Mahakama ya Kimataifa
ya Haki (ICJ) inayoungwa mkono na
Umoja wa Mataifa imeanza kusikiliza kesi
ya kugombea mpaka kati ya nchi za
Kenya na Somalia mjini The Hague
nchini Uholanzi, ambapo mwanasheria mkuu wa
Kenya Profesa Githu Muigai amesema
ataongoza jopo la mawakili na maofisa
wa ngazi za juu kutoka nchini
Kenya ili kuitetea nchi hiyo.
Mwanasheria Mkuu wa Kenya, Profesa Githu Muigai. |
Aidha mwanasheria huyo wa
Kenya amesema kuwa Kenya inataraji kuituhumu
Somalia katika kesi hiyo kwa kuvunja mkataba
wa mwaka 2009 ambapo amesema nchi hizo
zilikubaliana kutatua mzozo huo unaohusisha
sehemu za nchi hizo ndani ya Bahari
ya Hindi kupitia mazungumzo. Eneo hilo
linalogombaniwa lina ukubwa wa kilomita za
mraba 42,000 na linasadikiwa kuwa na
utajiri wa mafuta na gesi.
Katika mgogoro huo Somalia
inataka mpaka wake wa baharini uendelee
kwa kufuata mstari wa mpaka ulio nchi
kavu unaolekea kusini mashariki mwa nchi
hiyo wakati Kenya nayo ikitaka mpaka
huo uwekwe kwa kufuata mstari usiopinda
unaoelekea mashariki, hali hiyo imesababisha
kutengeneza umbo la pembetatu kutokana na
madai ya nchi hizo mbili za Afrika
Mashariki. Kesi hiyo inataraji kudumu kwa wiki
moja ili kutoa mwelekeo wa namna nchi
hizo zitavyofikia maridhiano.
Kesi hiyo iliwasilishwa ICJ tangu Agosti, 2014.
No comments:
Post a Comment