Sir Bob Charlton enzi zake. |
Leo bwana ndiyo “birthday” ya shujaa Sir Robert "Bobby"
Charlton alizaliwa 11 Oktoba 1937. Ni mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu wa
Uingereza, Anajulikana kama mmojawapo wa viungo wa kati wenye uwezo wa hali ya
juu wa muda wote. Nembo muhimu katika timu ya taifa ya Uingereza ambapo
alishinda Kombe la Dunia na Ballon d'O r mwaka 1966. Yeye alicheza karibu muda
wote katika klabu yake ya Manchester
United, ambapo alikuwa mashuhuri kwa uwezo wake wa kushambulia na kupiga
mashuti yaliypachikwa jina "Long Lange Shot" yaliyopigwa toka umbali
mrefu. Alionywa kwa kadi
mara mbili tu katika maisha yake ya soka; mara moja dhidi ya Argentina mwaka
1966 katika Kombe la Dunia, na katika mechi ya ligi kuu dhidi ya Chelsea.
Alizaliwa huko Ashington, Northumberland. Charlton alicheza mechi yake ya
kwanza kwa Manchester United katika kikosi cha kwanza mwaka 1956, na zaidi ya
misimu miwili alipata nafasi ya uhakika katika timu. Ni moja ya wachezaji
walionusurika katika ajali ya anga mjini Munich mwaka 1958 baada ya kuokolewa
na Harry Gregg, baada ya kuisaidia timu ya Mashetani Wekundu kushinda kombe la
Football League mwaka 1965 pia alishinda Kombe la Dunia na medali katika timu
ya taifa ya Uingereza mwaka 1966 na kombe la “Football League” akiwa na
Mashetani Wekundu mwaka uliofuata. Mwaka 1968 akiwa nahodha wa Manchester United
alishinda Kombe la Ulaya akifunga mabao mawili katika mechi ya fainali .
Amefunga mabao zaidi kwa United (249) kuliko mchezaji mwingine yeyote na
kutokea kuwa mfungaji bora England wa muda wote wa timu ya Taifa kwa mabao 49 na Wayne Rooney kumpiku juzi kati kwa goli 50 katika
mechi 107 alizocheza.
Hivyo kuanzia Mei 1968
hadi Septemba 2015, kwa Rooney kuvunja rekodi hiyo ndani ya Uingereza. Bobby
Charlton alikuwa na rekodi ya kucheza mechi nyingi kwa Manchester United (758),
kabla ya kuzidiwa na Ryan Giggs. Aliichezea Uingereza mara nne katika Kombe la
Dunia (1958, 1962, 1966, na 1970), na kuisaidia Uingereza kushinda shindano
hilo mwaka 1966.
Sir Bob Charlton siku za karibuni |
Wakati wa kustaafu kwake
kutoka timu ya England mwaka 1970, alikuwa ameichezea timu ya Taifa mechi nyingi
kuliko mchezaji yeyote (mara 106 katika ngazi ya juu) ila Wayne Rooney kaivunja
kwa mechi 107, kwa aliyocheza mwaka jana
dhidi ya Uswisi. Rekodi hii tangu wakati huo ilikuwa kwa upande wa Bobby Moore
na Peter Shilton. Aliondoka Manchester United na kuwa meneja wa Preston North
End katika msimu wa 1973-1974. Ambapo alikuwa mchezaji-meneja na baadaye kuwa
mkurugenzi wa Wigan Athletic, Msimu uliofuata akawa mwanachama wa bodi ya
wakurugenzi Manchester United tangu mwaka 1984 mpaka sasa msimu wa 2016/17.
Huyu ndiye Sir Robert
"Bobby" Charlton aliyeshikilia rekodi ya ufungaji wa mabao Uingereza
kwa miaka 47, HAPPY BIRTHDAY LEGEND!
Unakaribishwa kuacha comment yako hapo chini!
No comments:
Post a Comment