Reli hiyo ya kati ni
ya kutoka Dar es Salaam, Mwanza, Kigoma na inatarajiwa kuunganisha Tanzania na
nchi za Rwanda na Burundi
Wakati wa mazungumzo
ikulu Dar es Salaam Rais Magufuli alisema serikali inataka kuona mambo yakifanyika
na kutoa matokeo bila kupoteza muda, kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu.
Serikali ya Tanzania
imetenga shilingi trilioni moja kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi katika bajeti ya
sasa.
"Sisi tumeamua
kuanza ujenzi na tayari Wakandarasi 32 wamejitokeza kuomba kujenga reli ya kati
kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro umbali wa kilomita 200 za mwanzo na
tutatumia fedha zetu wenyewe," alisema Dkt Magufuli kwa mujibu wa taarifa
kutoka ikulu.
"Kazi hii
tunataka ianze mwaka huu wa fedha, kwa sababu upembuzi yakinifu na usanifu
umeshafanyika, kwa hiyo na nyie ongezeni kasi ili mradi huu wote ukamilike,
nataka uwe umekamilika kabla sijaondoka madarakani."
Dkt Magufuli alisema
mradi huo una manufaa makubwa kwa Tanzania na nchi nyingine nane zinazotegemea
bandari ya Dar es Salaam na kwamba kukamilika kwake kutatoa mchango mkubwa
katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania ambayo inataka kuwa nchi ya kipato cha kati
ifikapo mwaka 2025.
Kwa mujibu wa taarifa
ya ikulu, Bw Qian aliahidi kuwa Serikali ya China itaongeza msukumo katika
uharakishaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa reli hiyo
ya kati.
"Mheshimiwa Rais
Magufuli nimeielewa dhamira yako na kiu uliyonayo, naona kabisa kwamba dhamira
ya kisiasa ipo ya kutosha, tunachotakiwa kukifanya ni kuwasukuma wataalamu wetu
waongeze kasi," alisema.
„Na mimi nakuahidi
kuwa tulikuwa tunakwenda kwa kasi ya kilometa 100 kwa saa, sasa tutaongeza na
kwenda kilometa 200 kwa saa."
Chanzo: BBC Swahili
Unaweza toa comment yako hapo chini!
No comments:
Post a Comment