Thursday 8 September 2016

NUKUU KUNTU: UMUHIMU WA KUJADILI MASUALA YA KITAIFA KWA UHURU


Baba wa Taifa Mwalimu na Ndugu Julius K. Nyerere.
"Kwanza, ni lazima kurudisha tena uhuru na utaratibu wa kujadili masuala yote makubwa na kufikia uamuzi baada ya mjadala. Viongozi wetu hivi sasa wanaogopa kutumia nguvu za hoja ili kutoa maamuzi muhimu. Kwa sasa wanatumia hila zaidi kuliko hoja. Vitisho kwao ni mbinu rahisi zaidi kuliko adha ya kutumia akili na kupata hoja safi ya kumjibu mpinzani katika mjadala. Viongozi hawa wakipewa nafasi watatumia hoja ya nguvu tu; na hawatakuwa  na haja ya kutumia akili kichinichini baadhi yao tayari wameanza kutumia hoja ya vitisho na kama tukiacha utamaduni wa woga ukazagaa tutakuwa tunakarbisha udikteta".

Maneno kuntu ya Mwalimu na Ndugu Julius K.Nyerere(1914-1999), kwenye kitabu cha UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA. Uk. 45/46.

No comments:

Post a Comment