya  19.5%, hawana hasara hivyo!

Adidas wanaelewa biashara ikoje wikiendi ya septemba 10, kuna Manchester derby kati ya Man U na Man City, tayari washatoa viatu vipya  aina ya "Adidas ACE16+Purecontrol Viper Pack" kwa kijana wao Pogba kwajili ya matangazo ni vya teknolojia ya hali juu asikubishie mtu!
Fedha zimerudi ni muda wa biashara ya uwanjani kinachofuata. Si kucheza na kuleta makombe OT tu, huu ni muda wenye akaunti  zenye "maono" zimekwishanona.

No comments:

Post a Comment