Wednesday 19 October 2016

Monday 17 October 2016

HII NI TAARIFA KUTOKA JKT KWA UTAPELI UNAENDESHWA KUTUMIA JINA LAO


VIDEO: RAIS JPM ADAI MASSABURI ALIKUWA NA WAKE WANNE AU WATANO

Rais JPM(kulia) akitoa neno kwenye ibada ya kumuaga Dk. Massaburi kwenye viwanja vya Karimjee
Mapema leo Okkoba 17 2016, ilikuwa ni shughuli ya kumuaga aliyekuwa meya wa jiiji la Dar Es Salaam Dk. Didas Masaburi(20101-2015) aliyefariki Oktoba 12, 2016.
  Sasa “stori” ni kuwa Rais John Magufuli  alitoa  bonge la “headline” wakati wa kutoa hotuba kwa wananchi baada ya msomaji wa wasifu wa Dk. Masaburi kutaja kuwa  marehemu ameacha mke mmoja, Rais Magufuli alipata nafasi ya kuzungumza na kusema anafahamu Dk. Masaburi alikuwa na wake wanne au watano na hata watoto anafahamu kuwa anao zaidi ya 20, aidha Rais Magufuli amewaomba watoto wa marehemu kushikamana na kuwa wamoja.
Kuangalia video hii bonyeza hapa


 Chanzo: Millardayo

VIDEO: MSANII KOFFI OLOMIDE AWAOMBA RADHI WAKENYA


Mwanamuziki wa Congo, Koffi Olomide ambaye Julai mwaka huu aliwasili  Nairobi Kenya  kwa ajili ya shoo na baadae kuripotiwa kukamatwa kwa tuhuma za kumshambulia “dancer” wake wa kike ni baada ya kusambaa kwa video iliyomuonyesha akifanya kitendo hicho. Baada ya kupita miezi kadhaa tangu kutokea kwa tukio hilo na Koffi Olomide kutowahi kujitokeza hadharani kulizungumzia, amejitokeza kupitia kipindi cha TV cha Churchill Show, baada ya kupita miezi mitatu amewaomba msamaha wakenya na mashabiki wake kwa ujumla n kunukuliwa akisema

’Kupitia Churchill show, nataka kusema na nyinyi na kutuma ujumbe wa upendo, heshima na urafiki, mimi nasikitika kwa kile kilichotokea na maombi yangu nisamehewe kwa kile kilichotokea, mimi ni mwanadamu tu licha kwa kuwa ni maarufu’:- Koffi Olomide



Sunday 16 October 2016

NGOMA MPYA: RAYVANNY & NEYLEE- RUDI

Kitu kipya kwa mashabiki kinaitwa Rudi toka kwa  Rayvanny na Neylee
Kudownload Bonyeza hapa

UCHAGUZI MAREKANI: TRUMP ATAKA CLINTON "AFANYIWE UKAGUZI WA DAWA"


Mgombea wa Republican, Bw. Donald Trump
Mgombea kiti cha Urais kwa tiketi ya chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump, amemshutumu mpinzani wake Bi Hillary Clinton kwa kutumia aina fulani ya dawa, wakati wa mjadala wao uliopita wa moja kwa moja wa runinga.

Anasema kuwa alikuwa na haiba mwanzo mwanzo wa mjadala huo.
Sasa anapendekeza kuwa wafanyiwe majaribio ya matumizi ya dawa, kabla ya kufanyika kwa mjadala wao wa mwisho hapo siku ya Jumatano ya wiki hii.
Katika mkutano wake wa hivi punde uliofanyika New Hampshire, Bwana Trump kwa mara nyingine, amedai kuwa kuna njama za kumuibia kura.
Timu ya kampeini ya Bi Clinton, imesema kwamba wapigaji kura, sasa wameona bayana kile anachokiita juhudi za aibu za Bwana Trump za kutaka kuhujumu shughuli za upigaji kura.
Trump, anazidi kudidimia katika majimbo mengi, huku akikabiliwa na madai ya udhalilishaji wanawake kingono.


Chanzo: BBC Swahili

MAGAZETI YA LEO HAYA HAPA UNAWEZA UKAYAPITIA

Front Pages za Magazeti ya leo Oktoba 16, 2016 yapo tayari hapa.


SHIRIKA LA NDEGE LA LA KENYE LAAHIRISHA SAFARI KISA WAFANYAKAZI HAWAJATOKEA KAZINI



Shirika la ndege la Kenya Airways limeahirisha safari zake tano za kwenda ndani na nje ya nchi leo October 16 2016 kutokana na upungufu wa Wahudumu wa ndege kazini.
Taarifa inasema sababu hasa ya kuahirisha safari hizo tano za MombasaKilimanjaro,JubaMaputoHarare na Lusaka ni kutofika kazini kwa Wahudumu wa ndege ambao wamepangiwa zamu kwa wakati huo.
Imeelezwa kuwa baadhi ya Wafanyakazi wa shirika hilo hawajaripoti kazini toka Ijumaa iliyopita ambapo shirika linaendelea kufatilia kujua chanzo ni nini na jinsi ya kutatua tatizo na Mwajiri.
Kwa utaratibu ndege za abiria huwa na masharti yake kwenye kila safari ikiwa ni pamoja na kuwa na namba flani ya idadi ya Wahudumu ndani ya ndege ambayo ni lazima itimie, sasa kutokana na Wahudumu wa Kenya Airways kuwa wachache imebidi ndege nyingine zisisafiri.

Chanzo: Millardayo



DIAMOND, HARMONIZE NA DJ DOMMY WACHUKUA TUZO ZA AFRIMMA 2016

Watanzania Diamond, Harmonize na dj Dommy wameshinda tuzo Afrimma(African Music Magazine Awards) 2016 ambapo mwanamuziki Diamond ameshinda tuzo hiyo katika kipengele cha msanii bora wa kiume kwa upande wa Afrika Mashariki.  Vilevile Harmonize ambaye amesainiwa WCB nae ameshinda tuzo ya msanii bora chipukizi barani Afrika. Kwa upande wa Dj dommy  ameshinda tuzo ya Dj bora Afrika. Mdada  Akothee kutoka Kenya ameshinda tuzo ya msanii mora wa mike  Afrika Mashariki. SautiSol kutoka Kenya wameshinda tuzo ya Kundi Bora Afrika. Kwa upande wa Afrika Magharibi mwanadada Efya wa Ghana ameshinda kipengele cha msanii bora wa kike Afrika Magharibi alichokuwa akishindana na wakali kama  Yemi Alade(Nigeria) na Tiwa Savage(Nigeria).

LIST NZIMA YA WASHINDI WA AFRIMMA 2016 HII HAPA:
Best Male West Africa  Olamide (Nigeria)
Best Female West Africa  Efya
Best Male North Africa – Amr Diab
Best Female North Africa – Ibtissam
Best African DJ USA – Dj Dee Money
Best Male Central Africa – C4 Pedro
AFRIMMA Video of the year – Brother brother Bisa Kdei
Best Female Central Africa – Daphne
Music Producer of the year – Masterkraft
Best male South Africa  AKA
Best African Dancer – Brenda Derry ( Cameroon)
Best Female Southern Africa  Chikune
Best Rap Act – Phyno (Nigeria)
Best African Group – Sauti Sol (Kenya)
Best collaboration – Reggae blues ( Harrysong, Kcee) Nigeria
Crossing boundaries with Music – Wizkid (Nigeria)
Song of the year – Tecno Duro (Nigeria)
Best Gospel Act – Willy Paul (Kenya)
Best Male East Africa – Diamond Platnumz ( Tanzania)
Artist of the year – Flavour ( Nigeria)
Best Newcomer – Harmonize (Tanzania)
Best Dancehall Act – Shatta Wale
Best Video Director – Patrick Elis
Carribean Artist of the year – Machel Montano.