Kiungo Yaya Toure akiwa na wakala wake, Dimitri Seluk(kushoto) |
Dimitri Seluk ni
wakala ambaye sio maarufu sana aliyedumu
kwa miaka 15 na kiungo Muivory Coast Yaya Toure, ambaye kwake ni zaidi ya baba kwani Toure humwita “Papushka” na aliamua kumpa heshima ya jina lake kwa kumwita mwanae wa mwisho, unajua balaa lake?
Zinaweza kuwa stori za
kawaida jinsi tunavyosonga mbele kutokana
na mkongwe Bastian Schweinsteiger kuachwa kwenye
“list” ya watakaokuwepo kwenye ligi ya mabingwa na kocha wake Jose Mourinho
ndani ya Old Trafford sasa upande wa mbili ndani ya mji wa Manchester, Man City,
Msenegali Yaya Toure,aliyetimka Barcelona iilyokuwa chini ya Guardiola mwaka
2010 na kuhamia Man City, amebaki Etihad baada ya dirisha la usajili kufungwa
rasmi na hivyo hana nafasi tena ya kushiriki Michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa.
Toure amwenye miaka 33
hajaingia kiwanjani kwenye mechi tatu za mwanzo wa msimu zaidi mechi moja ya kuwania kufuzu kucheza makundi ya Ligi ya
Mabingwa dhidi ya Steaua Bucharest ya
Guardiola, kitendo hicho kikamkera wakala
wake Dimitri Seluk akaamua kumbwatukia
Pep kwa maneno ya shombo.
“Kama atachukua taji
la Ligi ya Mabingwa msimu huu, basi nitasafiri mpaka England na nitasema mbele
ya runinga kwamba Pep Guardiola ni meneja bora kabisa duniani,” Seluk
alinukuliwa na gazeti la Sunday Mirror.
Wakala huyo anadhani ni wakati sahihi kwa mchezaji huyo kung’oa
nanga kwenye kikosi hicho kwenye dirisha la usajili mwezi wa kwanza.
Wakala huyo anaona ni
ukandamizaji uliokikuka misingi kwa mteja wake kuwekwa nje hasa akiwa ni
mchezaji aliyeibeba vilivyo Man City. “Haya ni maamuzi ya Pep na tunapaswa
kuyaheshimu. Yaya ni mchezaji mwenye weledi na hivyo basi anafanya kila kitu
ambacho anaelekezwa kufanya” alidai
“Pengine maono ya Pep, kwamba anafaa kucheza dakika 10 za
mwisho za mchezo wa Kombe la Ligi dhidi ya timu ya daraja la tatu……….ndiyo,
natania tu lakini” alinukuliwa wakala huyo
No comments:
Post a Comment