Monday 5 September 2016

WIZI WA KURA AFRIKA MBIONI KUFIKIA UKOMO


Wakati nchi ya Gabon ikikumbwa na machafuko baada ya uchaguzi mkuu kuisha uliomrejesha Rais aliyekuwepo madarakani  Ali Bongo Ondimba, mwana wa Rais wa zamani Omari Bongo wataalamu wa mambo ya chaguzi wanadai udanganyifu wa matokeo barani Afrika unazidi kuwa mgumu,  huku kwakuwa wananchi wenyewe wanasimamia vyema  ulinzi wa kura,  mashirika mbalimbali ya kijamii ambayo yamekuwa mstari wa mbele kufuatilia chaguzi mbalimbali, kukosoa pamoja na kuenea kwa teknolojia ya simu za mikononi.

Ijumaa ya wiki iliyopita kiongozi mkuu wa upinzani nchini Gabon, Jean Ping  alijitangaza kuwa mshindi  na Rais halali nchini Gabon na kutaka kurudiwa upya kwa uhesabuji wa kura, kufuatia  madai ya Rais Ali Bongo  kuwa aliibuka mshindi kwa kura zaidi ya elfu sita katika uchaguzi uliofanyika Agosti 27 mwaka huu. "Kwa chaguzi za hivi karibuni hasa Afrika ya Kati na Magharibi nchi za Senegal, Ghana na Cape Verde zinaonyesha jinsi gani demokrasia inavyokomaa" anadai  ndugu Aboubacary Mbodji, katibu mkuu wa kundi la kudai haki la RADDHO.

Meneja wa tasisi ya siasa na utawala wa Afrika Magharibi(OSIWA), Mathias Hounkpe amesema kuwa  kadiri miaka inavyozidi kwenda udanganyifu kwenye chaguzi unazidi kuwa mgumu.

Meneja wa tasisi ya Siasa na Utwala wa Afrika Magharibi(OSIWA,  ndugu Mathias Hounkpe.

Afrika Magharibi imekuwa katika wakati mgumu wa machafuko hasa yanayotokea Gabon na yale yaliyotokea Senegal na Burkinafaso miaka ya nyuma.
Nchi za Afrika Mashariki pia, ikiwemo Tanzania, Uganda na Burundi zimekuwa katika hali ya kuarifiwa kuwepo kwa udanganyifu kwenye chaguzi kutokana na baadhi ya wagombea kulalamika waziwazi kuwa wameibiwa ila hayajaleta mchafuko makubwa kama ilivyo  hali ya Afrika Magharibi.

No comments:

Post a Comment