Aliandika kwenye akaunti yake ya twitter: "Sasa sijiwezi tena, sipo poa kiakili, na naondoka kwa staha na nashukuru mashabiki wangu."
Hata hivyo, hajafafanua iwapo ataacha sekta ya uimbaji kabisa, au ataacha tu uimbaji wa muziki wa kufoka. Mwanamuziki huyo wa umri wa miaka 33 hata hivyo amesema hataki "kuonewa huruma".
Lil Wayne amekuwa akigonga vichwa vya habari hivi karibuni kwa visa mbalimbali, huku rapa Rick Ross akionekana kujibu maneno ya shabiki aliyehitaji Tunechi kusainiwa Maybach Music Group(MMG) kwa kuandika “Muunganishe Birdman kwenye simu”
Amekuwa na mzozo wa muda mrefu na lebo ya Cash Money Records inayomilikiwa na baba yake kimuziki Birdman, ishu kubwa ni kuhusiana na kucheleweshwa kwa albamu yake ya 11, ambayo imepewa jina Tha Carter V. Alishutumu kampuni hiyo siku kadhaa zilizopita akitumbuiza na Drake mjini Miami.
balaa lingine ni la hivi juzi kati baada ya polisi wa Miami kufika nyumbani kwake kisiwa cha La Gorce baada ya mtu kupiga simu 911 akisema kulikuwa na ufyatuaji risasi. Habari hizo hazikuwa za kweli.
Lil Wayne WEEZY FVerified account@LilTunechi
I AM NOW DEFENSELESS AND mentally DEFEATED & I leave gracefully and thankful I luh my fanz but I'm dun
Hawa ni kati ya wasanii walioguswa;
Missy Elliott @MissyElliott @LilTunechi Prayers up 4 whatever u may be enduring right now this to will pass & may u find PEACE I will always be a fan of your work
Chris Clemons @chrisclemons91
@LilTunechi The game will never be the same!!! Long live the of my generation.
No comments:
Post a Comment