Thursday 8 September 2016

FIFA YAWATIA 'LOCK' YA KUTOSAJILI REAL MADRID NA ATLETICO MADRID

Kocha wa Atetic Madrd Diego Simeone (kushoto) na kocha wa Real Madrid Zindine Zidane
Kamati ya rufaa ya shirikisho ya soka duniani, FIFA imeweka wazi kuwa imekataa rufani ya Real Madrid na Atletico Madrid  kwa kuvunja sheria ya kimataifa ya michezo isiyo ruhusu vilabu kusajili wachezaji chini ya miaka 18.
Vilabu vyote vinatakiwa vitumikie adhabu ya  kutosajili hivyo kutokuwa na kandarasi na mchezaji yoyoTe kitaifa na kimataifa kwa misimu  miwili mfululizo kuanzia sasa.NHivyo klabu hizo zitatumikia adhabu  mpaka Januari, 2018.

Atletico Madrid wamepigwa faini ya euro 822,000 na Real Madrid waO wamelimwa euro 329,000. Japo taarifa toka Atetico Madrid zinadai watakata rufaa juu ya hilo.
Kwa upande wa wapinzani wa Barca walikutwa na dhahama hiyo mwaka 2014.

ISHU ILIKUWA VIPI?
Real Madrid  wamekutwa na hatia baada ya uchunguzi wa FIFA ulionyesha wAlifanya vitendo hivyo mwaka 2005 mpaka 2014, huku Atletico toka mwaka 2007 na 2014.
Kutokana na taarifa hizo kutakuwa na utata kwa Madrid kumpata kipa wa Man U wanayemtolea udenda, na kwa pande Atletico Madrid watakosa nafasi ya kupata mbadala wa  Antonie Griezmann anayetarajiwa kung'oka..

Hii ndio “PRESS REEASE“ YA FIFA

The FIFA Appeal Committee has decided to reject the appeals lodged by Spanish clubs Atlético de Madrid and Real Madrid and to confirm in their entirety the decision rendered by the FIFA Disciplinary Committee in the respective cases relating to the protection of minors.
As such, both clubs are to serve a transfer ban that prevents them from registering any players at national and international level for the next two complete and consecutive registration periods for breaching articles 5, 9, 19 and 19bis as well as annexes 2 and 3 of the Regulations on the Status and Transfer of Players (the “Regulations”). The transfer ban applies to each club as a whole – with the exception of the women’s, futsal and beach soccer teams – and does not prevent the release of players.
Additionally, Atlético de Madrid and Real Madrid have been fined CHF 900,000 and CHF 360,000 respectively, while both clubs have been issued with a reprimand and a warning and given 90 days in which to regularise the situation of all minor players concerned.
The grounds of the decisions taken by the FIFA Appeal Committee were communicated to the parties concerned today.


FUNNY FACT: KUNA UNAFUU WA KUCHEPUKA NA MKE WA MTU?

Eti sababu 11 zenye unafuu kuchepuka na mke mtu, usiichukulie poa sana, kwasababu ukichukulia poa sana, FUNNY FACT ni kuwa kuna  sababu  nyingi zenye umuhimu. Zicheki zifuatazo;
1. Hawezi kuomba kodi ya nyumba maana mume wake ndio analipa.
2. Hawezi kuomba umnunulie gari mume wake atahoji.
3. Hawezi kutaka umnunulie vitu vya garama sijui iphone 7 mpya au Samsung galaxy.
4. Hakugandi kama luba, mara text,mara calls sijui ujinga gani maana mumewe atamsanukia.
5. Hawezi kukuuliza maswali ya kijinga jinga kama hivi kweli unanipenda, unanijali au hutoniacha.
6. Hawana usumbufu wa vibomu visivyo na maana, eti mara sina vocha, niungie kifurushi kwako hayo hayapo.
7. Wanapatikana wanapohitajika na kama kabanwa anatoa reasonable excuses.
8. Hakuulizi utamuoa lini na malalamiko ya kijinga kijinga.
9. Hawana shida kushare mwanaume, yaani hakubani  kama una mpenzi wako mwingine anakuruhusu uwe nae ili mradi atakapokuhitaji upatikane bila shida.
10. Ukiwa na shida ndogo ndogo anakusaidia kutatua.
11. Ukimpa mimba anamsingizia mume wake
UKISHIKWA KWENYE MKONO WA MUMEWE MIMI NITAKUWA NIPO MTANDAONI.


ANGALIZO:  Jiheshimu, mke wa mtu  si wa kuchezea,  kimaadii si jambo jema na  si  ustarabu! 
                     

NUKUU KUNTU: UMUHIMU WA KUJADILI MASUALA YA KITAIFA KWA UHURU


Baba wa Taifa Mwalimu na Ndugu Julius K. Nyerere.
"Kwanza, ni lazima kurudisha tena uhuru na utaratibu wa kujadili masuala yote makubwa na kufikia uamuzi baada ya mjadala. Viongozi wetu hivi sasa wanaogopa kutumia nguvu za hoja ili kutoa maamuzi muhimu. Kwa sasa wanatumia hila zaidi kuliko hoja. Vitisho kwao ni mbinu rahisi zaidi kuliko adha ya kutumia akili na kupata hoja safi ya kumjibu mpinzani katika mjadala. Viongozi hawa wakipewa nafasi watatumia hoja ya nguvu tu; na hawatakuwa  na haja ya kutumia akili kichinichini baadhi yao tayari wameanza kutumia hoja ya vitisho na kama tukiacha utamaduni wa woga ukazagaa tutakuwa tunakarbisha udikteta".

Maneno kuntu ya Mwalimu na Ndugu Julius K.Nyerere(1914-1999), kwenye kitabu cha UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA. Uk. 45/46.

Monday 5 September 2016

FUNNY FACT: MOURINHO BETRAYED CHELSEA

kipa Petr Czech

Jose Mourinho came to Chelsea to destroy them while waiting for United job. It's FUNNY FACT you can't believe, he sold Juan Mata,  De bryune, Ashley Cole, Petr Czech, Andre Schurlle, Felipe Luiz, Salah( total of 9 quality players) and bought Baba, Pappy.....(whatever), Cuadrado, Eto'o to replace them. Did this man ever had a good intention for Chelsea?
Mohamed Salah katika mja ya mapambano yake
In 2 months.
He bought Bailly, Henrick, Ibramohivic and Pogba for United and use Juan Mata in first eleven while he dropped him at Chelsea for the reason  that he can't fit in his football philosophy.
Juan Mata(mwenye jezi) na Mourinho(katikati) wakiwa Man U

NDEGE ZILIZOBEBA MIRAA MARUFUKU SOMALIA

Serikali ya Somalia imesitisha kwa muda ndege zote zinazoingiza miraa kutoka taifa jirani la Kenya.
Biashara hiyo ina thamani ya mamia ya mamilioni ya madola kila mwaka.
Waziri wa maswala ya anga nchini Somalia Ali Ahmed Jama Jangali,amesema kuwa marufuku hiyo itaanza kutekelezwa siku ya Jumanne lakini hakutoa maelezo zaidi.
Miraa ni maarufu sana nchini Somalia ,ambapo hutafunwa kwa saa kadhaa na hutumika kusisimua mwili .
Miraa mingi katika sehemu ya kusini na katikati mwa Somalia hutoka nchini Kenya.
Haikuzwi nchini Somalia.
Miraa hutumika na imepigwa marufuku nchini  Tanzania, Marekani pamoja na mataifa kadhaa ya Ulaya.



Chanzo:BBC Swahili

POGBA HAKWENDA MAN U KUCHEZA TU, KUNA BIASHARA TAYARI IMESHANUFAISHA WATU!

Mourinho(kushoto) na Pogba
Ilionekana biashara kichaa kwa  kocha Arsene Wenger wa  "The Gunners" akasema haiwezi tokea yeye kufanya kitu kama hicho kwenye ulimwengu wa soka. Ndiyo kuna biashara ya ziada nyuma zaidi ya Jose Mourinho kutaka huduma ya uwanjani Man U. Si bure kufanya vile, kuna watu waliwaza.
Wadhamini wa Man U, Adidas na Chevrolet pamoja na wengineo wana siri zao, siri?
Sasa ndivyo biashara imeshafanyika, Agosti 9, Paul Pogba kiungo mfaransa alivunja rekodi ya kuwa mshambuliaji bora duniani kwa kusajiliwa kwa pauni milioni 100, balaa ni kuwa wiki tatu za mwanzo pesa imerudi kwa kuuza jezi pekee, pauni milioni 200 Man U washazitia mfukoni na wanamalizia deni lao kwa Juve  taratibu.
Achana hiyo mwenzake aliyesajiliwa toka PSG, Zlatan Ibrahimovic wiki ya kwanza tu kwenye mauzo ya jumla Man U walilamba pauni milioni 76. Zlatani akasema jezi yake itauza kurudisha hela walizomnunulia Pogba!
Unajua mawazo yao(Adidas na Chevrolet) ? Kibiashara tu kwenye mitandao ya kijamii kabla na baada ya kumsajili walisharudisha hela, cheki lile liubunifu #POGBACK si snapchat, tweeter, Instagram, blogs, websites, na facebook. Dunia ya kidigitali!  Unajua soka la sasa linaangalia nini?
Mchezaji ataingiza shilingi ngapi kwenye mauzo ya jezi, matangazo ya televisheni na mchezaji ana mvuto?
Mikataba ya udhamini  klabu itapata, unadhani Man U ni "wajinga" kupelekea kukosa karibu  dola milioni 100 kila mwaka toka kwa Adidas. Adidas walitaka kijana mwenye "mvuto" kuwepo kwenye picha za matangazo. Sababu moja nzito! Magari ya Chevrolet yalikuwa hayauzi sana UK na Ulaya, ishu kubwa ya kwanza waliyofanikiwa ilikuwa ni kumshusha Pogba kwenye uwanja wa mazoezi wa AON(AON Training Centre) ndani ya ndinga ya kifahari  kali mpya ya Chevrolet Camaro(new model). Utamaduni wa zamani ulizoeleka kumtangaza mchezaji kupitia "press conference", sasa kuna ishu ya ziada za kufanya matangazo ya biashara zingine, mambo yanabadilika.  Kwasasa biashara ya Chevrolet imeanza kukua vyema Uaya, sababu kwenzi nayo hiyo!
Pogba akiwa ndani ya Chevrolet Camaro akiingia uwanja wa mazoezi wa AON siku akitambulishwa

Kwa uchache huo, Pogba anavyo vyote. Nani asimununue japo sio mkali kivile, enzi za kina Andre Pirlo huyu Pogba ana uwezo gani? kibaya zaidi kilichomkimbiza toka Man U  2012 kwenda Juve ni "jitu"  likiwa uwanjani ila sura ya upole, kiungo Paul Scholes, unadhani Sir Alex Ferguson hakuwa na akili.
Zaidi usajili wake hatujaujadili sana kwakuwa ni "kijana mweusi", ubaguzi wote kwenye michezo tena Uingereza kupenda vyao, lakini akachukuliwa kwa bei hiyo!
Unajua kinachotokea mwaka huu wa fedha, Man U watapata faida zaidi  ya dola milioni 665 kwa mwaka 2015/2016 ukiweka pembeni na  pesa walizomsajili Pogba ambazo pauni milioni 100 na " kiasi" fulani ziada ni sawa na  "turnover" ya  19.5%, hawana hasara hivyo!

Adidas wanaelewa biashara ikoje wikiendi ya septemba 10, kuna Manchester derby kati ya Man U na Man City, tayari washatoa viatu vipya  aina ya "Adidas ACE16+Purecontrol Viper Pack" kwa kijana wao Pogba kwajili ya matangazo ni vya teknolojia ya hali juu asikubishie mtu!
Fedha zimerudi ni muda wa biashara ya uwanjani kinachofuata. Si kucheza na kuleta makombe OT tu, huu ni muda wenye akaunti  zenye "maono" zimekwishanona.

WAKALA WA YAYA AMBWATUKIA PEP GUARDIOLA

Kiungo Yaya Toure akiwa na wakala wake, Dimitri Seluk(kushoto)
Dimitri Seluk ni wakala ambaye  sio maarufu sana aliyedumu  kwa miaka 15 na  kiungo Muivory Coast Yaya Toure, ambaye kwake  ni zaidi ya baba kwani  Toure humwita “Papushka”  na aliamua kumpa heshima ya  jina lake kwa  kumwita mwanae wa mwisho, unajua balaa lake?
Zinaweza kuwa stori za kawaida  jinsi tunavyosonga mbele kutokana na mkongwe Bastian  Schweinsteigekuachwa  kwenye “list” ya watakaokuwepo kwenye ligi ya mabingwa na kocha wake Jose Mourinho ndani ya Old Trafford sasa upande wa mbili ndani ya mji wa Manchester, Man City, Msenegali Yaya Toure,aliyetimka Barcelona iilyokuwa chini ya Guardiola mwaka 2010 na kuhamia Man City, amebaki Etihad baada ya dirisha la usajili kufungwa rasmi na hivyo hana nafasi tena ya kushiriki Michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa.
Toure amwenye miaka 33 hajaingia kiwanjani kwenye mechi tatu za mwanzo wa msimu zaidi mechi moja ya  kuwania kufuzu kucheza makundi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Steaua Bucharest  ya Guardiola, kitendo hicho kikamkera  wakala wake Dimitri Seluk  akaamua kumbwatukia Pep  kwa maneno ya shombo.
“Kama atachukua taji la Ligi ya Mabingwa msimu huu, basi nitasafiri mpaka England na nitasema mbele ya runinga kwamba Pep Guardiola ni meneja bora kabisa duniani,” Seluk alinukuliwa na gazeti la Sunday Mirror.
Wakala huyo  anadhani  ni wakati sahihi kwa mchezaji huyo kung’oa nanga kwenye kikosi hicho kwenye dirisha la usajili mwezi wa kwanza.
Wakala huyo anaona ni ukandamizaji uliokikuka misingi kwa mteja wake kuwekwa nje hasa akiwa ni mchezaji aliyeibeba vilivyo Man City. “Haya ni maamuzi ya Pep na tunapaswa kuyaheshimu. Yaya ni mchezaji mwenye weledi na hivyo basi anafanya kila kitu ambacho anaelekezwa kufanya” alidai
“Pengine maono ya  Pep, kwamba anafaa kucheza dakika 10 za mwisho za mchezo wa Kombe la Ligi dhidi ya timu ya daraja la tatu……….ndiyo, natania tu lakini” alinukuliwa wakala huyo


WIZI WA KURA AFRIKA MBIONI KUFIKIA UKOMO


Wakati nchi ya Gabon ikikumbwa na machafuko baada ya uchaguzi mkuu kuisha uliomrejesha Rais aliyekuwepo madarakani  Ali Bongo Ondimba, mwana wa Rais wa zamani Omari Bongo wataalamu wa mambo ya chaguzi wanadai udanganyifu wa matokeo barani Afrika unazidi kuwa mgumu,  huku kwakuwa wananchi wenyewe wanasimamia vyema  ulinzi wa kura,  mashirika mbalimbali ya kijamii ambayo yamekuwa mstari wa mbele kufuatilia chaguzi mbalimbali, kukosoa pamoja na kuenea kwa teknolojia ya simu za mikononi.

Ijumaa ya wiki iliyopita kiongozi mkuu wa upinzani nchini Gabon, Jean Ping  alijitangaza kuwa mshindi  na Rais halali nchini Gabon na kutaka kurudiwa upya kwa uhesabuji wa kura, kufuatia  madai ya Rais Ali Bongo  kuwa aliibuka mshindi kwa kura zaidi ya elfu sita katika uchaguzi uliofanyika Agosti 27 mwaka huu. "Kwa chaguzi za hivi karibuni hasa Afrika ya Kati na Magharibi nchi za Senegal, Ghana na Cape Verde zinaonyesha jinsi gani demokrasia inavyokomaa" anadai  ndugu Aboubacary Mbodji, katibu mkuu wa kundi la kudai haki la RADDHO.

Meneja wa tasisi ya siasa na utawala wa Afrika Magharibi(OSIWA), Mathias Hounkpe amesema kuwa  kadiri miaka inavyozidi kwenda udanganyifu kwenye chaguzi unazidi kuwa mgumu.

Meneja wa tasisi ya Siasa na Utwala wa Afrika Magharibi(OSIWA,  ndugu Mathias Hounkpe.

Afrika Magharibi imekuwa katika wakati mgumu wa machafuko hasa yanayotokea Gabon na yale yaliyotokea Senegal na Burkinafaso miaka ya nyuma.
Nchi za Afrika Mashariki pia, ikiwemo Tanzania, Uganda na Burundi zimekuwa katika hali ya kuarifiwa kuwepo kwa udanganyifu kwenye chaguzi kutokana na baadhi ya wagombea kulalamika waziwazi kuwa wameibiwa ila hayajaleta mchafuko makubwa kama ilivyo  hali ya Afrika Magharibi.

WASANII WAMEPOKEA VIBAYA STORI YA LIL WAYNE KUACHA MUZIKI


Mpaka sasa wasanii na mashabiki kibao wamepokea stori hizo kwa huzuni wakiwemo  Missy Elliott, Lupe Fiasco, Chevy Woods,  Flying Lotus, na wengineo, Mkali Liltunechi ameamua hilo baada ya kuona muziki wake umeandamwa na matatizo kibao.
Aliandika kwenye Twitter: "Sasa sijiwezi tena, sipo poa kiakili, na naondoka kwa staha na nashukuru mashabiki wangu."

Hata hivyo, hajafafanua iwapo ataacha sekta ya uimbaji kabisa, au ataacha tu uimbaji wa muziki wa kufoka. Mwanamuziki huyo wa umri wa miaka 33 hata hivyo amesema hataki "kuonewa huruma".
Lil Wayne amekuwa akigonga vichwa vya habari hivi karibuni kwa visa mbalimbali,  huku rapa Rick Ross akionekana kujibu maneno ya shabiki  aliyehitaji Tunechi kusainiwa Maybach Music Group(MMG) kwa kuandika “Muunganishe Birdman kwenye simu”

Amekuwa na mzozo wa muda mrefu na  lebo ya Cash Money Records inayomilikiwa na babaye kimuziki Birdman, kuhusiana kucheleweshwa kwa albamu yake ya 11, ambayo imepewa jina Tha Carter V. Alishutumu kampuni hiyo siku mbili zilizopita akitumbuiza na Drake mjini Miami.
Polisi Miami walifika nyumbani kwake kisiwa cha La Gorce baada ya mtu kupiga simu 911 akisema kulikuwa na ufyatuaji risasi. Habari hizo hazikuwa za kweli.


Hii ndio “tweet”  ya Lil Wayne;
 Lil Wayne WEEZY FVerified account‏@LilTunechi
I AM NOW DEFENSELESS AND mentally DEFEATED & I leave gracefully and thankful I luh my fanz but I'm dun

Hawa ni kati ya wasanii walioguswa;

 Missy Elliott ‏@MissyElliott  @LilTunechi Prayers up 4 whatever u may be enduring right now this to will pass & may u find PEACE  I will always be a fan of your work


Chris Clemons ‏@chrisclemons91
@LilTunechi       The game will never be the same!!! Long live the  of my generation.


WASANII WAMEPOKEA VIBAYA STORI YA LIL WAYNE KUACHA MUZIKI


Mpaka sasa wasanii na mashabiki kibao wamepokea  kwa huzuni stori ya mkali wa rap mwenye vionjo vya mziki vilivyozaa vijana kadhaa kama Future, YG, na Young  Thug kuwa ameacha muziki. Wakali kibao waizungumzia "ishu" hiyo  huzuni, wakiwemo  Missy Elliott, Lupe Fiasco, Chevy Woods,  Flying Lotus, na wengineo, Mkali Liltunechi ameamua hilo baada ya kuona muziki wake umeandamwa na matatizo kibao.
Aliandika kwenye akaunti yake ya twitter: "Sasa sijiwezi tena, sipo poa kiakili, na naondoka kwa staha na nashukuru mashabiki wangu."

Hata hivyo, hajafafanua iwapo ataacha sekta ya uimbaji kabisa, au ataacha tu uimbaji wa muziki wa kufoka. Mwanamuziki huyo wa umri wa miaka 33 hata hivyo amesema hataki "kuonewa huruma".
Lil Wayne amekuwa akigonga vichwa vya habari hivi karibuni kwa visa mbalimbali,  huku rapa Rick Ross akionekana kujibu maneno ya shabiki  aliyehitaji Tunechi kusainiwa Maybach Music Group(MMG) kwa kuandika “Muunganishe Birdman kwenye simu”

Amekuwa na mzozo wa muda mrefu na  lebo ya Cash Money Records inayomilikiwa na baba yake kimuziki Birdman, ishu kubwa ni kuhusiana na kucheleweshwa kwa albamu yake ya 11, ambayo imepewa jina Tha Carter V. Alishutumu kampuni hiyo siku kadhaa zilizopita akitumbuiza na Drake mjini Miami.
balaa lingine ni la hivi juzi kati baada ya polisi wa  Miami kufika nyumbani kwake kisiwa cha La Gorce baada ya mtu kupiga simu 911 akisema kulikuwa na ufyatuaji risasi. Habari hizo hazikuwa za kweli.


Hii ndio “tweet”  ya Lil Wayne;
 Lil Wayne WEEZY FVerified account‏@LilTunechi
I AM NOW DEFENSELESS AND mentally DEFEATED & I leave gracefully and thankful I luh my fanz but I'm dun

Hawa ni kati ya wasanii walioguswa;

 Missy Elliott ‏@MissyElliott  @LilTunechi Prayers up 4 whatever u may be enduring right now this to will pass & may u find PEACE  I will always be a fan of your work


Chris Clemons ‏@chrisclemons91
@LilTunechi       The game will never be the same!!! Long live the  of my generation.


Sunday 4 September 2016

MOURINH0 KAMGEUKA SCHWEINSTEIGER

Ilionekana kama mvumilivu hula mbivu kwa  kiungo Bastian Schweinsteiger baada ya kocha wa Man U, Jose Mourinho  kuonyesha kutomhitaji  ila kiungo  alikaza na kuonekana shujaa mbele ya “special one”  siku chache baada ya jina lake kujumuishwa kwenye kikosi cha Man United kwenye msimu wa ligi wa 2016-17,  ila balaa limekuja baada ya Bastian Schweinsteiger kugeuziwa kibao na kocha wake Mourinho baada ya jina lake kutojumuisha katika kikosi kitakachoshiriki Ligi ya Europa. Schweinsteiger ambaye huko nyuma alicheza kwa mafanikio makubwa kunako klabu ya Bayern Munich ameichezea Ujerumani michezo 121.
Kiungo huyo mkongwe amestaafu soka la kimataifa  baada ya Jumatano  iliyopita kufanyiwa sherehe ya kuagwa kwenye Timu ya Taifa ya Ujerumani maarufu kama Die Manschaft kufutiwa kufanyika mchezo maalum dhidi ya Finland na kushinda mabao 2-0.
Katika kikosi hicho, viungo 10 wametajwa huku jina la Schweisteiger likipigwa panga.
Kikosi kizima kipo hivi:
Makipa: David De Gea, Sergio Romero, Sam Johnstone
Mabeki: Eric Bailly, Phil Jones, Marcus Rojo, Daley Blind, Chris Smalling, Luke Shaw, Timothy Fosu-Mensah, Antonio Valencia, Matteo Darmian, Axel Tuanzebe
Viungo: Paul Pogba, Juan Mata, Jesse Lingard, Michael Carrick, Ashley Young, Ander Herrera, Henrikh Mkhitaryan, Marouane Fellaini, Morgan Schneiderlin, Memphis Depay
Washambuliaji: Wayne Rooney, Zlatan Ibrahimovic, Anthony Martial, Marcus Rashford.


BECKHAM: MWACHENI ROONEY MPAKA ATAKAPOONA HAWEZI

Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya England, David Beckham ameweka hilo wazi baada ya kuona staa Wayne Rooney wengi wakimzungumzia kuwa ni muda kumpumzika kwa sasa.
Beckham ambaye aliichezea kwa mafanikio ya wastani timu ya taifa kuliko klabu alizopita alituma jumbe hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram kuelekea mechi dhidi ya Slovakia ambapo Rooney anakwenda kuvunja rekodi ya kucheza mechi nyingi ndani ya timu ya taifa leo usiku.
"Cheza mpaka muda utapofika huwezi tena......hakuna hisia unazopata ukiwa unacheza kwaajili ya Taifa lako ukiwa Wembley" alidai David Beckham.
Wayne Rooney kwa miezi ya karibuni ameonekana hayuko 'fit' na hasa wadau wakiona ni nafasi ya kipekee kuwaachia makinda waliopo.
Mshambuliaji nyota na nahodha wa Uingereza Wayne Rooney anatarajia kustaafu soka la kimataifa baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 itakayofanyika nchini Urusi.
Kwa upande wake akihojiwa Rooney ambaye amefunga mabao 53 katika mechi 115 kwa Uingereza, amesema pindi Kombe la Dunia la Urusi litakapomalizika anadhani wakati wake wa kuaga soka la kimataifa utakuwa umefika.
Nyota huyo aliendelea kudai kuwa michuano hiyo itakuwa nafasi yake ya mwisho kufanya kila kitu na Uingereza hivyo bado ataendelea kufurahia miaka miwili iliyobakia.
Kama Rooney akicheza mchezo wa Jumapili hii wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Slovakia, atakuwa amevunja rekodi ya David Beckham ya kucheza mechi nyingi katika timu ya taifa.
Soma ujumbe  wa Beckham hapo chini kupitia mtandao wa Instagram:
" So tonight Wayne becomes England’s most capped outfield player .. I keep listening to people say Wayne should stop playing for his country to prolong his club career .. Wayne should retire from playing for his country… Seriously .. As a player you retire when you’re ready.. Representing you’re country is the highest level you can reach as a professional player , walking out in an England shirt at Wembley is one of the greatest feelings as a player you can ever have … Don’t let anyone take that away from you .. Every kid around the world that loves this game dreams of walking out in the national team colours and representing the country they love .. Continue till you can’t give anymore .. Congratulations mate @manchesterunited @england”.
David Beckham na Wayne Rooney mwenye jezi no.10 kiindi wakiiwa wote timu ya  taifa

BECKHAM: MWACHENI ROONEY MPAKA ATAKAPOONA HAWEZI

Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya England, David Beckham ameweka hilo wazi baada ya kuona staa Wayne Rooney wengi wakimzungumzia kuwa ni muda kumpumzika kwa sasa.
Beckham ambaye aliichezea kwa mafanikio ya wastani timu ya taifa kuliko klabu alizopita alituma jumbe hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram kuelekea mechi dhidi ya Slovakia ambapo Rooney anakwenda kuvunja rekodi ya kucheza mechi nyingi ndani ya timu ya taifa leo usiku.
"Cheza mpaka muda utapofika huwezi tena......hakuna hisia unazopata ukiwa unacheza kwaajili ya Taifa lako ukiwa Wembley" alidai David Beckham.
Wayne Rooney kwa miezi ya karibuni ameonekana hayuko 'fit' na hasa wadau wakiona ni nafasi ya kipekee kuwaachia makinda waliopo.
Mshambuliaji nyota na nahodha wa Uingereza Wayne Rooney anatarajia kustaafu soka la kimataifa baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 itakayofanyika nchini Urusi.
Kwa upande wake akihojiwa Rooney ambaye amefunga mabao 53 katika mechi 115 kwa Uingereza, amesema pindi Kombe la Dunia la Urusi litakapomalizika anadhani wakati wake wa kuaga soka la kimataifa utakuwa umefika.
Nyota huyo aliendelea kudai kuwa michuano hiyo itakuwa nafasi yake ya mwisho kufanya kila kitu na Uingereza hivyo bado ataendelea kufurahia miaka miwili iliyobakia.
Kama Rooney akicheza mchezo wa Jumapili hii wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Slovakia, atakuwa amevunja rekodi ya David Beckham ya kucheza mechi nyingi katika timu ya taifa.
Soma ujumbe  wa Beckham hapo chini kupitia mtandao wa Instagram:
" So tonight Wayne becomes England’s most capped outfield player .. I keep listening to people say Wayne should stop playing for his country to prolong his club career .. Wayne should retire from playing for his country… Seriously .. As a player you retire when you’re ready.. Representing you’re country is the highest level you can reach as a professional player , walking out in an England shirt at Wembley is one of the greatest feelings as a player you can ever have … Don’t let anyone take that away from you .. Every kid around the world that loves this game dreams of walking out in the national team colours and representing the country they love .. Continue till you can’t give anymore .. Congratulations mate @manchesterunited @england”.
David Beckham na Wayne Rooney mwenye jezi no.10 kiindi wakiiwa wote timu ya  taifa

MAMA THERESA WA CALCUTTA ATANGAZWA KUWA MTAKATIFU

Maelfu ya watu wameshuhudia kwa pamoja ambapo Papa Francis amemtangaza mtawa Mama Teresa kuwa mtakatifu.
Mwanamama huyo wa Albania ambaye alifariki mwaka wa 1997 alianzisha shirika la hisani la kimishenari ili kuwasaidia wasionacho katika mtaa wa mabanda wa Calcutta nchini India.
Hivyo kuanzia sasa ataitwa mtakatifu Teresa wa Calcutta.
Waandishi na wataalamu wa mambo wanasema kuwa maisha yake yanaenda sambamba na maono ya Papa Francis kuhusu kanisa linalojikakamua kuwasaidai watu masikini.
Lakini wakosoaji wanasema kuwa Mama Teresa hakuwasaidia watu waliokuwa wagonjwa na alilaumiwa kwa kujaribu kuwabadilisha dini watu masikini wa kabila la Hindu nchini India kuwa Wakristo.
 Mama Theresa

TAIFA STARS HAINA REKODI DHIDI DHIDI YA SUPER EAGLE

Taifa Stars imeshindwa kuvimba ili kuitafuta rekodi iliyowekwa na Wanaigeria katika mechi nane za kimataifa walizokutana.
Mchezo wa jana uliochezwa uwanja wa Akwa Ibom huko Nigeria, ulikuwa wa mwisho  wa kundi G katika hatua za kufuzu AFCON 2017 huko Gabon dhidi ya Super Eagles, mchezo ulikwisha huku mshambuliaji kijana  wa Man City, Kelechi Iheanacho akitupia dakika ya 77.
Kwa goli hilo ndoto za Taifa Stars iliyokuwa ikiongozwa na nahodha wake Mbwana Samatta anayekipiga klabu ya Genk ya huko Ubelgiji ziliishia kuambulia historia ya sare ya mechi tatu na kufungwa mechi tano(ya jana ikiwemo) hivyo hakuna  "ubabe" wowote kwa Taifa Stars dhidi ya Super Eagle iliyoongozwa na kiungo mkongwe Mikel Obi na mshambuliaji machachari Ahmed Mussa. 

Mafarao wa Misri ni kati ya waliopenya ndani ya kundi la G.