Jumba hilo ambalo jina
lake kamili ni Jumba la Amani na Usalama la Julius Nyerere limejengwa kwa
ufadhili kutoka Ujerumani.
Litakuwa makao ya
idara ya Amani na Usalama ya AU na litatumiwa pia na maafisa wa kutoa tahadhari
ya mapema kuhusu mizozo barani pamoja na kuratibu juhudi za kulinda amani za
AU.
Ujenzi wa jumba hilo,
ambalo ukubwa wake wa sakafu ni mita 13,500 mraba na linaweza kutumiwa na
wafanyakazi 360, uligharimu euro 27 milioni.
Jumba hilo afisi za
kufanyia kazi, vyumba vya mikutano vya kutumiwa na Baraza la Amani na Usalama,
chumba cha kuratibia shughuli, maktaba na vyumba vya shughuli za pembeni.
Mwalimu Nyerere,
ambaye alikuwa rais wa Tanzania hadi 1985, alikuwa mmoja wa viongozi
waanzilishi wa Muungano wa Nchi za Afrika (OAU) ambao sasa ni Umoja wa Afrika
(AU).
Alishiriki sana katika
jitihada za kuendeleza bara la Afrika na kusaidia mataifa ambayo hayakuwa
yamepata uhuru kujipatia uhuru wake.
Mwalimu Nyerere
alipigania sana kumalizwa kwa ubabe wa Wazungu katika nchi za Rhodesia (sasa
Zimbabwe), Afrika Kusini, na taifa la Kusini Magharibi mwa Afrika/Namibia (sasa
Namibia).
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment