Showing posts with label KUNTU ZA MBASI. Show all posts
Showing posts with label KUNTU ZA MBASI. Show all posts

Monday, 7 November 2016

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU MAREKANI

UMOJA WA MATAIFA ULIPONICHANIA MKEKA WA “PERFECT COMBO” YA SAUTI NYORORO VS WAPINGA UMAGHARIBI

Na
PETER MMBAGA
+255 656 859 045.


 Kuna mwalimu wangu kwa jina la Emmanuel Maqway, nina sababu za mimi kujivunia tafakuri hii aliwahi kutusisitizia kiujumla wanafunzi wake kuwa usipokuwa mwanaminifu kwa vitu vidogo vidogo  hata vikubwa ni tatizo, sasa katika vitu vidogo wamefanikiwa, uwezo, utekelezaji  na wana misimamo ya aina yake!
Nimemkumbuka Delilah kwenye Biblia, wasomaji biblia mtanielewa hapa zaidi, kipindi mamia ya mijianaume ya kifilisti iliposhindwa kupambana na Samson, ikamtumia  mwanamke kumwangusha mwamba. Fikiria mwanamke mmoja tu!
Kisa cha kanisa la Anglikana kuanzishwa, ilikuwaje?Mwaka 1527, Mfalme Henry VIII  wa Uingereza aliwaza penzi la Anne Boleyn aliyekuwa  msaidizi wa mkewe Catherine wa Aragon na  kutaka kumuoa, kanisa Katoliki likaweka pingamizi kwakuwa talaka haruhusiwi, Henry VIII akaona dola kubwa ya Uingereza haiwezi ingiliwa na dola ya Roma, akajitoa rasmi ndani ya ukatoliki na kuupiga marufuku Uingereza. Mfalme Henry VIII akampa mkewe talaka na akawa kiongozi mkuu wa kanisa la Anglikana. Twende taratibu utanielewa, nguvu ya mwanamama hiyo!
Hata dola ya Israeli kugawanyika kusini na kaskazini moja ya sababu ni  matokeo ya mfalme Suleimani kuwa na “masuria”  ubavuni  mwake walitokea Misri waliomletea miungu ya Baali  kipindi cha malkia wa Sheba akamuasi Mungu   wa kweli! “Masuria” hao?
Maajabu ya wanawake ni wavumilivu, jasiri, na uwezo wa hali ya juu sana ila ni watu wa kupenda  ushauri, kujaliwa na kusikilizwa, usiyafanye yote hayo na  usiombe achoke, akasirike na yamfike, utajuta!  Utajua yeye ni mwanamke, kiumbe chenye nguvu!
Dunia ina mambo ila wanadamu wana mambo ya ajabu, na ukistaajabu ya Musa, utayaona ya firauni, haitii shaka unapoona  kuhusu kisichotarajiwa kabisa lakini kuna wanaojua kabisa kitatukia. Twende taratibu, utanielewa!
Kuna jamaa anaitwa Pablo Reyes pale Marekani kashajijengea umaarufu kwa alichokiandika desemba mwaka jana kupitia  ukurasa wake wa facebook, kuwa  mwaka 2016 tulioko sasa, kuna vifo vya watu maarufu duniani  kama mpiganaji wa mtaani, Kimbo Slice, mwanamuziki mwingereza Prince, mwanandondi Muhammad Ali, Gorilla, na nchi ya Marekani itashuhudia mauaji ya kinyama(mfano mdogo, polisi na watu weusi), vyote hivyo vimeshatokea. Utabiri umetimia!
Kwa maelezo yake kilichobaki ni kifo cha Donald Trump, mgombea urais Marekani kupitia chama cha Republican na mwanamama Hillary Clinton, mgombea kupitia chama cha Democratic  kuwa rais wa kwanza mwanamke nchini Marekani, utabiri wake utatimia? 
Mgombea urais Marekani kwa chama cha Democratic, Mama Hillary Clinton.
Unajua Wamarekani kesho Jumanne ya novemba 8,  wanaamua nani awe Rais?, na Pablo alipotaja mwanamama kuiongoza Marekani, ndipo jicho lilipojikita, hapohapo  Washington D.C, jirani ni shirika  la fedha duniani(IMF) kuna mwanamama  mwenye misimamo yake wa kifaransa anaitwa Christine Lagarde  anakwenda kwenye muhula wa pili  wa miaka mitano baada ya kuongoza taasisi hiyo yenye nguvu duniani toka 2011, masharti magumu yaliyobadilisha siasa za dunia ya tatu yaliletwa nao!
Bosi wa IMF, Mama Christine Lagarde.
Malkia wa Uingereza, Elizabeth II anaongoza “sakata” akimpa nguvu ya kiutendaji, Theresa May ambaye kaikamata nafasi ya Waziri Mkuu hivi karibuni , pale Ujerumani yalikwishatimia kwa kansela Angela Merkel, Anasubiri kwa hamu kwakuwa wamepata nguvu ya pamoja na anagombea kwa msimu mwingine wa nne huku chama chake cha CDU(Christian Democratic Union) kikishika nafasi ya tatu nyuma ya chama cha Demokrasia ya kijamii(SDP) na Alternative fur Deutschland(AfD) kwenye chaguzi za majimbo, waandamaji kumsakama wakitaka aachie ngazi  kwa kuruhusu wahamiaji  mwaka 2015 nchini Ujerumani  tena siku ya kumbukumbu ya miaka 26 ya muungano wa Ujerumani “Germany Unity Day” mapema Oktoba 3, mwaka huu  ila hajapata kigugumizi na vyama vyote vitamsapoti mwakani 2017 kwenye uchaguzi. Kutilia mkazo hasa ndani ya EU (Umoja wa Ulaya) kuwa na sauti  ya mamuzi kutosikiliza sauti ya nchi moja kutokana na ukubwa. Moja kwa moja  mfano ni Uingereza, “mzizi” wa yeye mpka kuja kujitoa EU. “Aliona haiwezekani nchi ndogo kama Ugiriki anaisaidia bajeti yake halafu wawe na maamuzi sawa” nawaza hivyo,  Ukifuatilia kwa undani wanahusika pia kinamama.
Mahakama ya kiuhalifu ya kimataifa (ICC) ina mwanamama Mgambia,  mwendesha mashtaka mkuu(The Hague), anaitwa Fatou Bensounda ni mkakamavu mwenye maamuzi ya kijasiri asingewekwa pale,  kuna kitu cha ziada anacho kuanzia alipoiongoza wizara ya Sheria Gambia kabla ya kuteuliwa mwaka 2012.
Mwendesha Mashtaka ICC, Mama Fatou Bensounda.
Umoja wa Mataifa(UN)  daah! “wamechana mkeka” kwa mwanamama kurithi nafasi ya Ban Ki-Moon, mreno Antonio Gueterrez  kachukua, japo changamoto aliiona  ukiangalia nafasi ya wagombea 12, nane  walikuwa ni wanawake wa shoka  na “nilibet” kinamama watang’ara kama Christiana Figueres, Irina Bokova,  au Hellen Clark na baadhi yao wapo kwenye “ukubwa” wa mashirika ndani ya UN, bado tutaona “impact” yao.
Unajua ubongo wangu unawaza nini? kwenye  zama zakwenye  “fifty-fifty” haya maswala ya kutafuta usawa na haki kwenye mfumo dume ndiyo sauti hizi nyororo utapokwenda kufurahia hotuba na maamuzi zao! Ndio utazifurahia, Taratibu utanielewa!
Harakati za kuzuzururisha akili mataifani  kwa tafakuri na Wabasi wangu, tunaoamini kwenye falsafa za Ubasi, Amani akadai “Msuguano hatarishi wenye harufu ya chechendani ya miaka kumi inaweza tokea kupitia hili kwani kina Putin na wenzake kupinga sera za kihafidhina watazidi kubisha ila hisia zitawapanda kwa wao kuona sauti nyororo zinawapelekesha”, kati ya wale nane  mmoja angechukua, “anyway”  UN wamechana mkeka!
“Pia sauti nyororo zitaona zinapingwa sana nazo zitaingiza hisia kuonyesha  dunia maamuzi yao yalivyo ili heshima ionekane”.
 “Eti msuguano hatarishi ndio  utatokea? Hasa kwenye miaka kumi, wakati wengi wa hawa viongozi watatawala kwa vipindi visivyozidi vinne?” Akajibu mbasi mwingine kwa jina la Mlang’a.
Wakati tafakuri ikiendelea  mara kuna bajaj ikapita na bonge la mziki “me and you na, perfect combo, eeh na perfect combo….”
“Perfect Combo”, ndio ameimba mwanarapu Joh Makini wimbo aliomshirikisha Mnigeria Chidinma, nikawaambia wabasi wangu kuwa kweli hii itakuwa “Perfect Combo”  kwakuwa maamuzi, misimamo, dukuduku, matarajio yao yanaelekea kwenye mrengo mmoja wa kusaidia kizazi cha kinadada kwa kuwatia nguvu ya kujiamini kutoyumbishwa na misimamo ya mfumo dume iliyokwepo, na hata ukisikiliza kwa umakini hotuba zao wanavyojielezea na hasa usawa wa kijinsia na haki unavyojielekeza kuna mabadiliko watafanya, tena makubwa ya kimapinduzi.
Ni suala sio la kipuuzi au kupepesa macho kuukataa ukweli, bado wanaume na hata baadhi ya wanawake tunaamini  nguvu ya hoja kuhusu mfumo dume, waaminio biblia wanaamini mstari usemayo “……..kweli itakuweka huru”, wengi wanatetea kwenye umma kinafiki wakikutana sirini mfumo dume ndio hoja,  Twende taratibu, nadhani unaanza kunielewa!
Kinamama hawa wanaunganisha “nguvu” ya pamoja ukizingatia nchi na taasisi wanazotoka nazo zina “nguvu” za kuitawala dunia kwa masharti yao itakavyo, wana mamlaka kubwa, wataalamu wa kutosha, na uchumi mkubwa ambao ndio “silaha” ya kuteka dunia ya tatu, japo sio nchi zote zinaweza kutingishwa!
Kweli sio nchi zote zinaweza kutingishwa? Hapa ndipo kwenye ule msuguano hatarishi utakao leta cheche mbasi wangu aliounena, na nisiuopenda kuuona ila, unaweza kutokea.
 Je, misimamo ya  mataifa na taasisi zao kwenye kutoa maamuzi na kuingilia mataifa inapingwa na imeathiri vipi dunia hasa mataifa yasiyo na udini na huu unaoitwa ubeberu? Hapa namuwaza sosholisti Vladimir Putin wa Urusi, Kim  Jong-un wa Korea Kaskazini  na Xi Jinping wa China. Kwanini msuguano utakuwa mkubwa sana na kupelekea msuguano hatarishi wenye cheche?
Sauti nyororo kutoa “speech” nzito kutoakana na mataifa na taasisi nzito, na ndipo napata kigugumizi kwa kuwaona wapingaji hawa kutoka mataifa haya yanayokataa kwa uwazi ubeberu nawazungumzia  Korea Kaskazini,  China, Cuba na Urusi. Mnanielewa sio?
Je, Waarabu hasa Mashariki ya kati na misimamo yao ya kidini na utamaduni wao, kwenye hii ‘fifty-fifty”  na “order” ya sauti nyororo  wataelewa, kwakuwa tu, kule kwao hata gari kinamama hawaruhusiwi kuendesha!
Na nguvu ya utekelezaji wa sera zao wanaweza kuzipenyeza kwa namna yoyote ile hata kwa nguvu, angalia Uganda kusitishiwa misaada kisa kupinga sheria za ndoa ya jinsia moja, misaada wamekata!
Sio hatuwezi kusimama bila wao, ila mifumo ilishazoea hiyo hali hivyo lazima mkatae huku haijasitishwa, hapo sitaki kupagusia kwakuwa sio “engo” husika. Akili haipo sawa“ UN wamechana mkeka”. Sio “kesi”, kwanini?
Maamuzi ya dunia yanategemea sana haya mataifa na taasisi hizi, kumbuka suala la demokrasia na mfumo wa vyama vingi  kwenye dunia ya tatu uliletwa na shirika la fedha duniani (IMF) kupitia mpango waliouita “Structural Adjustment Programme”, zaidi  Marekani ndiye mama wa sauti za kutaka mambo yaende atakavyo, siasa ya dunia kaikalia na anaijua, nchi na taasisi  zenye nguvu kimaamuzi na utekelezaji duniani zina watu hawa, kwenye nafasi ya wanawake wenye nguvu duniani sita bora Miss Lagarde, Angel Merkel na Hillary Clinton wamo.
Sasa sidhani kama hawa wapingaji wa sera za mabeberu, watarudisha kuni nyuma kutochochea moto, upande wa pili ukiweka mkaa!  Mnanielewa sio?
Sio  kitu cha kushangaza kwenye mifumo yenye mizizi ya kidini, kikabila, kijamii na mazoea vilikuwa vinapinga na havioni nafasi ya mwanamke kwenye mambo makubwa, jiulize ile presha ya kupinga itaongezeka au kupungua kwa asilimia ngapi? 
Sitamani kuzidi  kuziona ghiliba za nchi wanachama wa ubeberu zilivyo na ushirikiano toka muda mrefu. Tangu enzi za vita ya pili ya dunia, Marekani na Uingereza huku taasisi ya IMF na UN zote zipo Marekani na zaidi yule mwanamama kiongozi wa IMF ni mfaransa, sapoti kubwa inaongezeka!
Mnanielewa sasa? maslahi na maamuzi nguvu ya kura “veto” ndani ya UN, na hasa ndani ya baraza la usalama ambapo China na Urusi wapo ila Marekani, Uingereza na Ufaransa  nao ni memba  wa kudumu na jinsi nchi  hizi zilivyo na ukaribu watazidi kulekeza nguvu kwenye maslahi yao kidunia na upande wa pili ni dhahiri hawatokaa kimya.
Ninapoangalia nguvu ya sauti nyororo ipenyayo masikioni bila kutumia nguvu, ila maneno yapenyanyo yanaweza kuwa na zuri au baya, ukicheza tu huponyoki. Ila masoshalisti na wenye “imani kali” watapindua unyororo wa sauti hiyo, na sauti hizi“zitajiongeza” kwa kutumia hisia, nini kitatokea? Msuguano hatarishi!
Bado natafakari baada ya miaka nane mpaka kumi ya vipindi vya sauti hizi nyororo karibu zote zikiachia ngazi. Dunia itaingia kwenye hatua kuelekea historia, kwa wale  “Standpoints feminists” wanayoiamini, japo UN wametuchania mkeka mimi na Wabasi wangu  katika fikra pana, mwanafalsafa E.Maqway na  ndugu Amani.
“End will justifies the meaning” Waingereza husema!


Friday, 14 October 2016

“Argue, Don't Shout" Ya Mwalimu Nyerere Tuiishi Kwa Vitendo

Hii ni makala niliyokuwekea uisome hapa Oktoba 14, ila siku iliyofuata Oktoba 15, 2016  imepata nafasi kwenye gazeti la TanzaniaDaima
   
   
Na 
Peter C. Mmbaga

Ndiyo muda wangu wa kuingia “Giningi” na Wabasi  wenzangu ambao tunaamini kwenye mawazo ya  chanya pasipo kupepesa  macho, safari ya Giningi inahitaji ufunge mkanda kweli kweli na leo nipo njiani kuongea na  kumpa pongezi za  “kuondoka” zake mapema mbasi wangu katika fikra Mwalimu mkuu, Baba Makongoro  kwakuwa angebaki mpaka sasa angekuwa anaduwaa kama mimi na vile hapendi  kuonekana  kwenye   “maamuzi  ya umimi”,  anakuwa mpole tu.
Kumbuka kipindi kile wakisema  baadhi ya viongozi   waliokuwa wanafanya mambo  tofauti, yeye alitoa tamko gani? Kwenye kitabu chake cha “Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania” anabaki kama mshauri tu, japo kutokana na hadhi yake ama “popularity” aliyokuwa nao asingesikilizwa na wananchi kweli, katika kukataza?
Aliwaachia uhuru wajitathimini  wenyewe, na uhuru ni mbaya sana, walipoona   mbasi wangu katika fikra  chanya hajaja juu wakaona sawa tu, mambo yanafanyika,  anajifanya haoni. Kumbe “mbasi” ulikuwa “unawachora” tu.
“Giningi yetu” ina raha yake huku yupo Baba wa maridhiano, mbasi wangu katika fikra, Mandela yeye anatabasamu tu anasema “Real leaders must be ready to sacrifice  all for the freedom of their people“ kwa tafsiri isiyo rasmi ni kuwa “ Vingozi wa kweli wanatakiwa wawe tayari kujitoa vilivyo kwa  uhuru wa wananchi”, naye namwangalia natabasamu  kwa kuwa kazi aliyoiamua  Rais JPM ni ngumu  sana kwakuwa  wapiga vita mfumo  mzuri wapo  na hasa watendaji, “We got a Long Way To Freedom” ila kwa imani atawatumbua tu!
Baba Makongoro bwana ananifurahisha sana akasema “Siku Wamarekani wakinisifia nimefanya kazi nzuri nitajiuliza kuwa nimekosea wapi?”  ndiyo kitu nilichompendea hasa kwa kauli hizi za kujiamini kwa nukuu nilyooina kwenye gazeti moja la kila siku miaka mitatu nyuma, ni kauli ya Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), chuo ambacho Mwalimu alikianzisha na mara kwa mara kufika hapo kwa ajili ya mijadala na wanafunzi kuhusu uhuru na maendeleo ya Afrika na dunia kwa ujumla, Bashiru Ally, anaamini Mwalimu anastahili  kupewa tuzo  lakini ananyimwa kutokana na kuyaudhi mataifa ya magharibi wakati aliongoza harakati za kudai haki za binadamu na uhuru wa mataifa ya Afrika. Huu ndiyo ushujaa tunaouhitaji Rais JPM piga kazi kwa haki na kweli usihitaji kusifiwa na watu wa nje ila tu angalia uhuru uwepo kama Baba Makongoro alivyoutoa. Mwalimu vijana wa leo sio wa kipindi kile  “pesa” inawanunua wanashindwa kutetea maslahi ya nchi,  hasa wasomi dira hawaileti , ukanijibu “pesa ni matokeo” kama ulivyoainisha kwenye kitabu chako cha cha “Ujamaaa na Kujitegemea” lakini Mwalimu sasa sivyo, nadhani wakati nao unabadilika, ila  wanaamini,  pesa ndilo lenye nguvu!
Sasa hivi wasomi wanaonekana shujaa  kwenye dimbwi la mfumo  huu wakuogopa kuhoji, vyuo vikuu vimepoa  vimenyamaza, nahisi huko ndiko ulipowasikia kwa mara ya kwanza   kina ndugu Lowassa, JK  na wengineo,   ila sasa wanaogopa  kuitwa wasaliti ni bora kuliko kuonekana mnyenyekevu kwao halafu kwenye jamii uonekane “Kamuzu”. Wazee wetu  ukiwauliza watakujibu enzi za kupigania uhuru walimwita   huyu mtu walimwitaje  "aliyeolewa na wazungu" aliwabania waafrika haki zao, ndiyo nyimbo iliyokuwa kwenye mchamchaka.
Kwanini nimesema hayo?  Nakumbusha raia wote  na viongozi wasaliti kwa machinga, boda boda, mama ntilie , wasakatonge , wasio na ajira ni bora uonekane umemsaliti rafiki yako anayetafuta  “ujiko” kwa njia ya  “matukio” kuliko kuitwa "umeolewa nao" na jamii ni mbaya sana,  lakini Mwalimu hao watu tunao?
Wewe mwenyewe ukasema “Unyenyekevu ukizidi unazaa uoga, uoga huzaa unafiki na kujipendekeza, mwisho wake mauti”
Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu J.K Nyerere

Baba Makongoro kuna walimu  wamekuwa  ‘maarufu” kwa kipindi hichi kubwa ni kumpiga mwanafunzi  wa kidato cha tatu mwezi huu uliotuaga, kuna kitu baba nimegundua Walimu wengi wanakwenda pasipo ‘passion”, lengo ni kupata mkopo ambao miaka ya karibuni imekuwa  kipaumbele kwa walimu ili kusaidia changamoto za elimu yetu, japo wanafunzi wa siku hizi ni watukutu kufikia hatua ya kuchanganywa na malezi na utandawazi ambao tumeupokea “negative” sana kwenye matumizi yake.
Mtoto  kupewa adhabu hatujakataa, ni moja ya kufunza baba, kama wewe ulifanya pale Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam kwa mmoja wa viongozi wetu kugoma akiwa  Rais wa serikali ya wanafunzi-Daruso  enzi zako  wakigomea kutopatiwa maziwa na siagi, kweli enzi zako “walikula bata”  mbasi wangu, leo hii wanasota watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu  “no mkopo”, kipaumbele kimeharibu kila kitu na wengi wanakimbilia huo ualimu,  tasnia nyingine baada ya miaka kumi wasomi wengi watakuwa kwenye  tasnia moja halafu wasio na “passion” japo sio wote ama tasnia zote lakini Je, hali itakuwaje?
Enzi zako mtu akisema mimi ni mwalimu hiyo heshima anayopewa  ni nzito lakini leo sielewi, thamani imepungua sijui kisa ni nini? Ndo maana misongo ya mawazo  inakuwa mingi sana hata kupiga wanafunzi.
Mimi kusema kula bata ni kweli kwasababu   habari  hii niliwahi  kuhadithiwa na “anko” wangu aliyesoma na ndugu Rais  mstaafu kijana wako, Jakaya  Kikwete pale Shule ya Tanga (Tanga  School) enzi zako  Mwalimu Mkuu wa fikra yakini,  juu ya elimu,chakula(asubuhi chai nzito), na usafiri wa  bure kwa gharama za Serikali.  Ila nyakati zinabadilika!
Wakati tunaendelea na maongezi yetu ya Kibasi zaidi huko “Ginigi yetu”  kuna  msomi  enzi zake Mwalimu  akaniuliza leo hii madaftari  yanauzwa  kwa shilingi ngapi  wanafunzi, vipi madawati shuleni?  Nikamwambia najua, wajua, akanijibu halafu tuna misitu mikubwa nchini?
 Baba Makongoro ulivyooondoka kuna mwana hip hop aliimba “wasomi wanakimbilia siasa, Je, nchi itajengwa na nani? Hata mimi najiuliza nchi itajengwa na nani? Sielewi!

Mwalimu alizidi  nitoa tongotongo katika kuandaa  na maswala mengine yenye maslahi kitaifa yasiyohitaji mgawanyiko wa itikadi na uchama  kwa kile  waingereza wanachosema “number do not lie” wakimaanisha  nambari haidanganyi kwa kufanya mambo kwa  “ tathmini onyeshi” moja ni moja na nane si saba, kwakumshangaa  Waziri mwenye dhamana ya Afya  kukinzana na  Makamu wa Rais, kuhusu upungufu  wa madawa kwenye bohari ya Taifa!
Nakamwambia Mwalimu neno “siasa” ni mwiba kwa wananchi si neno  zuri kulizungumza  japo Rais JPM anawapa matumaini kuwa utendaji wake kwa kiasi chake kuna tija imeonekana Mwalimu,  kabla hatujaendelea zaidi   nikatafakari kuwa  ujasiri ni pale unapojua "siasa" si tatizo bali tatizo ni picha na taswira iliyojengeka mtu kuwa "mwanasiasa" ndani ya jamii na jibu tunalo kwa utendaji mzuri wa viongozi wetu  ili kugeuza neno "politics is dirty game". Itabadilika tu hii hali, kama enzi zako Ualimu ulivyoheshimika leo hii unaonekana taaluma ya kawaida! Sisi wenyewe hatupendi Mwalimu.
Nikamwona kifkra shujaa wa India, Mahatma Ghandi na falsafa yake kuwa “I love your Christ but not your Christianity” nikimaanisha  serikali na vyama vya siasa  ni sehemu salama na sera zenye weledi lakini  walioko ndani yake ndiyo kuna kila aina ya ubaya,udhalimu, na siasa chafu japo kuna wasafi na wenye kweli daima. Naipenda sera weledi yenye utekelezaji, itikadi ninayo,na “imani” kwa  kiongozi na mwananchi  mwenye misingi fanikishi ya kuileta “Tanzania ninayoitamani”, si kauli za kutofautiana  za  “makaisari” wetu na sio  ushabiki wa chama. Haya yakifanikiwa mbona “siasa nyeupe” itaonekana na tuishi ili kumuenzi Baba wa Taifa na hilo ndilo kusudi lake, siku siku ya leo tutoe  “speech” za kumsifia ila  hizo  sifa zake ninyi kiuhalisia na kiutendaji  mnaziishi kwenye vyombo vya habari.
Watanzania ni wepesi wa kusahau kama  zao la “kuamua” litaleta watu makini, wazalendo,wenye dira elekevu, na misimamo binafsi   tutakuwa tumefikia kiwango kikubwa katika “mchakato” wa kujitambua na kuutambua ukweli na ule mtazamo wa siasa ni mchezo mchafu (politics is the dirty game) tukiishi ya Baba Makongoro na sio kuienzi siku yake bila matendo sio maneno. Hata  Baba Makongoro kwenye “mjadala” wetu hapendi hilo swala.
Alichopenda ni “Argue, Don’t shout” na hichi ndicho serikali inakinzana na vyama vya upinzani sana, kwasababu kila mmoja anatoa kinachojipendelea ila tukumbuke tunajenga moja, Tanzania yetu katika siku hii ya kumuenzi Baba wa Taifa sio kwa makelele na sifa kedekede bila kuishi aliyoyaishi!
Pumzika kwa amani Mkuu, muda mwingine tutatembeleana!

Description: https://ssl.gstatic.com/ui/v1/icons/mail/images/cleardot.gif

Saturday, 8 October 2016

UKITAKA KUMFUGA CHATU, UANDAE UNGA WA KUMLISHA

Hii ni makala yangu  iliyotolewa leo Oktoba 8, 2016 kwenye gazeti la TanzaniaDaima, kama hukupata nakala yako na kwa kukujali msomaji wa petermmbaga.blogspot.com isome hapa kwa utulivu.



Na
PETER MMBAGA, UDSM(SJMC)

“Ukitaka kumfuga chatu, uandae unga wa kumlisha”  hiyo ni kauli ya “kijana wa zamani”   kwenye kijiwe kimoja nikiwa kwenye harakati za kumng’ojea mgeni  wangu kituo cha daladala  mida ya jioni baada ya jua  kunipiga vilivyo mchana wake, nikamuuliza “kijana wa zamani” unamaanisha nini?
Akanambia kijana huelewi nini? Mimi nina elimu ya mkoloni nayo inanipa nguvu kudadavuadavua  yaliyomo kidogo, Je, wewe vipi?
Nikamwambia nijibu basi  “mzee kijana” akasema “homu weki” hiyo, wakati natafakari kabla  mzee hajatoa hoja ya msingi juu ya maana ya msemo wake, ndipo stori kijiweni zikazidi kunoga, kuna mshikaji moja akazungumza kuhusu  UKUTA(akimaanisha operesheni ya  CHADEMA) aliyotakiwa kufanyika septemba mosi ikasogezwa tena oktoba mosi kisha kuahirishwa kwa mara nyingine.
Jamaa mmoja akadai hawa  maCHADEMA nao wamezidi kila kitu wanahisi wanaonewa, mwacheni  ndugu Magu(Rais John Magufuli) apige kazi bwana! Mzee tunayemwita “mzee wa busara”  akajibu hii ni kizungumkuti kila mtu anavutia kwake ila serikali iwe makini kwa kauli ya rais kusema hakuna siasa  mpaka 2020, sasa kazi ya vyama vya siasa ni nini?
Kuna mvutano wa CUF na Profesa Ibrahimu  Lipumba  nikawa nawaza kichwani mwangu wakati huohuo kuna mbasi akaja na akatusikilizisha sauti  ya Rais JPM juu ya kuhamia Dodoma. Kwa hisia kidogo akataja kuwa haiwezekani baba wa Taifa mwalimu Nyerere alisema makao makuu ni Dodoma hivyo kupinga”.
Mzee anayeuza kahawa akasema naona mmedakwa na kuhamia Dodoma, Yule mleta hadithi za Dodoma akasema “Bongo iliitwa Tanzania kila kitu kilipatikana hapa, get ready with dom” akatia na umombo  kwa mbwembwe kidogo, tukacheka sana!
Uchumi wa Tanzania, au uwepo wa Tanzania unahitaji kutegemeana ili kumvusha mama Tanzania kwenye lindi la umaskini, sasa wakati ninawaza hilo mulemule jamaa mmoja akasema “mgawanyiko wa kiuchumi na kiutendaji unabidi uguse nchi nzima”, serikali si inahama yote bwana!
Tukashindwa kuelewa anamaanisha nini? Akasema ule mlundikano wa wizara hapa Dar, au ukipita mtaa wa Magogoni unaona nini? Tukashangaa, nikamuuliza kwani tatizo ni nini?
Akanijibu “Mbasi nawe unaonekana huoni mbali, mimi naona tugawe wizara hata kimkoa  au kikanda hivi kama Arusha ndiyo kitivo cha utalii Tanzania, ni vema Wizara hata ikawa pale, haya maswala ya bandari na usafirishaji wa maji ukaa “centre” ya mikoa husika kama Dar, Tanga na Mtwara”
Mzee mkongwe akasema ni wazo zuri lakini mbona kwenye ofisi za mkoa ama wizara, ofisi ndogo za mkoa zipo hizo ofisi hata nchi zilizoendelea sidhani kama zina kitu kama hicho! Mbasi mmoja akasema hiyo haitoshi ila ili kuweka mgawanyo wa kiserikali, ili “decentralization” ya serikali za mitaa mpaka serikali kuu hawafiki vyema, hii ni sera ya kibunifu!

Mzee kijana akasema enzi hizo kwenye historia  ya utawala wa Mwingireza  kama vijana mnasoma,  Idara za serikali zilikuwa hazipo mikoani na wakuu wa Idara hawakutaka kuhama Dar, mchakato wa kupata sehemu tulivu ya mji mkuu mpaka kufika mwishoni mwa mwaka 1920, Idara ya kilimo na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mashariki zilihamia Morogoro, Idara ya mifugo ilikwenda Mpwapwa sasa je, kwa mgawanyo huo tu wa kipindi hicho wizara haziwezekani kweli? Tukajiumauma tukijibu “inawezekana mzee, eeh inawezakana mzee ila kwa mipango”
Kuna jamaa akatoa nje mada kidogo akadai “ving’ora viletavyo foleni vitapungua jijini bora waende dom”, tukamshangaa nikajiuliza hivi foleni Dar kumbe inachangiwa na misafara ya hawa waheshimiwa, nikacheka kidogo!
Wakati kahawa inaendelea kuchemshwa mzee wa kahawa akasema “nasikia wakuu wanaharakisha uboreshwaji wa hadhi ya kimataifa  hata kwa viwanja vya ndege Dodoma kurahisisha usafiri na hata mdege  umeshuka juzi toka Kanada”,  kuna mfanyakazi mmoja wa benki akadai mbona ukarabati wa  uwanja Dar unafanyika pia, hapo hakuna hoja labda useme fursa gani zimekwepo baada ya uwepo wa uwanja mkubwa wa Dar, ajira zimetoka na zitakazotoka kwa upanuzi unaoendelea.
Jamaa mmoja akanena “hapa Bongo hawajapaendeleza kivile, nadhani wangepaendeleza Dodoma vyema na nchi kiujumla hata kama wazo ni la tangu uhuru kuhusu kuhama, je, mikakati waliyoanza nayo kwa awamu zilizopita ikoje? Nikamjibu  jibu la swali kwa swali “kuhusu miundombinu kiujumla eeeh?”
Yule jamaa wa benki akamjibu “umefanya utafiti kuwa hawajajiandaa vyema, utafiti mbele ndipo ukosoe”, akabaki tunashangaa, asijue la kujibu!
Nikamuuliza mzee kahawa vipi? Akajibu piga domo kwanza, ndipo nikauliza hivi huo uchumi mnaozungumzia mipango miji inaridhishaje? Mzee wa kahawa akadakia akasema walicho “bugi” muda mrefu Dar haikuwa na mipango miji, na mimi nkamropokea “kazania kahawa wewe”
Mshikaji mmoja akajibu “mzee kaongea bonge la hoja wewe, mipango mikakati hamna jiulize wazo dogo la kujenga hata “hoteli” ya nyota kadhaa pale jirani na uwanja wa ndege wa J.K Nyerere  ili kupambana na ajira, pato la taifa, foleni  pamoja na muda kwa wasafiri  hilo haliwaziki kabisa, hii ndio Tanzania”
Aliposema foleni nikamkumbuka mbasi wangu mmoja aliyenieleza habari za semina moja aliyohudhuria katika hoteli ya Blue Pearl, moja kati ya wasemaji wa hiyo semina alizungumzia hali ya foleni ya Bongo aliyodai inavyosikitisha kwani haiwezekani atoke Afrika kusini kuja Tanzania kwa masaa matatu na kutoka uwanja wa ndege J.K Nyerere mpaka Blue Pearl kwa masaa hayohayo matatu, akastaajabu! Ila sisi hatukustaajabu ndio huku “kwetu” kulivyo!
Mzee wa busara akasema nasikitika  pale “nkulu” akimaanisha Ikulu, hata mashujaa wetu hawathaminiwi hata kwa kumbukumbu angalia, anwani ya nkulu wanaandika barabara ya “Barack Obama” hivi hata kuiita bararaba  ya  Mangi Marealle, Kinjekitie Ngwale au Mirambo. Kuna jamaa muuza chips jirani kwanye kibanda kilichoandikwa  “Hapa Kazi Tu chips” akasema  wakihamia kuna barabara inaweza kuitwa  barabara ya “George Bush”.  Nikamjibu kwa mbwembwe za kimombo “are you serious”. Akanijibu hapa Dar mbona imewezekana?
Kahawa ikawa tayari tukaanza kunywa uchungu wa kichangamsha mwili kile,  ndipo jamaa yetu wa bodaboda akatokea akisema  hii hela kutonekana mwisho wake ni nini?  “Mzee kijana”  akadakia akisema kila sehemu hakuna hela halafu eti majipu yametumbuliwa pesa iko wapi?
Yule jamaa wa benki akasema kwenye uchumi kuna kitu kinaitwa “economic paradoxes”, naona mnashangaa sana uongozi uliopita kulikuwa na ufisadi, na rushwa  na bado pesa ilikwepo lakini sasa hivi hela hamna mnasikia majipu yametumbuliwa mengi.



Mawasiliano kwa namba 0656 859045 au barua pepe petermmbaga29@gmail.com

Monday, 5 September 2016

POGBA HAKWENDA MAN U KUCHEZA TU, KUNA BIASHARA TAYARI IMESHANUFAISHA WATU!

Mourinho(kushoto) na Pogba
Ilionekana biashara kichaa kwa  kocha Arsene Wenger wa  "The Gunners" akasema haiwezi tokea yeye kufanya kitu kama hicho kwenye ulimwengu wa soka. Ndiyo kuna biashara ya ziada nyuma zaidi ya Jose Mourinho kutaka huduma ya uwanjani Man U. Si bure kufanya vile, kuna watu waliwaza.
Wadhamini wa Man U, Adidas na Chevrolet pamoja na wengineo wana siri zao, siri?
Sasa ndivyo biashara imeshafanyika, Agosti 9, Paul Pogba kiungo mfaransa alivunja rekodi ya kuwa mshambuliaji bora duniani kwa kusajiliwa kwa pauni milioni 100, balaa ni kuwa wiki tatu za mwanzo pesa imerudi kwa kuuza jezi pekee, pauni milioni 200 Man U washazitia mfukoni na wanamalizia deni lao kwa Juve  taratibu.
Achana hiyo mwenzake aliyesajiliwa toka PSG, Zlatan Ibrahimovic wiki ya kwanza tu kwenye mauzo ya jumla Man U walilamba pauni milioni 76. Zlatani akasema jezi yake itauza kurudisha hela walizomnunulia Pogba!
Unajua mawazo yao(Adidas na Chevrolet) ? Kibiashara tu kwenye mitandao ya kijamii kabla na baada ya kumsajili walisharudisha hela, cheki lile liubunifu #POGBACK si snapchat, tweeter, Instagram, blogs, websites, na facebook. Dunia ya kidigitali!  Unajua soka la sasa linaangalia nini?
Mchezaji ataingiza shilingi ngapi kwenye mauzo ya jezi, matangazo ya televisheni na mchezaji ana mvuto?
Mikataba ya udhamini  klabu itapata, unadhani Man U ni "wajinga" kupelekea kukosa karibu  dola milioni 100 kila mwaka toka kwa Adidas. Adidas walitaka kijana mwenye "mvuto" kuwepo kwenye picha za matangazo. Sababu moja nzito! Magari ya Chevrolet yalikuwa hayauzi sana UK na Ulaya, ishu kubwa ya kwanza waliyofanikiwa ilikuwa ni kumshusha Pogba kwenye uwanja wa mazoezi wa AON(AON Training Centre) ndani ya ndinga ya kifahari  kali mpya ya Chevrolet Camaro(new model). Utamaduni wa zamani ulizoeleka kumtangaza mchezaji kupitia "press conference", sasa kuna ishu ya ziada za kufanya matangazo ya biashara zingine, mambo yanabadilika.  Kwasasa biashara ya Chevrolet imeanza kukua vyema Uaya, sababu kwenzi nayo hiyo!
Pogba akiwa ndani ya Chevrolet Camaro akiingia uwanja wa mazoezi wa AON siku akitambulishwa

Kwa uchache huo, Pogba anavyo vyote. Nani asimununue japo sio mkali kivile, enzi za kina Andre Pirlo huyu Pogba ana uwezo gani? kibaya zaidi kilichomkimbiza toka Man U  2012 kwenda Juve ni "jitu"  likiwa uwanjani ila sura ya upole, kiungo Paul Scholes, unadhani Sir Alex Ferguson hakuwa na akili.
Zaidi usajili wake hatujaujadili sana kwakuwa ni "kijana mweusi", ubaguzi wote kwenye michezo tena Uingereza kupenda vyao, lakini akachukuliwa kwa bei hiyo!
Unajua kinachotokea mwaka huu wa fedha, Man U watapata faida zaidi  ya dola milioni 665 kwa mwaka 2015/2016 ukiweka pembeni na  pesa walizomsajili Pogba ambazo pauni milioni 100 na " kiasi" fulani ziada ni sawa na  "turnover" ya  19.5%, hawana hasara hivyo!

Adidas wanaelewa biashara ikoje wikiendi ya septemba 10, kuna Manchester derby kati ya Man U na Man City, tayari washatoa viatu vipya  aina ya "Adidas ACE16+Purecontrol Viper Pack" kwa kijana wao Pogba kwajili ya matangazo ni vya teknolojia ya hali juu asikubishie mtu!
Fedha zimerudi ni muda wa biashara ya uwanjani kinachofuata. Si kucheza na kuleta makombe OT tu, huu ni muda wenye akaunti  zenye "maono" zimekwishanona.