Sunday 4 September 2016

BECKHAM: MWACHENI ROONEY MPAKA ATAKAPOONA HAWEZI

Nahodha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya England, David Beckham ameweka hilo wazi baada ya kuona staa Wayne Rooney wengi wakimzungumzia kuwa ni muda kumpumzika kwa sasa.
Beckham ambaye aliichezea kwa mafanikio ya wastani timu ya taifa kuliko klabu alizopita alituma jumbe hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram kuelekea mechi dhidi ya Slovakia ambapo Rooney anakwenda kuvunja rekodi ya kucheza mechi nyingi ndani ya timu ya taifa leo usiku.
"Cheza mpaka muda utapofika huwezi tena......hakuna hisia unazopata ukiwa unacheza kwaajili ya Taifa lako ukiwa Wembley" alidai David Beckham.
Wayne Rooney kwa miezi ya karibuni ameonekana hayuko 'fit' na hasa wadau wakiona ni nafasi ya kipekee kuwaachia makinda waliopo.
Mshambuliaji nyota na nahodha wa Uingereza Wayne Rooney anatarajia kustaafu soka la kimataifa baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 itakayofanyika nchini Urusi.
Kwa upande wake akihojiwa Rooney ambaye amefunga mabao 53 katika mechi 115 kwa Uingereza, amesema pindi Kombe la Dunia la Urusi litakapomalizika anadhani wakati wake wa kuaga soka la kimataifa utakuwa umefika.
Nyota huyo aliendelea kudai kuwa michuano hiyo itakuwa nafasi yake ya mwisho kufanya kila kitu na Uingereza hivyo bado ataendelea kufurahia miaka miwili iliyobakia.
Kama Rooney akicheza mchezo wa Jumapili hii wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Slovakia, atakuwa amevunja rekodi ya David Beckham ya kucheza mechi nyingi katika timu ya taifa.
Soma ujumbe  wa Beckham hapo chini kupitia mtandao wa Instagram:
" So tonight Wayne becomes England’s most capped outfield player .. I keep listening to people say Wayne should stop playing for his country to prolong his club career .. Wayne should retire from playing for his country… Seriously .. As a player you retire when you’re ready.. Representing you’re country is the highest level you can reach as a professional player , walking out in an England shirt at Wembley is one of the greatest feelings as a player you can ever have … Don’t let anyone take that away from you .. Every kid around the world that loves this game dreams of walking out in the national team colours and representing the country they love .. Continue till you can’t give anymore .. Congratulations mate @manchesterunited @england”.
David Beckham na Wayne Rooney mwenye jezi no.10 kiindi wakiiwa wote timu ya  taifa

No comments:

Post a Comment