Tuesday 20 September 2016

MLIPUKO MFULULIZO MAREKANI HUENDA IKAWA NA SURA YA UGAIDI

Wakati wachunguzi wa shirika la kijasusi la Marekani  FBI, mjini New York wakifuatilia ushahidi  ili kubaini   chanzo  cha  bomu lililolipuka katika eneo la Chelsea huko Manhattan siku ya Jumamosi usiku na kifaa cha pili ambacho hakikulipuka kilichopatikana eneo hilo, shirika hilo  la FBI pia  limesema linachunguza bomu lingine lililopuka katika jimbo la New Jersey saa chache kabla yakutaka kuongea na waandishi wa habari.
Agenti maalum wa FBI, Richard Thornton.
Mlipuko huo ambao ulitokea saa chache kabla ya "agenti" maalum wa FBI kuhusu tukio hilo, Richard Thornton kuzungumza na waandishi wa habari, alidai “kwa sasa tunafanya uchunguzi wa awali kama ni gaidi, nasema uchunguzi wa awali kwasababu kuna vitu vingi hatufahamu, hatufahamu kama shambulio hili linahusisha kikundi gani cha ugaidi, hivyo ndivyo uchunguzi ulipofikia”

Katika tukio hilo lilotokea eneo la Chelsea watu 29 wamejeruhiwa na tayari watu hao wameruhusiwa kuondoka hospitalini baada ya matiba huku maofisa hao wa FBI wakisema kuwa wanachunguza madai ya kundi la Islamic State yakuwa mtu mmoja aliekuwa amevalia mavazi ya kiaskari mwenye asili ya Somalia na kuendesha shambulizi kwa kutumia kisu na kuwajeruhi watu nane ndani ya duka la Crossroads Center mall, jimbo la Minnesota nchini marekani siku ya hiyo hiyo ya Jumamosi ni mfuasi wao.


TOURE KUSTAAFU TIMU YA TAIFA KWA MALUMBANO YA WAKALA WAKE NA PEP

Yaya Toure
Itakuwa sio stori nzuri kwa kiungo wa Man city na timu ya taifa ya Cote d'Ivore, mkongwe Yaya Toure kustaafu kuitumikia timu yake ya taifa na zawadi ya kukaa "benchi" ya maneno isiyo ya "kifundi" toka kwa meneja wake Pep Gurdiola.
Toure mwenye miaka 33 ametoa tamko leo nakusema "Ni maamuzi magumu kuyachukua ila waache wachezaji wengine wapate nafasi, nawashakuru kwa sapoti mliyotoa mashabiki wangu".
Huku anatangaza kustaafu balaa ni kuwa kocha wake wa Man city, Pep Guardiola kaeleza kuwa hatocheza mechi yoyote mpaka aombe msamaha kutokana na kauli za wakala wake.
Wakala wa Toure, Dimitri Seluk zaidi ya wiki moja iliyopita alidai "Kama atachukua taji la Ligi ya Mabingwa msimu huu, basi nitasafiri mpaka England na nitasema mbele ya luninga kwamba Pep Guardiola ni meneja bora kabisa duniani,” Seluk alinukuliwa na gazeti la Sunday Mirror.
Wakala huyo alizidi kung'aka kuwa ni wakati sahihi kwa mchezaji huyo kung’oa nanga kwenye kikosi hicho kwenye dirisha la usajili mwezi wa kwanza, pia ni ukandamizaji uliokikuka misingi kwa mteja wake kuwekwa nje hasa akiwa ni mchezaji aliyeibeba vilivyo Man City. 
Sasa joto ya jiwe ipo kwa wakala wa Toure kujibu nakusema "si anataka (Pep) vita, atavipata...........anatakiwa amwombe msamaha Joe Hart, hawezi kumtoa mchezaji mwenye heahima yake England".
wakala wa Toure, Seluk(kushoto) na Yaya Toure

Dimitri ameyajibu hayomuda usiopungua masaa mawili mpaka matatu nakukazia zaidi yeye(Pep) ndio aombe msamaha kwa Toure kumuweka kwa benchi.
Toure aliyekuwemo kwenye kikosi cha "tembo" kilichochukua kombe la mataifa Afrika mwaka 2015, amelichezea taifa hilo mechi 102 na kufunga magoli 19.
Toure anastaafu baada ya kutumika kwa miaka 14.

TRUMP: KUMPA MATIBABU YA KISIASA GAIDI NI UDHAIFU KWA SERIKALI

Mgombea wa Democratic, Donald Trump
Akizungumza   mjini   Fort Myers  katika  jimbo  la  Florida  nchini  Marekani  Bwana  Donald Trump  amesema  kuwa   hatua  ya  serikali  ya  nchi  hiyo  inayoongozwa  na chama  cha  Democratic  kumpatia  matibabu  ya  kisasa  mshukiwa  wa  ugaidi  ni  ishara  ya  dhahiri   kuwa  kuna  udhaifu  mkubwa  ndani  ya  idara  ya  usalama  wa  taifa  ya  nchi  hiyo,  Bwana  Trump  alisema ‘’Sasa  tumemfanyia  ukarimu   wa  ajabu  sana,  ametibiwa  na  miongoni  mwa  madaktari  bora  duniani,  amepelekwa  kwenye  hospitali  ya  kisasa  na  amepewa  chumba  cha  kisasa  hospitalini  hapo  na  huenda  atapokea  huduma  zote  akiwa  humo,  ukizingatia  jinsi nchi  hii  ilivyo’’. Bwana  Ahmad  Khan  Rahami  wenye  umri  wa  miaka  28  ambaye  ni  mzaliwa  wa  Afghanistan  anatuhumiwa  kufanya  mashambulizi  ya  kigaidi  katika  miji  ya  New  York  na  New  Jersey  nchini  Marekani  jumamosi  iliyopita  ambapo  tayari  amefunguliwa  mashtaka  matano  ya  kujaribu  kutekeleza  mauaji.
Mshukiwa wa mlipuko miwili mfufulizo New York na New Jersey, Ahmad Rahmani Khan
Mgombea  urais  wa  Republican  nchini  Marekani  Bwana  Donald  Trump  ameelezea  masikitiko  yake  kuhusu  namna  serikali  ya  nchi  hiyo  ilivyomkarimu  mshukiwa  wa  vitendo  vya  kigaidi   katika  jiji  la  New  York  jumamosi  iliyopita   Bwana Ahmad Khan Rahami  ambapo  maofisa  wa  serikali  wanadaiwa  kumpatia  matibabu  mshukiwa  huyo  na  kisha  kumpatia  wakili  atakayemtetea  wakati  atakapopandishwa  kizimbani  kwa  tuhuma  za  ugaidi.

HALI YA KISIASA NCHINI KONGO IMO HATARINI

Watu  takribani  50  wamefariki  dunia  nchini  Jamhuri  ya  Kidemokrasia  ya  Congo  kufuatia  makabiliano  kati  ya  waandamanaji  na  polisi  katika  miji  mbalimbali  nchini  humo  yaliyoanza  jumatatu  wiki  hii  baada  ya  tume  ya   taifa  ya  uchaguzi  nchini  humo  kutangaza  kuahirisha  uchaguzi  wa  rais  hadi  mwaka  2017  kinyume  na  katiba   ya  nchi  hiyo.
Waziri   wa  mambo  ya  ndani  wa  Jamhuri  ya  Kidemokrasia  ya  Congo  Bwana  Evariste  Boshab  amesema  miongoni  mwa  watu  waliofariki  katika  maandamano  hayo  wamo  maofisa  kadhaa  wa   polisi  ambao  Waziri  huyo  wa  serikali  amesema  kuwa  baadhi    ya  maofisa  hao  wa  polisi waliuawa kwa  kuchomwa  moto  wangali  hai   na  waandamanaji  wanaomshinikiza  rais  wa  nchi  hiyo  Bwana  Joseph  Kabila  kuondoka  madarakani.
Aidha  kwa  upande  wake  mmoja  kati  ya  viongozi  wa  upinzani  nchini  humo  Bwana   Rene  Rughunda  alidai  ‘’Watu  wa  nchi  hii  wapo  tayari  kupambana  na  kurejesha  thamani  ya  demokrasia  ndani  ya  nchi  hii,  ikiwa  Bwana  Kabila  hataachia  madaraka  sisi  kama  watu  wa  nchi  hii  tutamlazimisha  kuachia  madaraka’’.
Miili  ya  watu  waliofariki  katika  maandamano  hayo  imeonekana  ikizagaa  barabarani  katika  mji  mkuu wa  nchi  hiyo  Kinshasa  ambapo  waandamanaji  wamechoma  moto  magari  ya  polisi  na  kuweka  vizuizi  barabarani. Upinzani  umepanga  kuendelea  na  maandano  zaidi  wiki  hii  ili  kuishinikiza  tume  ya  uchaguzi  ya  nchi  hiyo  kuratibu  tena  uchaguzi  wa  rais  nchini  humo  mwishoni  mwa  mwaka  huu  wa  2016  kwa  mujibu  wa  katiba  ya  nchi  hiyo.

COURTOIS: NATAMANI KURUDI MADRID



Inawezekana kuwa ni stori kutovutiwa  na   wapenzi  na mashabiki wa Chelsea baada ya  golikipa wao mbelgiji Thibaut Courtois kuonyesha kuvutiwa na maisha ya Madrid hivyo kuonyesha moja kwa moja hafurahii 'life' la Stamford Bridge. Courtois alipiga “stori” na gazeti la Marca, la huko Uhispaniola nalo limevujisha nia ya “goalie” huyo kurejea La Liga mchezaji alietengeneza jina  vyema Atletico Madrid kabla ya kutua Chelsea, amefunguka kuwa Madrid ni kama nyumbani hivyo ana hamu ya kuwepo mara nyingine.
Kwenye 'interview' na gazeti hilo alisema “Atletico ni klabu ya kifamilia, bado nawapenda”.
Alipohojiwa kuwa anataka kurudi Uhispaniola alidai “Ndio, kwasababu ya klabu hiyo(Atletico), na jinsi mji wa Madrid ulivyo na nchi nzima”



“Tokea mara ya kwanza nilipapenda Uhispaniola kwasababu ya watu wake, mtindo wa maisha,chakula…...bado “namaintain’ ulaji wao wa chakula, hata luninga zao nafuatilia……mimi ni nusu mhisipaniola’.
Kuhusu ratiba ya kurejea La Liga alisema “nina kandarasi ya misimu mitatu na Chelsea.  Mwaka 2008, mwaka wa mwisho wa kandarasi, nitapima kubaki au kuondoka”



RASHFORD KUWA KINDA ANAYELIPWA ZAIDI DUNIANI

Man United bado wanauguza vidonda vya kufugwa   3-1“wikendi” hii na Watford ila kuna kijana mdogo wa kujivunia ukiacha mastaa waliopo kikosini aliyefunga goli la pekee la United, ni kinda Marcus Rashford.
United wanatarajiwa “kuset” rekodi ya kandarasi nono ya pauni 50,000 kwa wiki mpaka 2020 pale  kandarasi yake ya sasa itakapokwisha ili kumfunga kuogopa “wanyemeleji”.
Hivyo, kijana mdogo tu mwenye miaka 18 anayetimiza miaka 19 mwezi ujao  anatarajia kuvunja rekodi ya dunia kuwa mchezaji  mdogo anayelipwa zaidi duniani kumfikia mreno  Renato Sanchez wa Byern Munchen. Alipewa kandarasi ya mwaka ya pauni milioni moja mwezi Mei baada ya kudumbukia kwenye soka la wakubwa mwezi wa pili na mpaka sasa amekuwa mfungaji mzuri toka mechi ya Europa alipofunga mara mbili dhidi ya FC Midtjylland na  alipokuwa na bosi Loius Van Gaal mpaka sasa akiwa bosi  mreno Jose Mourinho, hajageuka nyuma japo anatokea benchi kwa "aapearance"   gemu kadhaa.

PENZI JIPYA LA RONALDO HADHARANI


Winga  wa Madrid mwenye manjonjo yake Christiano Ronaldo anahusishwa na “stori” mpya yakuwa “penzini” na mrembo Desire Cordero, ambaye ashawahi kuvikwa taji la Miss Spain siku za nyuma.
Hilo limeripotiwa na gazeti la udaku la uhispania la Corazon Czn katika toleo lao jipya.
Wawili hao wameripotiwa kuwa pamoja sasa yapata mwezi mmoja na mrembo huyo kuhusishwa tayari kashaingia mjini Madrid kufanya “makazi” yake.
Hili ndilo gazeti la "Corazon Cznlililoripoti kwa kichwa kikisema "LA PAREJA SORPRESA DEL ANO" kwa tafsiri isiyo rasmi ikimaanisha "SUPRISE, WAPENZI WAPYA" na mstari wa chini "LLEVEN VIENDOSE UN MES"- "YAPATA MWEZI  SASA"    


Monday 19 September 2016

NANGAA: UCHAGUZI MKUU CONGO HADI MWAKANI

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila.
Pamoja na mkutano  wa  upatanishi ulioongozwa  na  aliyekuwa  mwenyekiti  wa  umoja  wa  Afrika  Bwana  Edem  Kodjo  uliofanyika  nchini  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwanzoni  mwa  mwezi  Septemba  mwaka  huu  kati ya wapinzani na serikali ya nchi hiyo inayoongozwa na Rais Joseph Kabila.  Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri  ya  Kidemokirasia  ya  Kongo   imesisitiza   kuwa  hakuna  uwezekano  wa  uchaguzi  kufanyika  nchini  humo  mwaka  huu  kama ilivyoelezwa kwenye katiba  ya  nchi  hiyo.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya nchi hiyo ambayo ilitarajiwa kuanza mchakato wake wa kufanyika kwa uchaguzi kuanza jumatatu ya wiki hii, Bwana Corneille Nangaa amesema suala hilo kwa sasa haliwezekani na badala yake anashauri uchaguzi ufanyike mwaka ujao.




Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, Corneille Nangaa.
Kufuatia  tamko  hilo  hali  si  shwari  ndani  ya  miji  mikubwa  ya  Jamhuri  ya  Kidemokrasia  ya  Kongo  ambapo  makundi  ya  upinzani  yamefanya  mkaandamano  makubwa  katika  miji  ya  nchi  hiyo  ikiwemo  Kinshasa  na  Kivu  pamoja  na  maeneo  mengine  ili  kuishinikiza  tume  ya  uchaguzi  ya  nchi  hiyo  itengue  uamuzi  huo  na  kuruhusu  uchaguzi  ufanyike  mwaka  huu  kwa  mujibu  wa  katiba

ICJ YAANZA KUISIKILIZA KESI YA MPAKA KATI YA KENYA NA SOMALIA

Mahakama  ya  Kimataifa  ya  Haki  (ICJ)  inayoungwa  mkono  na  Umoja  wa  Mataifa  imeanza  kusikiliza  kesi  ya  kugombea  mpaka  kati  ya  nchi  za  Kenya  na  Somalia  mjini  The  Hague  nchini  Uholanzi, ambapo  mwanasheria  mkuu  wa  Kenya  Profesa  Githu  Muigai  amesema  ataongoza  jopo  la  mawakili  na  maofisa  wa  ngazi  za  juu  kutoka  nchini    Kenya   ili  kuitetea  nchi  hiyo.
Mwanasheria Mkuu wa Kenya, Profesa Githu Muigai.
 Aidha  mwanasheria  huyo  wa  Kenya  amesema  kuwa  Kenya  inataraji kuituhumu Somalia  katika  kesi  hiyo  kwa  kuvunja  mkataba  wa  mwaka  2009  ambapo  amesema nchi  hizo  zilikubaliana  kutatua  mzozo  huo  unaohusisha  sehemu  za  nchi  hizo  ndani  ya  Bahari  ya  Hindi  kupitia  mazungumzo.  Eneo  hilo  linalogombaniwa  lina  ukubwa  wa  kilomita  za  mraba  42,000  na  linasadikiwa  kuwa  na  utajiri  wa  mafuta  na  gesi.

Katika  mgogoro  huo  Somalia  inataka  mpaka  wake  wa  baharini  uendelee  kwa  kufuata  mstari  wa  mpaka  ulio  nchi  kavu  unaolekea  kusini  mashariki  mwa  nchi  hiyo  wakati  Kenya  nayo  ikitaka  mpaka  huo  uwekwe  kwa  kufuata  mstari  usiopinda  unaoelekea  mashariki,  hali  hiyo  imesababisha  kutengeneza  umbo  la  pembetatu  kutokana  na  madai  ya  nchi  hizo  mbili  za  Afrika  Mashariki. Kesi  hiyo inataraji  kudumu  kwa  wiki  moja  ili  kutoa  mwelekeo  wa  namna  nchi  hizo  zitavyofikia  maridhiano. 
Kesi hiyo iliwasilishwa ICJ tangu Agosti, 2014.




ETI KILICHOMTOKEA CASILLAS KWA MOURINHO KIPO NJIANI KWA ROONEY?

Casillas(kushoto) na Mourinho.
 Ishu ya kutoogopa  na kuwa  "uso wa mbuzi" kwa mastaa huyu huyu kocha  Jose Mourinho  inatazamiwa kwa jicho la ajabu na mashabiki wa Man U. Inaelekea kilichomkuta Iker Casillas kwa kupigwa chini japo na ukongwe na heshima yake Madrid na kocha mwenye “vituko” Jose Mourinho kinaweza kutokea kwa Wayne Rooney akiwa na kocha huyo  ndani ya United.
Mashabiki wa United wanahisi Rooney anaweza kupigwa benchi na mwishowe kuuzwa kama vile Juan Mata.
Mourinho(kushoto) na Rooney.


Huo umekuwa utabiri wa mashabiki wengi kwenye mtandao wa “twitter” baada ya United kufungwa na Watford huku kiungo na nahodha huyo  kutofanya “tackling” na kupiga shuti “on target” na zaidi kutohusishwa kwenye kikosi kwenye  mechi ya Europa  dhidi ya Feyenoord ya Uholanzi.

Gundu kwa staa huyo aliyeshindwa kuibeba United kwa mechi Man City na Watford kwa kufungwa ukiachilia ambayo hakwenda Uholanzi dhidi ya Feyenoord,  uwezekano wa kupigwa chini ni rahisi kutokana na mawazo ya mashabiki hawa;