Ni
HISTORIA ILIOJEEE, Mtanzania pekee aliyabahatika kuteuliwa kwa kofia ya waziri mkuu na marais wawili
tofauti, hapa namaanisha Baba wa Taifa
mwl. Julius Kambarage Nyerere pamoja
na Rais wa awamu pili ndugu Alli Hassani
Mwinyi, si mwingine ni ndugu Cleopa
David Msuya .
Mara ya kwanza ilikuwa ni siku 13 baada ya uchaguzi
mkuu wa mwaka 1980 wa chama kimoja, ambapo kama kawaida mnapotoka uchaguzini,
moja ya kazi za kwanza ya Rais ni kumtangaza Waziri Mkuu, na ndipo hapa
November 07, 1980 Mwl. Julius Nyerere akamtangaza Cleopa Msuya kuwa Waziri
mkuu. huyu ndiye ndugu Cleopa David Msuya aliyezaliwa novemba 4, 1931, huko wilayani
Mwanga, tarafa ya Usangi katika kijiji cha Chomvu mkoani Kilimanjaro.
Ni kizazi cha wasomi wa Chuo Kikuu cha Makerere toka
mwaka 1952 mpaka 1955, ndugu Msuya aliyeanza kwa utumishi wa sekta ya umma, maendeleo ya vijiji toka mwaka
1956 hadi 1964. Kuanzia mwaka 1964 alihudumu kama katibu kiongozi kwenye wizara
tofauti tofauti ikiwemo wizara ya maendeleo ya jamii na utamaduni kutoka mwaka
1964 hadi 1965, wizara ya makazi na maendeleo ya maji kati ya mwaka 1965 mpaka
1967, 1967 mpaka 1970 ilihudumu kwenye wizara ya uchumi na mipango na baadaye
akahamishiwa wizara ya fedha toka mwaka 1970 hadi 1972.
Februari mwaka 1972 aliteuliwa kuwa waziri wa fedha
mpaka mwaka 1975 aliula tena kuiongoza wizara ya viwanda na biashara hadi mwaka 1983, alipoteuliwa kwa mara ya
kwanza kushika wadhifa wa kuwa waziri mkuu.
Alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa pili wa Rais, ndugu Msuya hakumaliza
awamu yote kwani mnamo Februari 24, 1983
alibadilishwa na nafasi yake kuchukuliwa na Hayati Edward Sokoine ambaye naye
hakumaliza awamu ile kwani alifariki mwaka mmoja tu baadaye yaani April 12,
1984.
Awamu pili
ndugu Msuya aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu
Desemba, 1994 alipoteuliwa na Rais Ali Hassani Mwinyi kupokea nafasi ya John Malecela ambaye alijiuzulu
siku mbili kabla ya uteuzi huu wakati kikao cha NEC-CCM, kikiendelea. Hivyo
kutokana na katiba kuruhusu akawa Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais wa
jamhuri ya Muungano.
Hapo nyuma
mnamo mwaka 1992, nchi yetu iliingia katika mageuzi makubwa ya mfumo wa kisiasa
pale ilipoamua kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa. Mabadiliko haya
yalisababisha Katiba ya nchi ifanyiwe mabadiliko ili kuruhusu mfumo huu wa
demokrasia ya vyama vingi ufanye kazi nchini ambapo nafasi mbalimbali za
uongozi pia ziliguswa na mabadiliko hayo hivyo mwaka 1994, kufuatia mfumo wa
demokrasia ya vyama vingi kuruhusiwa nchini ilijitokeza haja ya kuifanyia
mabadiliko nafasi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili
iweze kukidhi mageuzi haya ya kisiasa. Ilionekana kwamba katika mfumo huu mpya
wa demokrasia ya vyama vingi si rahisi tena kuwa na Makamu wa Rais wawili kama
ilivyokuwa wakati wa mfumo wa demokrasia ya chama kimoja hivyo ndugu Cleopa
mwana David ndiye
aliyemalizia rojo ya tamu na shubiri ya kuwa na vyeo viwili vikubwa kwa
wakati mmoja.
Nafasi alizokuwa nazo aliziacha kwenye uchaguzi mpya
wa kihistoria wa vyama vingi uliofanyika kwa mara ya kwanza mwa 1995, na
baadaye kuteuliwa kuwemo kwenye bunge maalum la katiba nafasi aliyodumu nayo
hadi kustaafu mwaka 2000. Alipata nafasi ya kuwa nwenyekiti wa kilimanjaro gvt
forum mwaka 2006.
Hadi kustaafu kwake ameeendelea kuwa kada mwaminifu
wa chama cha mapinduzi hadi hii leo.
Ni HISTORIA ILIOJEE kwetu sisi WAUNGWANA kumgusia ndugu Cleopa Msuya ambaye kipekee mpaka sasa
ndiye Waziri Mkuu wa kwanza Tanzania kupitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano
kwa mtindo wa sasa kuthibitishwa na Bunge na pia kushika vye vikubwa awamu
mbili yaani Waziri mkuu kikiongozana na Makamu wa Pili
wa Rais wa Jamhuri na baadaye
Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais
kwa wakati mmoja kwasababu ni HISTORIA ILIOJEEE!!!!
No comments:
Post a Comment