Saturday 15 October 2016

SIMBA I KILELENI

Mchezo wa VPL kati ya Simba iliyokuwa mwenyeji wa Kagera Sugar umemalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa goli mbili kwa bila.
Magoli ya Simba yamefungwa na beki Mzarimu Yassin akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Shiza Kichuya katika dakika ya 44 na goli la pili likifungwa na Shiza Kichuya kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 75.
Ushindi huo unaiwezesha Simba kufikisha alama 23 katika michezo tisa iliyocheza, ikishinda michezo saba na kutoa sare miwili na ikiwa na mchezo mmoja mkononi, Kagera Sugar inasalia kuwa na alama 15 ikiwa katika nafasi ya tatu ya msimamo wa VPL.


No comments:

Post a Comment