Wakati wachunguzi wa shirika la kijasusi
la Marekani FBI, mjini New York wakifuatilia ushahidi ili kubaini
chanzo cha bomu lililolipuka katika eneo la Chelsea
huko Manhattan siku ya Jumamosi usiku na kifaa cha pili ambacho hakikulipuka
kilichopatikana eneo hilo, shirika hilo la FBI pia limesema
linachunguza bomu lingine lililopuka katika jimbo la New Jersey saa chache
kabla yakutaka kuongea na waandishi wa habari.
Agenti maalum wa FBI, Richard Thornton. |
Mlipuko huo ambao ulitokea saa chache kabla ya
"agenti" maalum wa FBI kuhusu tukio hilo, Richard Thornton kuzungumza
na waandishi wa habari, alidai “kwa sasa tunafanya uchunguzi wa awali kama ni
gaidi, nasema uchunguzi wa awali kwasababu kuna vitu vingi hatufahamu,
hatufahamu kama shambulio hili linahusisha kikundi gani cha ugaidi, hivyo ndivyo
uchunguzi ulipofikia”
Katika tukio hilo lilotokea eneo la Chelsea watu 29
wamejeruhiwa na tayari watu hao wameruhusiwa kuondoka hospitalini baada ya
matiba huku maofisa hao wa FBI wakisema kuwa wanachunguza madai ya kundi la
Islamic State yakuwa mtu mmoja aliekuwa amevalia mavazi ya kiaskari mwenye
asili ya Somalia na kuendesha shambulizi kwa kutumia kisu na kuwajeruhi watu
nane ndani ya duka la Crossroads Center mall, jimbo la Minnesota nchini
marekani siku ya hiyo hiyo ya Jumamosi ni mfuasi wao.
No comments:
Post a Comment