Watu takribani 50 wamefariki dunia nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufuatia makabiliano kati ya waandamanaji na polisi katika miji mbalimbali nchini humo yaliyoanza jumatatu wiki hii baada ya tume ya taifa ya uchaguzi nchini humo kutangaza kuahirisha uchaguzi wa rais hadi mwaka 2017 kinyume na katiba ya nchi hiyo.
Waziri wa mambo ya ndani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Bwana Evariste Boshab amesema miongoni mwa watu waliofariki katika maandamano hayo wamo maofisa kadhaa wa polisi ambao Waziri huyo wa serikali amesema kuwa baadhi ya maofisa hao wa polisi waliuawa kwa kuchomwa moto wangali hai na waandamanaji wanaomshinikiza rais wa nchi hiyo Bwana Joseph Kabila kuondoka madarakani.
Aidha kwa upande wake mmoja kati ya viongozi wa upinzani nchini humo Bwana Rene Rughunda alidai ‘’Watu wa nchi hii wapo tayari kupambana na kurejesha thamani ya demokrasia ndani ya nchi hii, ikiwa Bwana Kabila hataachia madaraka sisi kama watu wa nchi hii tutamlazimisha kuachia madaraka’’.
Miili ya watu waliofariki katika maandamano hayo imeonekana ikizagaa barabarani katika mji mkuu wa nchi hiyo Kinshasa ambapo waandamanaji wamechoma moto magari ya polisi na kuweka vizuizi barabarani. Upinzani umepanga kuendelea na maandano zaidi wiki hii ili kuishinikiza tume ya uchaguzi ya nchi hiyo kuratibu tena uchaguzi wa rais nchini humo mwishoni mwa mwaka huu wa 2016 kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo.

No comments:
Post a Comment