Showing posts with label NEWS. Show all posts
Showing posts with label NEWS. Show all posts

Wednesday, 19 October 2016

MAGAZETI YA LEO HAYA HAPA UNAWEZA UKAYAPITIA

Kile kinachoonekana kwenye front pages za magazeti ya leo tarehe 19.10.2016

Monday, 17 October 2016

HII NI TAARIFA KUTOKA JKT KWA UTAPELI UNAENDESHWA KUTUMIA JINA LAO


VIDEO: RAIS JPM ADAI MASSABURI ALIKUWA NA WAKE WANNE AU WATANO

Rais JPM(kulia) akitoa neno kwenye ibada ya kumuaga Dk. Massaburi kwenye viwanja vya Karimjee
Mapema leo Okkoba 17 2016, ilikuwa ni shughuli ya kumuaga aliyekuwa meya wa jiiji la Dar Es Salaam Dk. Didas Masaburi(20101-2015) aliyefariki Oktoba 12, 2016.
  Sasa “stori” ni kuwa Rais John Magufuli  alitoa  bonge la “headline” wakati wa kutoa hotuba kwa wananchi baada ya msomaji wa wasifu wa Dk. Masaburi kutaja kuwa  marehemu ameacha mke mmoja, Rais Magufuli alipata nafasi ya kuzungumza na kusema anafahamu Dk. Masaburi alikuwa na wake wanne au watano na hata watoto anafahamu kuwa anao zaidi ya 20, aidha Rais Magufuli amewaomba watoto wa marehemu kushikamana na kuwa wamoja.
Kuangalia video hii bonyeza hapa


 Chanzo: Millardayo

Sunday, 16 October 2016

UCHAGUZI MAREKANI: TRUMP ATAKA CLINTON "AFANYIWE UKAGUZI WA DAWA"


Mgombea wa Republican, Bw. Donald Trump
Mgombea kiti cha Urais kwa tiketi ya chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump, amemshutumu mpinzani wake Bi Hillary Clinton kwa kutumia aina fulani ya dawa, wakati wa mjadala wao uliopita wa moja kwa moja wa runinga.

Anasema kuwa alikuwa na haiba mwanzo mwanzo wa mjadala huo.
Sasa anapendekeza kuwa wafanyiwe majaribio ya matumizi ya dawa, kabla ya kufanyika kwa mjadala wao wa mwisho hapo siku ya Jumatano ya wiki hii.
Katika mkutano wake wa hivi punde uliofanyika New Hampshire, Bwana Trump kwa mara nyingine, amedai kuwa kuna njama za kumuibia kura.
Timu ya kampeini ya Bi Clinton, imesema kwamba wapigaji kura, sasa wameona bayana kile anachokiita juhudi za aibu za Bwana Trump za kutaka kuhujumu shughuli za upigaji kura.
Trump, anazidi kudidimia katika majimbo mengi, huku akikabiliwa na madai ya udhalilishaji wanawake kingono.


Chanzo: BBC Swahili

SHIRIKA LA NDEGE LA LA KENYE LAAHIRISHA SAFARI KISA WAFANYAKAZI HAWAJATOKEA KAZINI



Shirika la ndege la Kenya Airways limeahirisha safari zake tano za kwenda ndani na nje ya nchi leo October 16 2016 kutokana na upungufu wa Wahudumu wa ndege kazini.
Taarifa inasema sababu hasa ya kuahirisha safari hizo tano za MombasaKilimanjaro,JubaMaputoHarare na Lusaka ni kutofika kazini kwa Wahudumu wa ndege ambao wamepangiwa zamu kwa wakati huo.
Imeelezwa kuwa baadhi ya Wafanyakazi wa shirika hilo hawajaripoti kazini toka Ijumaa iliyopita ambapo shirika linaendelea kufatilia kujua chanzo ni nini na jinsi ya kutatua tatizo na Mwajiri.
Kwa utaratibu ndege za abiria huwa na masharti yake kwenye kila safari ikiwa ni pamoja na kuwa na namba flani ya idadi ya Wahudumu ndani ya ndege ambayo ni lazima itimie, sasa kutokana na Wahudumu wa Kenya Airways kuwa wachache imebidi ndege nyingine zisisafiri.

Chanzo: Millardayo



Saturday, 15 October 2016

UJENZI WA RELI MPYA TANZANIA KUHARAKISHWA

Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli akiagana na Waziri wa Biashara toka China, Bw. Qian Keming baada ya mazungumzo, Ikulu jijini Dar Es Salaam

Mradi wa ujenzi wa reli ya kati nchini Tanzania unatarajiwa kuharakishwa kufuatia mazungumzo kati ya Rais John Magufuli na Naibu Waziri wa Biashara wa China Qian Keming.
Reli hiyo ya kati ni ya kutoka Dar es Salaam, Mwanza, Kigoma na inatarajiwa kuunganisha Tanzania na nchi za Rwanda na Burundi
Wakati wa mazungumzo ikulu Dar es Salaam Rais Magufuli alisema serikali inataka kuona mambo yakifanyika na kutoa matokeo bila kupoteza muda, kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu.
Serikali ya Tanzania imetenga shilingi trilioni moja kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi katika bajeti ya sasa.
"Sisi tumeamua kuanza ujenzi na tayari Wakandarasi 32 wamejitokeza kuomba kujenga reli ya kati kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro umbali wa kilomita 200 za mwanzo na tutatumia fedha zetu wenyewe," alisema Dkt Magufuli kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu.
"Kazi hii tunataka ianze mwaka huu wa fedha, kwa sababu upembuzi yakinifu na usanifu umeshafanyika, kwa hiyo na nyie ongezeni kasi ili mradi huu wote ukamilike, nataka uwe umekamilika kabla sijaondoka madarakani."
Dkt Magufuli alisema mradi huo una manufaa makubwa kwa Tanzania na nchi nyingine nane zinazotegemea bandari ya Dar es Salaam na kwamba kukamilika kwake kutatoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania ambayo inataka kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
Kwa mujibu wa taarifa ya ikulu, Bw Qian aliahidi kuwa Serikali ya China itaongeza msukumo katika uharakishaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa reli hiyo ya kati.
"Mheshimiwa Rais Magufuli nimeielewa dhamira yako na kiu uliyonayo, naona kabisa kwamba dhamira ya kisiasa ipo ya kutosha, tunachotakiwa kukifanya ni kuwasukuma wataalamu wetu waongeze kasi," alisema.
„Na mimi nakuahidi kuwa tulikuwa tunakwenda kwa kasi ya kilometa 100 kwa saa, sasa tutaongeza na kwenda kilometa 200 kwa saa."





Chanzo: BBC Swahili




Unaweza toa comment yako hapo chini!

VIGEZO VYA KUPATA MKOPO VYAWEKWA WAZI

Naibu Waziri wa Elimu, Injiania Ester Mayanja
Kama umekosa mkopo wa bahati mbaya hivi ni vigezo viulivyokuwa vikizingatiwa zaidi, hayo yamewekwa wazi baada ya Bodi ya mkopo ya wanafunzi wa elimu ya juu hapa nchini  kuwa imetangaza majina ya wanufaika wapya wa mkopo kwa mwaka mpya wa masomo 2016/2017.
Akizungumza na waandishi wa habari Naibu Waziri Elimu,Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya alisema, “Tumeangalia sifa zifuatazo: fani ya kwanza tumesema awe kwenye fani ya sayansi za tiba na afya, ya pili ualimu wa sayansi na hisabati, ya tatu uhandisi wa viwanda,kilimo, mifugo, mafuta na gesi asilia, sayansi asilia na sayansi ya ardhi,ufanisi majengo na miundo mbinu.”
“Lakini pia tumesisitiza wale wenye mahitaji maalum,kama vile ulemavu na uyatima,lakini hata tukisema kwamba uyatima hatumaanishi yatima mwenye uwezo, maana yake anaweza kuwa amefiwa na mzazi mmoja mwingine yupo lakini pia mzazi aliyetangulia ameacha fursa za kutosha kiasi kwamba hali ni nzuri,huyo tunasema yule ambaye ni yatima maskini,”alisisitiza.
“Vile vile ufaulu, na ufaulu huo uwe katika maeneo yale ya vipaumbele kwa mfano unaweza ukawa umefaulu masomo ya kukuwezesha kuingia kwenye sayansi pengine ufaulu wako hauko wa juu sana, pengine tuchukulie tutaanza na wa division 1, wakishajaa unaingia 2, wakishajaa unaendelea. Kwahiyo hatutaweza kumchukua wa chini wakati mwingine wa juu bado hajapata kwasababu hiyo inatusaidia katika upimaji wa haki,”aliongeza.
Aidha mhandisi Manyanya amesema kuanzia mwaka huu wa masomo wanufaika wote wa mikopo watakopeshwa kulingana na uwezo wao kiuchumi katika vipengele vyote vya mikopo.
Hii hapa “press release” ya taarifa hiyo;

TCRA YAWATAKA MAWAKALA WASIINGIZE BIDHAA ZA SAMSUNG NOTE 7

Mamlaka ya wawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka wafanyabiashara wenye leseni za kuingiza simu nchini, zinazotolewa na mamlaka hiyo, kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Kampuni ya Samsung ya kurejesha simu za kisasa za Samsung Galaxy Note 7 baada ya kubainika zina matatizo ya betri. Akizungumza Dar es Salaam Ijumaa hii na gazeti la habari leo, meneja mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy, alisema ni vyema mawakala hao wakatekeleza maagizo hayo, kwani simu hizo ni hatari kuendelea kutumika.

“Simu hiyo tayari Samsung wenyewe wamesema ina matatizo ya betri na mara mbili sasa imelipuka, hakuna faida ya mtu kuendelea kuitumia unaweza ukasababisha hatari kubwa, inapolipuka inaweza kukuondoa mikono, inaweza kulipua nyumba na matatizo mengine tunawataka wenye simu hizo kuziridisha haraka,” alisema Mungy.
“Taarifa tulizonazo haijaingia sana hapa nchini lakini wapo walioletewa kama zawadi kutoka nje ya nchi nawaomba warudishe huko kuepuka matatizo yanayoweza kujitokeza,” aliongeza.
Samsung iliwataka watu waliokuwa wamenunua jumla ya simu milioni 2.5 mwezi Septemba mwaka huu, kuzirejesha madukani baada ya wateja wengi kulalamika kwamba betri za simu hizo zilikuwa zinalipuka. Katika hatua nyingine, wiki iliyopita, Kampuni hiyo ya Samsung ya Korea Kusini ilitangaza kuwa imesitisha utengenezaji wa simu aina ya Galaxy Note 7.

Aidha Mungy aliwataka wananchi ambao tayari wanatumia simu hizo kuzizima na kuzirudisha haraka katika maduka walikozinunua ili kuepusha hatari ambayo tayari Samsung wameshaitoa.


MAGAZETI YA LEO YAPO HAPA KWA AJILI YAKO!

Ebwana eeh!  Front Pages ya baaadhi ya magazeti ya leo  Oktoba 15, 2016 yapo hapa kwa ajili yako msomaji wangu.














Friday, 14 October 2016

BREAK NEWS: ALLOCATION YA MKOPO KWA WALIOOMBA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

 Hii ndio Batch ya kwanza ya majina yapatayo 3966
 Kutazama Bofya hapa







Toa comment yako kwa kile ulichokiona!

KWELI WEWE NI BABA WA TAIFA

Usiyoyajua kuwa MWL. JULIUS KAMBARAGE NYERERE yanayofanya kuwa na heshima nzito:
1.Alizaliwa tarehe 13/04/1922 Butiama na kufariki tarehe kama ya leo 14/10/1999 kule London.Ni Rais wa kwanza Afrika kuachia madaraka kwa hiari yake mwenyewe.
2.Ni Rais wa kwanza kuhama Ikulu na kwenda kuishi kwenye nyumba aliyoijenga kwa mkopo akiwa bado Raisi.
3.Ni kati ya Rais aliyekuwa analipwa mshahara mdogo duniani na pengine kati ya raisi aliyewahi kulipwa mshahara mdogo barani Afrika mpaka sasa.
4. Ni Mtanganyika wa kwanza kusoma chuo kikuu nchini Uingereza na Muafrika wa pili kupata Degree nje ya Afrika, akisomea English, Political Economy, Social Anthropology, British History, Economic History, Constitutional Law, and Moral Philosophy.
5. Ni kiongozi aliyeisaidia China kuingia Umoja wa Mataifa na hotuba yake maarufu akisema
kwamba,"Umoja wa Mataifa si serikali ya dunia bali ni sehemu ambayo dunia nzima inakutana,
kwahiyo kumtoa China katika umoja wa mataifa ni kumtoa kuwa sehemu ya dunia".
6. Ndio mwanzilishi wa harakati za kupinga ubaguzi wa rangi Afrika ya Kusini- Anti Apartheid Movement mwaka 1959 pamoja na Trevor Huddleston nchini Uingereza.
7. Ni mmoja kati ya waanzilishi wa Umoja wa Afrika, 1963.
8. Amezisaidia nchi nyingi za Afrika kupata uhuru kuliko mtu mwingine yoyote katika historia ya ukoloni, nchi hizo ni Zambia (1964), Malawi (1964), Botswana (1966), Lesotho (1966), Mauritius (1968), Swaziland (1968) and Seychelles (1976) na baadae 1975 (Mozambique), (Angola), 1980 (Zimbabwe), 1990
(Namibia) na 1994 (South Africa).
9. Mwaka 2009 alitajwa na raisi wa mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa kama "World Hero of Social Justice".
10. Amepokea shahada mbalimbali kutoka, University of Edinburgh (UK), Duquesne University (USA), University of Cairo (Egypt), University of Nigeria (Nigeria), University of Ibadan (Nigeria), University of Liberia (Liberia), University of Toronto (Canada), Howard University (USA), Jawaharlal Nehru University (India), University of Havana (Cuba), National University of Lesotho, University of the Philippines, Fort Hare University (South Africa),Sokoine University of Agriculture (Tanzania), and Lincoln University (PA, USA).
11. Alipokea Tuzo ya Order of José Marti Cuba 1975, Order of the Aztec Eagle (Collar) Mexico 1975, Order of Amílcar Cabral Guinea Bissau 1976, the Nehru Award for International Understanding in 1976, the Third World Prize in 1982, Order of Eduardo Mondlane
Mozambique 1983, the Nansen Medal for outstanding services to Refugees in 1983, Order of Agostinho Neto Angola 1985, Sir Seretse Khama SADC Medal 1986, Joliot-Curie Medal of Peace 1988, the Lenin Peace Prize in 1987, the International Simón Bolívar Prize in
1992, and the Gandhi Peace Prize in 1995, Statesman of the 20th century by the Chama Cha Mapinduzi 2000, Order of the Companions of O. R. Tambo (Gold) South Africa 2004, Royal Order of Munhumutapa Zimbabwe 2005, Most Excellent Order of the Pearl of Africa (Grand Master) Uganda 2005, Order of Katonga Uganda 2005, National Liberation Medal Rwanda 2009, National Liberation Medal Rwanda 2009, Campaign Against Genocide Medal Rwanda 2009, Order of the Most Ancient Welwitschi Mirabilis Namibia 2010, Tanzania Professional Network Award 2011, Order of Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Tanzania 2011, National Order of the Republic (Grand Cordon) Burundi 2012 and Order of Jamaica, Jamaica.
12. Mwaka 2007 Rais Yoweri Museveni wa Uganda alimpa tuzo ya Katongo, Medali ya juu kuliko zote ya Jeshi la Uganda kwa heshima ya upinzani wake dhidi ya ukoloni na serikali ya Idi Amin.
13. Mitaa, barabara, majengo, vituo, shule, vyuo na vitu vilivyopewa jina lake; Daraja la Nyerere-Kigamboni,Julius Nyerere University of Kankan, in Kankan, Guinea, Nyerere Drive,Gaborone (1.6 km) in Botswana, Nyerere Avenue, Mombasa (1.5 km)
and Nyerere Road, Kisumu (2 km) in Kenya, Julius Nyerere Street, Windhoek (1.1 km) in Namibia, Julius Nyerere Street, Durban (0.5 km) in South Africa, Nyerere Road, Kitwe (1.4 km) in Zambia, Julius Nyerere Way, Harare (1 km) in Zimbabwe, Julius Nyerere International Airport, Julius Nyerere International Convention Centre, Nyerere Day- Public Holiday 14/10, Nyerere Cup, Nyerere Road, Unguja, Zanzibar (6.5 km), Nyerere Secondary School in Mwanga District and J.K. Nyerere Secondary School in Moshi, Kilimanjaro Region, Mwalimu J. K. Nyerere Secondary School in Mbozi District, Mbeya Region, Nyerere Memorial School in Korogwe, Tanga Region, Nyerere High School Migoli in Iringa Region, Nyerere Secondary School in Unguja, Zanzibar, Mwalimu Nyerere Foundation, Mwalimu Nyerere Museum Centre and Mwalimu Nyerere Memorial Academy- Tanzania.
14. Baadhi ya vitabu alivyoviandika ni, Freedom and Unity (Uhuru na Umoja), Freedom and Socialism (Uhuru na Ujamaa), The Arusha
Declaration, Education for self-reliance, The varied paths to socialism, The purpose is man, Socialism and development, Freedom and Development (Uhuru Na Maendeleo), Ujamaa, Crusade for Liberation, Education for Self-Reliance, na Uongozi na Hatima ya Tanzania.
15. Pamoja na kujulikana kama - Baba wa Taifa la Tanzania, Nchi za Kusini mwa Afrika zinamtambua kama baba wa Ukombozi wa Nchi za Kusini.
16. Pamoja na kujua lugha ya Kiswahili na Kiingereza kwa Ufasaha - pia alikuwa akifahamu lugha ya Kigiriki na Kilatini.
17. Julius Nyerere ameandikwa kwenye kitabu cha Enyclopia kama mtu pekee duniani katika historia ya karne ya 21, aliyeweza kuwafanya watu wa makabila, dini, asili na historia tofauti kujiona kama watu wamoja.

TUJIKUMBUSHE: RAIS MSTAAFU BENJAMIN WILIAM MKAPA AKITANGAZA KIFO CHA MWALIMU

Leo ni kumbukumbu ya miaka 17 ya kifo cha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, tukiamini kwa mengi mazuri  aliyoyatenda ila kwa vitendo vyenye weledi pekee.
Mwalimu Nyerere(kushoto) na Rais wa awamu ya tatu, Ndugu Benjamin Mkapa

Kwa kukumbuka siku hii, nakuletea video ya Rais mstaafu enzi hizo mwaka 1999, ndugu Benjamin Wliiam Mkapa akitangaza tanzia hii.
    Bofya hapa kutazama 

MAJINA YA WANAFUNZI WOTE WALIOCHAGULIWA SOKOINE UNIVERSITY OF AGRICULTURE KWA SELECTION YA PILI

 
                                                        Kutazama majina bofya hapa



Unaweza kuacha comment yako hapa kwa kile ulichokiona!

TCU WAACHIA SELECTION YOTE YA WANAFUNZI KUJIUNGA VYUO VIKUU MBALIMBALI TANZANIA KWA MWAKA WA MASOMO 2016/2017

                                                 
                                                               Bonyeza hapa kuangalia



Unakaribishwa kuacha comment yako kwa kile ulichokiona!

Wednesday, 12 October 2016

ETHIOPIA KUFANYA MAGEUZI MFUMO WA UCHAGUZI


Kansela Merkel akikamilisha ziara yake Afrika ameahidi kutoa mafunzo kwa maafisa wa polisi wa Ethiopia kuhusu namna ya kukabiliana na waandamanaji. Ametaka waandamanaji wapewe uhuru wa kuandamana na uhuru kwa wapinzani.
Waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn amesema serikali yake inataka kufanya mageuzi ya mfumo wa uchaguzi, ambao kwa muda mrefu umeutenga upinzani na kuchangia kutokea kwa maandamano mabaya ambayo yamedumu kwa miezi kadhaa. Haya yanajiri wakati Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akimaliza ziara yake nchini humo ambapo amesema waandamanaji waruhusiwe kuandamana.
Waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn amewaambia wanahabari kuwa “kufuatia mfumo uliopo sasa wa uchaguzi nchini humo, asilimia 51 ya kura inatosha kutwaa ushindi wa viti vyote". Na sasa serikali yake inataka kufanya marekebisho ili kuhakikisha mfumo huo unabadilishwa ili watu wote wakiwemo wapinzani wawakilishwe bungeni.

Chini ya mfumo uliopo sasa, muungano wa Hailemariam ambao ndio unatawala, ulishinda viti vyote 546 vya ubunge katika uchaguzi mkuu, uliofanywa mwaka jana. Hii hapa kauli ya Hailemariam kuhusu suala, la demokrasia na usalama nchini mwake."Ethiopia imejitolea kukuza demokrasia.Ethiopia imejitolea kuwa na demokrasia ya vyama vingi kulingana na katiba yetu. na Ethiopia imejitolea kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa. Lakini Ethiopia pia inapinga ghasia ya misimamo mikali au makundi yanayojihami kwa fujo".
Hailemariam aliyasema hayo baada ya kukutana na mgeni wake Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, akimaliza ziara yake ya siku tatu barani Afrika, ambapo amesema demokrasia iliyoimarika inahitaji kuwepo na upinzani pamoja na uhuru wa vyombo vya habari. Ameitaka Ethiopia kuwapa uhuru waandamanaji bila ya ukandamizaji wa aina yoyote. Kando na kuhimiza serikali kufanya mazungumzo na upinzani, Merkel pia ameahidi kuwa, nchi yake itatoa mafunzo kwa maafisa wa polisi wa Ethiopia kuhusu namna ya kukabiliana na waandamanaji.

Akiwa Ethiopia, Kansela Merkel amemwambia mwenyeji wake Waziri Mkuu Desalegn kuwa waandamanaji waruhusiwe kuandamana na kuwa hatua yoyote ya vyombo vya usalama iwe kulingana na sheria. Kadhalika amesema wanaharakati wa upinzani na watetezi wa haki za kibinadamu wanapaswa kuwa na uhuru wa kutekeleza majukumu yao. Lakini Waziri Mkuu Hailemariam amepinga madai kuwa maafisa wa polisi walitumia mbinu za fujo dhidi ya waandamanaji, na kuahidi kuwa serikali yake itachunguza visa hivyo.
Wiki iliyopita, zaidi ya watu 50 waliuawa kwenye mkanyagano baada ya polisi kujaribu kuwatawanya waandamanaji. Hali iliyosababisha kuongezeka kwa maandamano zaidi, na kulazimisha serikali kutangaza hali ya hatari nchini humo mwote. 
Ethiopia imekumbwa na maandamano ya miezi kadhaa ambapo waandamanaji wanashinikiza kupatikana kwa uhuru wa kisiasa na haki ya kumiliki ardhi, huku wakilaumu serikali kwa kuendeleza utawala wa kimabavu.
Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, watu 400 wamekufa nchini Ethiopia kutokana na maandamano hayo dhidi ya serikali. Hayo yamesemwa na makundi ya kutetea haki za kibinadamu pamoja na wanaharakati wa upinzani.

Jumatatu wiki hii, rais wa Ethiopia alitangaza bungeni kuwa sheria za uchaguzi zitafanyiwa marekebisho ili kuruhusu vyama vingi vya kisiasa na kuwapa nafasi wapinzani. Hata hivyo, matumizi ya mtandao yangali yamezimwa nchini humo, baada ya maandamano kuzidi kwa muda wa wiki moja ambapo pia waandamanaji walifanya uharibifu katika biashara na afisi za ubalozi wa nchi zinazofikiriwa kushirikiana na serikali.
Marekani na mataifa mengine yameitaka serikali ya Ethiopia kujizuia katika kukabiliana na waandamanaji huku maafisa wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wakitaka uchunguzi huru ufanywe kuhusu matukio hayo katika eneo la Oromia.
Merkel amekamilisha ziara yake ya siku tatu katika nchi za Mali, Niger na Ethiopia yenye lengo la kuhimiza uimarishaji wa usalama ili kupunguza wimbi la wakimbizi. Ethiopia ni mojawapo ya nchi inayowahifadhi wakimbizi wengi duniani. Mamia ya maelfu ya wakimbizi hao wakitoka Somalia, Sudan Kusini na kwingineko. Sawa na Ujerumani ambayo.
Merkel pia inakumbwa na mzigo wa wakimbizi kwa sasa, ambapo takriban wakimbizi mioni moja waliingia Ujerumani tangu mwaka jana pekee.pia amefungua rasmi jingo jipya la Muungano wa Afrika ambalo pia litakuwa la baraza la amani na usalama. Jengo hilo lililopo Addis Ababa limejengwa kwa ufadhili wa yuro milioni 27 kutoka Ujerumani.


Chanzo: DW

.

KANSELA MERKEL AZINDUA JUMBA LA MWALIMU NYERERE ADDIS ABABA


Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amezindua jumba jipya makao makuu ya Umoja wa Afrika ambalo limepewa jina la rais mwanzilishi wa taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere ambaye siku ya Oktoba 14, 2016 itakuwa kumbukumbuku ya kifo chake.
Jumba hilo ambalo jina lake kamili ni Jumba la Amani na Usalama la Julius Nyerere limejengwa kwa ufadhili kutoka Ujerumani.

Litakuwa makao ya idara ya Amani na Usalama ya AU na litatumiwa pia na maafisa wa kutoa tahadhari ya mapema kuhusu mizozo barani pamoja na kuratibu juhudi za kulinda amani za AU.
Ujenzi wa jumba hilo, ambalo ukubwa wake wa sakafu ni mita 13,500 mraba na linaweza kutumiwa na wafanyakazi 360, uligharimu euro 27 milioni.
Jumba hilo afisi za kufanyia kazi, vyumba vya mikutano vya kutumiwa na Baraza la Amani na Usalama, chumba cha kuratibia shughuli, maktaba na vyumba vya shughuli za pembeni.

Mwalimu Nyerere, ambaye alikuwa rais wa Tanzania hadi 1985, alikuwa mmoja wa viongozi waanzilishi wa Muungano wa Nchi za Afrika (OAU) ambao sasa ni Umoja wa Afrika (AU).
Alishiriki sana katika jitihada za kuendeleza bara la Afrika na kusaidia mataifa ambayo hayakuwa yamepata uhuru kujipatia uhuru wake.
Mwalimu Nyerere alipigania sana kumalizwa kwa ubabe wa Wazungu katika nchi za Rhodesia (sasa Zimbabwe), Afrika Kusini, na taifa la Kusini Magharibi mwa Afrika/Namibia (sasa Namibia).



Chanzo: BBC Swahili

JPM AWATAKA WATUMISHI KUREJESHA POSHO


Rais JPM amewataka Watumishi wa Umma walioalikwa katika kilele cha sherehe za Mwenge ambazo zitafanyika tarehe 14 Oktoba kutohudhuria na warudishe posho za safari walizolipwa. 
Viongozi waliotajwa kutakiwa kufuta safari zao za kwenda Bariadi ni pamoja na wakuu wote wa mikoa, wilaya, wakurugenzi wote wa  mamlaka za serikali za mitaa, mameya, na wenyeviti wote wa Halmashauri  za majiiji, manispaa, miji na wilaya pamoja na watumishi ambao huambatana nao wakiwemo madereva na wasaidizi wao ambao kwa idadi hufikia takribani 1,500.
Kwa kuwa sherehe za kilele cam bio za mwenge wa Uhuru huambatana na maandhimisho ya siku ya kumbukumbuku ya Baba wa Taifa, hayati, Mwalimu J.K  Nyerere aliyefariki miaka 17 iliyopita, agizo hilo limewataka viongozi wote wa mikoa na wilaya kubaki katika maeneo yao ya kazi na kujiwekea utaratibu wa jinsi ya kuienzi siku hiyo.

 Hii hapa ni “Press Release” ya taarifa hiyo.

Tuesday, 11 October 2016

KINDA WA MIAKA KUMI ALA MKATABA JUVE

Kinda Rasheed Al Hajjawi
Mabingwa hao wa Italia, Juventus wamemchukua “kinda”  mpalestina Rasheed Al Hajjawi mwenye miaka 10, baada ya kuzungumzwa sana kwenye “media: za kiarabu siku za karibuni.   Licha ya kukulia mjini Gaza, “kinda” huyo alizaliwa na kukulia Norway.

Habari za kunaswa kwa kinda huyo zimekuja baada ya “skauti ya kisasa” ya kunyaka matukio, habari na vipaji ya mtandao wa kijamii kupitia Youtube, huku wakibashiri kuwa ni Lionel Messi mpya. ndani ya wiki ya karibuni  siku ya Jumanne pia kumetokea dogo mwingine kwa jina la Karamoko Dembele mwenye miaka 13, aliyefanya "appearance"  kwa dakika 10 za mwisho kwenye mechi ya Celtic U20's katika ushindi wa goli 3-1 dhidi ya Hearts.

Dembele akiingia uwanjani 

DOGO SI WA MCHEZOMCHEZO
Kweli si wa mchezomchezo kabla ya kutua alishaibuka kwenye mazoezi ya klabu ya Liverpool, na pia kuwa karibu na mastaa wa Real Madrid.
Dogo Rasheed akiwa Liverpool

Kwenye mtandao wa “facebook”  dogo kazitundika picha za mastaa kadhaa aliopiga nao stori.

 
Dogo akiwa na kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane


Tuesday, 27 September 2016

BONGO KUAPISHWA LEO


Bwana Ali Bongo
Rais  wa  Gabon  Bwana  Ali  Bongo  Ondimba  anataraji  kuapishwa  leo usiku wa jumanne  kushika   hatamu  ya  uongozi  wa  nchi  hiyo  ya  Afrika  magharibi  kwa  muhula  wa  pili  baada  ya  kumshinda  mpinzani  wake  Bwana  Jean  Ping kufuatia  uamuzi  wa  mahakama  ya  kikatiba  nchini  humo  kutupilia  mbali  shauri  la  upinzani  la  kutaka  kura  zihesabiwe  upya  jumamosi  iliyopita.
Jumuiya  ya  kimataifa  imelaani uamuzi  huo  wa  mahakama  kwa  kushindwa  kufanya  kazi  kwa  uhuru  na  usawa  ambapo  akijibu  tuhuma  hizo  rais  wa  Gabon  Bwana  Ali  Bongo  Ondimba  alikuwa  na  machache  ya  kusema ‘’Jumuiya  ya  kimataifa  haikuja  kupiga  kura  hapa  bali  watu  wa  Gabon  ndio  waliofanya  hivyo  nami  nawajibika  kwa  ajili  yao’’

Taarifa  kutoka  ndani  ya  ofisi  ya  rais  nchini  humo  inadai  kuwa  hafla  ya  kuapishwa  kwa  Bwana  Ali  Bongo  itafanyika  jumanne  hii  mjini  Libreville  nchini  humo  lakini  haijaweka  wazi  ni  muda  gani  hasa  tukio  hilo  litafanyika.

KIZZA KUREJEA UGANDA

Bwana Kiiza Besigye
Kiongozi  wa  upinzani  nchini  Uganda  Bwana  Kizza  Besigye  anataraji  kurejea  nchini  humo  alhamisi   wiki  hii  akitokea  katika  nchi  za  Uingereza  na  Marekani  ambako  alikwenda kwa  ziara  ya  wiki  tatu  na  kueleza  hali  halisi  ya  kisiasa  nchini  Uganda  pamoja  na  harakati  zake  za  upinzani  dhidi  ya  serikali  ya  rais  Yoweri  Museveni  wa  nchi  hiyo. 
Chama  kikuu  cha  upinzani  nchini  humo  cha  Forum  Democratic  change (FDC)  kimewataka  wafuasi  wake  kujitokeza  kwa  wingi  siku  ya  alhamisi  wiki  hii  kumlaki  kiongozi  wao  Kizza  Besigye  ambaye  amekuwa  akikabiliana  na  kile  kinachotajwa  na  jumuiya  ya  kimataifa  kama  ukandamizaji  wa  demokarasia  nchini  Uganda  unaofanywa  na  serikali  inayoongozwa  na  Bwana  Yoweri  Kaguta  Museveni  ambapo  hivi  sasa  Bwana  Kizza  Besigye  anakabiliwa  na  kesi  ya  uhaini  kufuatia kujitangaza  mshindi  katika  uchaguzi  wa  rais  nchini  humo  Februari  mwaka  huu  kisha  kujiapisha  mwenyewe  kama    rais  wa  Uganda.

Jeshi  la  polisi  la  Uganda  kupitia  msemaji wake Bwana   Andrew Kawesi limekanusha  kuwepo  kwa  maandamano  ya  kumpokea  kiongozi  huyo  wa  upinzani  ambapo  msemaji  huyo  wa  polisi  amesema  hawajatoa  kibali  cha  maandamano  hayo.