Bwana Kiiza Besigye |
Kiongozi
wa upinzani nchini
Uganda Bwana Kizza Besigye anataraji kurejea
nchini humo alhamisi wiki
hii akitokea katika
nchi za Uingereza
na Marekani ambako
alikwenda kwa ziara ya
wiki tatu na
kueleza hali halisi
ya kisiasa nchini
Uganda pamoja na
harakati zake za
upinzani dhidi ya
serikali ya rais
Yoweri Museveni wa
nchi hiyo.
Chama
kikuu cha upinzani
nchini humo cha
Forum Democratic change (FDC) kimewataka wafuasi
wake kujitokeza kwa
wingi siku ya
alhamisi wiki hii
kumlaki kiongozi wao
Kizza Besigye ambaye
amekuwa akikabiliana na
kile kinachotajwa na
jumuiya ya kimataifa
kama ukandamizaji wa
demokarasia nchini Uganda
unaofanywa na serikali
inayoongozwa na Bwana
Yoweri Kaguta Museveni
ambapo hivi sasa
Bwana Kizza Besigye
anakabiliwa na kesi
ya uhaini kufuatia kujitangaza mshindi
katika uchaguzi wa
rais nchini humo
Februari mwaka huu kisha kujiapisha
mwenyewe kama rais wa Uganda.
Jeshi la polisi
la Uganda kupitia
msemaji wake Bwana Andrew Kawesi
limekanusha kuwepo kwa
maandamano ya kumpokea
kiongozi huyo wa
upinzani ambapo msemaji
huyo wa polisi
amesema hawajatoa kibali
cha maandamano hayo.
No comments:
Post a Comment