Tuesday 11 October 2016

KINDA WA MIAKA KUMI ALA MKATABA JUVE

Kinda Rasheed Al Hajjawi
Mabingwa hao wa Italia, Juventus wamemchukua “kinda”  mpalestina Rasheed Al Hajjawi mwenye miaka 10, baada ya kuzungumzwa sana kwenye “media: za kiarabu siku za karibuni.   Licha ya kukulia mjini Gaza, “kinda” huyo alizaliwa na kukulia Norway.

Habari za kunaswa kwa kinda huyo zimekuja baada ya “skauti ya kisasa” ya kunyaka matukio, habari na vipaji ya mtandao wa kijamii kupitia Youtube, huku wakibashiri kuwa ni Lionel Messi mpya. ndani ya wiki ya karibuni  siku ya Jumanne pia kumetokea dogo mwingine kwa jina la Karamoko Dembele mwenye miaka 13, aliyefanya "appearance"  kwa dakika 10 za mwisho kwenye mechi ya Celtic U20's katika ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Hearts.

Dembele akiingia uwanjani 

DOGO SI WA MCHEZOMCHEZO
Kweli si wa mchezomchezo kabla ya kutua alishaibuka kwenye mazoezi ya klabu ya Liverpool, na pia kuwa karibu na mastaa wa Real Madrid.
Dogo Rasheed akiwa Liverpool

Kwenye mtandao wa “facebook”  dogo kazitundika picha za mastaa kadhaa aliopiga nao stori.

 
Dogo akiwa na kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane


No comments:

Post a Comment