Showing posts with label SIASA. Show all posts
Showing posts with label SIASA. Show all posts

Wednesday, 12 October 2016

ETHIOPIA KUFANYA MAGEUZI MFUMO WA UCHAGUZI


Kansela Merkel akikamilisha ziara yake Afrika ameahidi kutoa mafunzo kwa maafisa wa polisi wa Ethiopia kuhusu namna ya kukabiliana na waandamanaji. Ametaka waandamanaji wapewe uhuru wa kuandamana na uhuru kwa wapinzani.
Waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn amesema serikali yake inataka kufanya mageuzi ya mfumo wa uchaguzi, ambao kwa muda mrefu umeutenga upinzani na kuchangia kutokea kwa maandamano mabaya ambayo yamedumu kwa miezi kadhaa. Haya yanajiri wakati Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akimaliza ziara yake nchini humo ambapo amesema waandamanaji waruhusiwe kuandamana.
Waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn amewaambia wanahabari kuwa “kufuatia mfumo uliopo sasa wa uchaguzi nchini humo, asilimia 51 ya kura inatosha kutwaa ushindi wa viti vyote". Na sasa serikali yake inataka kufanya marekebisho ili kuhakikisha mfumo huo unabadilishwa ili watu wote wakiwemo wapinzani wawakilishwe bungeni.

Chini ya mfumo uliopo sasa, muungano wa Hailemariam ambao ndio unatawala, ulishinda viti vyote 546 vya ubunge katika uchaguzi mkuu, uliofanywa mwaka jana. Hii hapa kauli ya Hailemariam kuhusu suala, la demokrasia na usalama nchini mwake."Ethiopia imejitolea kukuza demokrasia.Ethiopia imejitolea kuwa na demokrasia ya vyama vingi kulingana na katiba yetu. na Ethiopia imejitolea kuhakikisha haki za binadamu zinalindwa. Lakini Ethiopia pia inapinga ghasia ya misimamo mikali au makundi yanayojihami kwa fujo".
Hailemariam aliyasema hayo baada ya kukutana na mgeni wake Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, akimaliza ziara yake ya siku tatu barani Afrika, ambapo amesema demokrasia iliyoimarika inahitaji kuwepo na upinzani pamoja na uhuru wa vyombo vya habari. Ameitaka Ethiopia kuwapa uhuru waandamanaji bila ya ukandamizaji wa aina yoyote. Kando na kuhimiza serikali kufanya mazungumzo na upinzani, Merkel pia ameahidi kuwa, nchi yake itatoa mafunzo kwa maafisa wa polisi wa Ethiopia kuhusu namna ya kukabiliana na waandamanaji.

Akiwa Ethiopia, Kansela Merkel amemwambia mwenyeji wake Waziri Mkuu Desalegn kuwa waandamanaji waruhusiwe kuandamana na kuwa hatua yoyote ya vyombo vya usalama iwe kulingana na sheria. Kadhalika amesema wanaharakati wa upinzani na watetezi wa haki za kibinadamu wanapaswa kuwa na uhuru wa kutekeleza majukumu yao. Lakini Waziri Mkuu Hailemariam amepinga madai kuwa maafisa wa polisi walitumia mbinu za fujo dhidi ya waandamanaji, na kuahidi kuwa serikali yake itachunguza visa hivyo.
Wiki iliyopita, zaidi ya watu 50 waliuawa kwenye mkanyagano baada ya polisi kujaribu kuwatawanya waandamanaji. Hali iliyosababisha kuongezeka kwa maandamano zaidi, na kulazimisha serikali kutangaza hali ya hatari nchini humo mwote. 
Ethiopia imekumbwa na maandamano ya miezi kadhaa ambapo waandamanaji wanashinikiza kupatikana kwa uhuru wa kisiasa na haki ya kumiliki ardhi, huku wakilaumu serikali kwa kuendeleza utawala wa kimabavu.
Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, watu 400 wamekufa nchini Ethiopia kutokana na maandamano hayo dhidi ya serikali. Hayo yamesemwa na makundi ya kutetea haki za kibinadamu pamoja na wanaharakati wa upinzani.

Jumatatu wiki hii, rais wa Ethiopia alitangaza bungeni kuwa sheria za uchaguzi zitafanyiwa marekebisho ili kuruhusu vyama vingi vya kisiasa na kuwapa nafasi wapinzani. Hata hivyo, matumizi ya mtandao yangali yamezimwa nchini humo, baada ya maandamano kuzidi kwa muda wa wiki moja ambapo pia waandamanaji walifanya uharibifu katika biashara na afisi za ubalozi wa nchi zinazofikiriwa kushirikiana na serikali.
Marekani na mataifa mengine yameitaka serikali ya Ethiopia kujizuia katika kukabiliana na waandamanaji huku maafisa wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wakitaka uchunguzi huru ufanywe kuhusu matukio hayo katika eneo la Oromia.
Merkel amekamilisha ziara yake ya siku tatu katika nchi za Mali, Niger na Ethiopia yenye lengo la kuhimiza uimarishaji wa usalama ili kupunguza wimbi la wakimbizi. Ethiopia ni mojawapo ya nchi inayowahifadhi wakimbizi wengi duniani. Mamia ya maelfu ya wakimbizi hao wakitoka Somalia, Sudan Kusini na kwingineko. Sawa na Ujerumani ambayo.
Merkel pia inakumbwa na mzigo wa wakimbizi kwa sasa, ambapo takriban wakimbizi mioni moja waliingia Ujerumani tangu mwaka jana pekee.pia amefungua rasmi jingo jipya la Muungano wa Afrika ambalo pia litakuwa la baraza la amani na usalama. Jengo hilo lililopo Addis Ababa limejengwa kwa ufadhili wa yuro milioni 27 kutoka Ujerumani.


Chanzo: DW

.

Tuesday, 27 September 2016

BONGO KUAPISHWA LEO


Bwana Ali Bongo
Rais  wa  Gabon  Bwana  Ali  Bongo  Ondimba  anataraji  kuapishwa  leo usiku wa jumanne  kushika   hatamu  ya  uongozi  wa  nchi  hiyo  ya  Afrika  magharibi  kwa  muhula  wa  pili  baada  ya  kumshinda  mpinzani  wake  Bwana  Jean  Ping kufuatia  uamuzi  wa  mahakama  ya  kikatiba  nchini  humo  kutupilia  mbali  shauri  la  upinzani  la  kutaka  kura  zihesabiwe  upya  jumamosi  iliyopita.
Jumuiya  ya  kimataifa  imelaani uamuzi  huo  wa  mahakama  kwa  kushindwa  kufanya  kazi  kwa  uhuru  na  usawa  ambapo  akijibu  tuhuma  hizo  rais  wa  Gabon  Bwana  Ali  Bongo  Ondimba  alikuwa  na  machache  ya  kusema ‘’Jumuiya  ya  kimataifa  haikuja  kupiga  kura  hapa  bali  watu  wa  Gabon  ndio  waliofanya  hivyo  nami  nawajibika  kwa  ajili  yao’’

Taarifa  kutoka  ndani  ya  ofisi  ya  rais  nchini  humo  inadai  kuwa  hafla  ya  kuapishwa  kwa  Bwana  Ali  Bongo  itafanyika  jumanne  hii  mjini  Libreville  nchini  humo  lakini  haijaweka  wazi  ni  muda  gani  hasa  tukio  hilo  litafanyika.

KIZZA KUREJEA UGANDA

Bwana Kiiza Besigye
Kiongozi  wa  upinzani  nchini  Uganda  Bwana  Kizza  Besigye  anataraji  kurejea  nchini  humo  alhamisi   wiki  hii  akitokea  katika  nchi  za  Uingereza  na  Marekani  ambako  alikwenda kwa  ziara  ya  wiki  tatu  na  kueleza  hali  halisi  ya  kisiasa  nchini  Uganda  pamoja  na  harakati  zake  za  upinzani  dhidi  ya  serikali  ya  rais  Yoweri  Museveni  wa  nchi  hiyo. 
Chama  kikuu  cha  upinzani  nchini  humo  cha  Forum  Democratic  change (FDC)  kimewataka  wafuasi  wake  kujitokeza  kwa  wingi  siku  ya  alhamisi  wiki  hii  kumlaki  kiongozi  wao  Kizza  Besigye  ambaye  amekuwa  akikabiliana  na  kile  kinachotajwa  na  jumuiya  ya  kimataifa  kama  ukandamizaji  wa  demokarasia  nchini  Uganda  unaofanywa  na  serikali  inayoongozwa  na  Bwana  Yoweri  Kaguta  Museveni  ambapo  hivi  sasa  Bwana  Kizza  Besigye  anakabiliwa  na  kesi  ya  uhaini  kufuatia kujitangaza  mshindi  katika  uchaguzi  wa  rais  nchini  humo  Februari  mwaka  huu  kisha  kujiapisha  mwenyewe  kama    rais  wa  Uganda.

Jeshi  la  polisi  la  Uganda  kupitia  msemaji wake Bwana   Andrew Kawesi limekanusha  kuwepo  kwa  maandamano  ya  kumpokea  kiongozi  huyo  wa  upinzani  ambapo  msemaji  huyo  wa  polisi  amesema  hawajatoa  kibali  cha  maandamano  hayo.

TRUMP AWAKUMBUKA "WATU WEUSI" KWENYE MDAHALO

Bwana Trump(kushoto) akimsalimu Bi. Hillary mapema leo
Wagombea  urais  wa  marekani, Bi  Hillary  Clinton  wa  chama  cha  Democratics  na  Bwana  Donald  Trump  wa  Republican  wamechuana  vikali  katika  mdahalo  uliofanyika  mjini  New  York  nchini  humo  usiku  wa  kuamkia  jumanne  ambapo  katika  mdahalo  huo  masuala  ya  sera  za  ulipaji  kodi,  ajira  na  uchumi  yamechukua  nafasi  kubwa  huku  wagombea   hao  wakitupiana  maswali  ya  hapa  na  pale.
Akiongea  kwa  bashasha  na  tabasamu  Bi  Hilary  Clinton  wa  Democratic  alimtaka  Bwana  Donald  Trump  kuweka  wazi  taarifa  zake  za  ulipaji  kodi  ili  kuwathibitishia  wamarekani  kuwa  atachangia  kuinua  uchumi  wa  taifa  hilo  na  kuwalipa  vizuri  watumishi  wa  umma,  mambo  yalikuwa  hivi, ’Tupo  na  Bwana  Trump  jukwaani  jioni  ya  leo  tukijadili  mambo  yanayolikumba  taifa  letu, ninyi  mnapaswa  kutupima  kwamba  ni  nani  kati  yetu  anafaa  kuwa  rais  wa  Marekani  lakini  naamini  mimi nitashinda kwa  kura  yako  Novemba  nane’’
Kwa  upande  wake  mgombea  wa  chama  cha  Republican  Bwana  Donald  Trump  amemjibu  Bi  Hillrary  Clinton  wa  Democratic  kwa  kumtaka  aweke  wazi  jumbe  za   barua  pepe  zaidi  ya  33,000  za  serikali  alizozitumia  kupitia  anuani  yake  binafsi wakati  mwanamama  huyo  akiwa  waziri  wa  mambo  ya  nchi  za  nje  wa  Marekani  na  hapa  Bwana  Trump  anasema “Tunahitaji  kuboresha  uhusiano  mzuri  ndani  ya  jamii  nchini  hapa,  ninasema  uhusiano  mzuri  nikiwa  na  maana  kuwa  kumbukumbu  za  hivi  karibuni  zinathibisha  kudorora  kwa  uhusiano  kati  ya  polisi  na  raia  na  wanaoathirika  zaidi  ni  wamarekani  weusi  wenye  asili  ya  Afrika”.

Uchaguzi  wa  rais  nchini  marekani  unataraji  kufanyika  Novemba  8  mwaka  huu  2016  ambapo  hivi  sasa  kampeni  za  ushindani  kati  ya  wagombea  hao  wawili  zimepamba  moto  huku  kura  za  maoni  zikionyesha kuwa uungwaji  mkono  wa  Bwana  Donald  Trump  wa  Republican  na  ule  wa  Bi  Hillary  Clinton  wa  Democratic  umekaribiana  kwa  viwango  kikubwa.

KIZZA KUREJEA UGANDA

Bwana Kiiza Besigye
Kiongozi  wa  upinzani  nchini  Uganda  Bwana  Kizza  Besigye  anataraji  kurejea  nchini  humo  alhamisi   wiki  hii  akitokea  katika  nchi  za  Uingereza  na  Marekani  ambako  alikwenda kwa  ziara  ya  wiki  tatu  na  kueleza  hali  halisi  ya  kisiasa  nchini  Uganda  pamoja  na  harakati  zake  za  upinzani  dhidi  ya  serikali  ya  rais  Yoweri  Museveni  wa  nchi  hiyo. 
Chama  kikuu  cha  upinzani  nchini  humo  cha  Forum  Democratic  change (FDC)  kimewataka  wafuasi  wake  kujitokeza  kwa  wingi  siku  ya  alhamisi  wiki  hii  kumlaki  kiongozi  wao  Kizza  Besigye  ambaye  amekuwa  akikabiliana  na  kile  kinachotajwa  na  jumuiya  ya  kimataifa  kama  ukandamizaji  wa  demokarasia  nchini  Uganda  unaofanywa  na  serikali  inayoongozwa  na  Bwana  Yoweri  Kaguta  Museveni  ambapo  hivi  sasa  Bwana  Kizza  Besigye  anakabiliwa  na  kesi  ya  uhaini  kufuatia kujitangaza  mshindi  katika  uchaguzi  wa  rais  nchini  humo  Februari  mwaka  huu  kisha  kujiapisha  mwenyewe  kama    rais  wa  Uganda.

Jeshi  la  polisi  la  Uganda  kupitia  msemaji wake Bwana   Andrew Kawesi limekanusha  kuwepo  kwa  maandamano  ya  kumpokea  kiongozi  huyo  wa  upinzani  ambapo  msemaji  huyo  wa  polisi  amesema  hawajatoa  kibali  cha  maandamano  hayo.

Tuesday, 20 September 2016

TRUMP: KUMPA MATIBABU YA KISIASA GAIDI NI UDHAIFU KWA SERIKALI

Mgombea wa Democratic, Donald Trump
Akizungumza   mjini   Fort Myers  katika  jimbo  la  Florida  nchini  Marekani  Bwana  Donald Trump  amesema  kuwa   hatua  ya  serikali  ya  nchi  hiyo  inayoongozwa  na chama  cha  Democratic  kumpatia  matibabu  ya  kisasa  mshukiwa  wa  ugaidi  ni  ishara  ya  dhahiri   kuwa  kuna  udhaifu  mkubwa  ndani  ya  idara  ya  usalama  wa  taifa  ya  nchi  hiyo,  Bwana  Trump  alisema ‘’Sasa  tumemfanyia  ukarimu   wa  ajabu  sana,  ametibiwa  na  miongoni  mwa  madaktari  bora  duniani,  amepelekwa  kwenye  hospitali  ya  kisasa  na  amepewa  chumba  cha  kisasa  hospitalini  hapo  na  huenda  atapokea  huduma  zote  akiwa  humo,  ukizingatia  jinsi nchi  hii  ilivyo’’. Bwana  Ahmad  Khan  Rahami  wenye  umri  wa  miaka  28  ambaye  ni  mzaliwa  wa  Afghanistan  anatuhumiwa  kufanya  mashambulizi  ya  kigaidi  katika  miji  ya  New  York  na  New  Jersey  nchini  Marekani  jumamosi  iliyopita  ambapo  tayari  amefunguliwa  mashtaka  matano  ya  kujaribu  kutekeleza  mauaji.
Mshukiwa wa mlipuko miwili mfufulizo New York na New Jersey, Ahmad Rahmani Khan
Mgombea  urais  wa  Republican  nchini  Marekani  Bwana  Donald  Trump  ameelezea  masikitiko  yake  kuhusu  namna  serikali  ya  nchi  hiyo  ilivyomkarimu  mshukiwa  wa  vitendo  vya  kigaidi   katika  jiji  la  New  York  jumamosi  iliyopita   Bwana Ahmad Khan Rahami  ambapo  maofisa  wa  serikali  wanadaiwa  kumpatia  matibabu  mshukiwa  huyo  na  kisha  kumpatia  wakili  atakayemtetea  wakati  atakapopandishwa  kizimbani  kwa  tuhuma  za  ugaidi.

HALI YA KISIASA NCHINI KONGO IMO HATARINI

Watu  takribani  50  wamefariki  dunia  nchini  Jamhuri  ya  Kidemokrasia  ya  Congo  kufuatia  makabiliano  kati  ya  waandamanaji  na  polisi  katika  miji  mbalimbali  nchini  humo  yaliyoanza  jumatatu  wiki  hii  baada  ya  tume  ya   taifa  ya  uchaguzi  nchini  humo  kutangaza  kuahirisha  uchaguzi  wa  rais  hadi  mwaka  2017  kinyume  na  katiba   ya  nchi  hiyo.
Waziri   wa  mambo  ya  ndani  wa  Jamhuri  ya  Kidemokrasia  ya  Congo  Bwana  Evariste  Boshab  amesema  miongoni  mwa  watu  waliofariki  katika  maandamano  hayo  wamo  maofisa  kadhaa  wa   polisi  ambao  Waziri  huyo  wa  serikali  amesema  kuwa  baadhi    ya  maofisa  hao  wa  polisi waliuawa kwa  kuchomwa  moto  wangali  hai   na  waandamanaji  wanaomshinikiza  rais  wa  nchi  hiyo  Bwana  Joseph  Kabila  kuondoka  madarakani.
Aidha  kwa  upande  wake  mmoja  kati  ya  viongozi  wa  upinzani  nchini  humo  Bwana   Rene  Rughunda  alidai  ‘’Watu  wa  nchi  hii  wapo  tayari  kupambana  na  kurejesha  thamani  ya  demokrasia  ndani  ya  nchi  hii,  ikiwa  Bwana  Kabila  hataachia  madaraka  sisi  kama  watu  wa  nchi  hii  tutamlazimisha  kuachia  madaraka’’.
Miili  ya  watu  waliofariki  katika  maandamano  hayo  imeonekana  ikizagaa  barabarani  katika  mji  mkuu wa  nchi  hiyo  Kinshasa  ambapo  waandamanaji  wamechoma  moto  magari  ya  polisi  na  kuweka  vizuizi  barabarani. Upinzani  umepanga  kuendelea  na  maandano  zaidi  wiki  hii  ili  kuishinikiza  tume  ya  uchaguzi  ya  nchi  hiyo  kuratibu  tena  uchaguzi  wa  rais  nchini  humo  mwishoni  mwa  mwaka  huu  wa  2016  kwa  mujibu  wa  katiba  ya  nchi  hiyo.

Monday, 19 September 2016

NANGAA: UCHAGUZI MKUU CONGO HADI MWAKANI

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila.
Pamoja na mkutano  wa  upatanishi ulioongozwa  na  aliyekuwa  mwenyekiti  wa  umoja  wa  Afrika  Bwana  Edem  Kodjo  uliofanyika  nchini  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwanzoni  mwa  mwezi  Septemba  mwaka  huu  kati ya wapinzani na serikali ya nchi hiyo inayoongozwa na Rais Joseph Kabila.  Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri  ya  Kidemokirasia  ya  Kongo   imesisitiza   kuwa  hakuna  uwezekano  wa  uchaguzi  kufanyika  nchini  humo  mwaka  huu  kama ilivyoelezwa kwenye katiba  ya  nchi  hiyo.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya nchi hiyo ambayo ilitarajiwa kuanza mchakato wake wa kufanyika kwa uchaguzi kuanza jumatatu ya wiki hii, Bwana Corneille Nangaa amesema suala hilo kwa sasa haliwezekani na badala yake anashauri uchaguzi ufanyike mwaka ujao.




Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, Corneille Nangaa.
Kufuatia  tamko  hilo  hali  si  shwari  ndani  ya  miji  mikubwa  ya  Jamhuri  ya  Kidemokrasia  ya  Kongo  ambapo  makundi  ya  upinzani  yamefanya  mkaandamano  makubwa  katika  miji  ya  nchi  hiyo  ikiwemo  Kinshasa  na  Kivu  pamoja  na  maeneo  mengine  ili  kuishinikiza  tume  ya  uchaguzi  ya  nchi  hiyo  itengue  uamuzi  huo  na  kuruhusu  uchaguzi  ufanyike  mwaka  huu  kwa  mujibu  wa  katiba

ICJ YAANZA KUISIKILIZA KESI YA MPAKA KATI YA KENYA NA SOMALIA

Mahakama  ya  Kimataifa  ya  Haki  (ICJ)  inayoungwa  mkono  na  Umoja  wa  Mataifa  imeanza  kusikiliza  kesi  ya  kugombea  mpaka  kati  ya  nchi  za  Kenya  na  Somalia  mjini  The  Hague  nchini  Uholanzi, ambapo  mwanasheria  mkuu  wa  Kenya  Profesa  Githu  Muigai  amesema  ataongoza  jopo  la  mawakili  na  maofisa  wa  ngazi  za  juu  kutoka  nchini    Kenya   ili  kuitetea  nchi  hiyo.
Mwanasheria Mkuu wa Kenya, Profesa Githu Muigai.
 Aidha  mwanasheria  huyo  wa  Kenya  amesema  kuwa  Kenya  inataraji kuituhumu Somalia  katika  kesi  hiyo  kwa  kuvunja  mkataba  wa  mwaka  2009  ambapo  amesema nchi  hizo  zilikubaliana  kutatua  mzozo  huo  unaohusisha  sehemu  za  nchi  hizo  ndani  ya  Bahari  ya  Hindi  kupitia  mazungumzo.  Eneo  hilo  linalogombaniwa  lina  ukubwa  wa  kilomita  za  mraba  42,000  na  linasadikiwa  kuwa  na  utajiri  wa  mafuta  na  gesi.

Katika  mgogoro  huo  Somalia  inataka  mpaka  wake  wa  baharini  uendelee  kwa  kufuata  mstari  wa  mpaka  ulio  nchi  kavu  unaolekea  kusini  mashariki  mwa  nchi  hiyo  wakati  Kenya  nayo  ikitaka  mpaka  huo  uwekwe  kwa  kufuata  mstari  usiopinda  unaoelekea  mashariki,  hali  hiyo  imesababisha  kutengeneza  umbo  la  pembetatu  kutokana  na  madai  ya  nchi  hizo  mbili  za  Afrika  Mashariki. Kesi  hiyo inataraji  kudumu  kwa  wiki  moja  ili  kutoa  mwelekeo  wa  namna  nchi  hizo  zitavyofikia  maridhiano. 
Kesi hiyo iliwasilishwa ICJ tangu Agosti, 2014.




Friday, 16 September 2016

TRUMP AANZA KUAMINI KUWA OBAMA KAZALIWA MAREKANI



Hilo limetokea  baada ya Donald Trump kuanza kuamini Obama amezaliwa Marekani ambapo mgombea huyo kwa mara nyingine alisisitiza kwamba hayuko tayari kuamini kwamba Bw Obama alizaliwa Marekani. Akihojiwa na gazeti la Washington Post, Bw Trumo alikataa kusema Bw Obama alizaliwa Marekani na badala yake akasema hangejibu swali hilo.
Ofisi ya kampeni ya mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump imetoa taarifa ikisema sasa anaamini Rais Obama alizaliwa nchini Marekani.
Trump huchukuliwa mwanzilishi wa kundi lijulikanalo kama "birther movement", ambalo huamini Rais Barack Obama hakuzaliwa katika jimbo la Hawaii, na kwa hivyo hakufaa kuhudumu kama rais wa Marekani.
Anasema taarifa hiyo iliyotiwa saini na mshauri mkuu wa Trump, Jason Miller hata hivyo si kwamba anakubali makosa.
Badala yake, Miller aliweka lawama kwa Hillary Clinton na kundi lake la kampeni la mwaka 2008, ambapo Bi Clinton alikuwa anashindania tiketi ya chama cha Democratic na  Obama.
Hakuna ushahidi wa kumhusisha Bi Clinton na kundi la Birther. Akijibu, Bi Clinton alisema kupitia Twitter kwamba mrithi wa Rais Obama "hawezi kuwa mtu aliyeongoza kundi la ubaguzi wa rangi la Birther".
Wanaopinga kwamba Obama alizaliwa Marekani wamekuwa wakisema alizaliwa Kenya (babake Obama alikuwa Mkenya).
Taarifa katika magazeti kadha ya Marekani zinaashiria uvumi huo ulienezwa mwaka 2008 na wafuasi sugu wa Bi Clinton ilipoanza kudhihirika kwamba mwanamke huyo hangeshinda uteuzi wa chama cha Democratic.
Madai hayo baadaye yalifufuliwa na wafuasi wa mgombea wa Republican John McCain alipoanza kuachwa nyuma na Obama kwenye kura za maoni, tovuti ya Fact Check imeripoti.
Obama
Trump alianza kujihusisha na suala hilo kabla ya uchaguzi mkuu wa 2012.
Aprili 2011,  Trump alimtaka Obama kuonyesha hadharani cheti chake cha kuzaliwa, wito ambao uliungwa mkono na wanasiasa wengi wa Republican akiwemo aliyekuwa gavana wa Alaska Sarah Palin.
Mwaka 2012 mgombea wa wakati huo wa Republican Mitt Romney alirejelea madai hayo kwenye mkutano wa kampeni Agosti mwaka huo.


Chanzo:BBC Swahili

Monday, 5 September 2016

WIZI WA KURA AFRIKA MBIONI KUFIKIA UKOMO


Wakati nchi ya Gabon ikikumbwa na machafuko baada ya uchaguzi mkuu kuisha uliomrejesha Rais aliyekuwepo madarakani  Ali Bongo Ondimba, mwana wa Rais wa zamani Omari Bongo wataalamu wa mambo ya chaguzi wanadai udanganyifu wa matokeo barani Afrika unazidi kuwa mgumu,  huku kwakuwa wananchi wenyewe wanasimamia vyema  ulinzi wa kura,  mashirika mbalimbali ya kijamii ambayo yamekuwa mstari wa mbele kufuatilia chaguzi mbalimbali, kukosoa pamoja na kuenea kwa teknolojia ya simu za mikononi.

Ijumaa ya wiki iliyopita kiongozi mkuu wa upinzani nchini Gabon, Jean Ping  alijitangaza kuwa mshindi  na Rais halali nchini Gabon na kutaka kurudiwa upya kwa uhesabuji wa kura, kufuatia  madai ya Rais Ali Bongo  kuwa aliibuka mshindi kwa kura zaidi ya elfu sita katika uchaguzi uliofanyika Agosti 27 mwaka huu. "Kwa chaguzi za hivi karibuni hasa Afrika ya Kati na Magharibi nchi za Senegal, Ghana na Cape Verde zinaonyesha jinsi gani demokrasia inavyokomaa" anadai  ndugu Aboubacary Mbodji, katibu mkuu wa kundi la kudai haki la RADDHO.

Meneja wa tasisi ya siasa na utawala wa Afrika Magharibi(OSIWA), Mathias Hounkpe amesema kuwa  kadiri miaka inavyozidi kwenda udanganyifu kwenye chaguzi unazidi kuwa mgumu.

Meneja wa tasisi ya Siasa na Utwala wa Afrika Magharibi(OSIWA,  ndugu Mathias Hounkpe.

Afrika Magharibi imekuwa katika wakati mgumu wa machafuko hasa yanayotokea Gabon na yale yaliyotokea Senegal na Burkinafaso miaka ya nyuma.
Nchi za Afrika Mashariki pia, ikiwemo Tanzania, Uganda na Burundi zimekuwa katika hali ya kuarifiwa kuwepo kwa udanganyifu kwenye chaguzi kutokana na baadhi ya wagombea kulalamika waziwazi kuwa wameibiwa ila hayajaleta mchafuko makubwa kama ilivyo  hali ya Afrika Magharibi.

Saturday, 3 September 2016

MAREKANI NA CHINA ZAIDHINISHA MKATABA WA MABADILIKO YA HALI YA HEWA YA PARIS


Nchi za Marekani na Uchina ambazo kwa pamoja huzalisha gesi chafu ya kaboni duniani kwa 40% - sasa zimeidhinisha mkataba wa Paris wa mabadiliko hali ya hewa duniani.
Baada ya kuwasili napamoja na viongozi wengine wa mataifa ya G20 kwa mkutano katika jiji la Hangzhou, rais wa Marekani Barack Obama amesema: " Historia itahukumu juhudi za leo kama za la muhimu na mafanikio”.
Kupunguzwa kwa gesi aina ya CO2 ndilo lengo linalotegemewa katika mabadiliko ya hali ya hewa.
Hatua kubwa kuelekea utekelezwaji wa makubaliano haya ilifikiwa mwezi Disemba, ambapo mataifa hayo yalikubaliana kupunguza gesi chafu kwa kiwango cha kuwezesha kupanda kwa joto la dunia kufikia chini ya nyuzi joto 2.
Mapema Jumamosi wajumbe wa kamati ya bunge la taifa la kongresi la watu wa Uchina- China's National People's Congress waliidhinisha "pendekezo la kuchunguza upya na kuidhinisha mapatano ya Paris " Jumamosi asubuhi katika kilele cha wiki nzima cha vikao vya bunge.
Mkataba wa Paris ni mapatano ya kwanza kuwahi kuzingatiwa zaidi miongoni mwa makubaliano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa duniani.
Utekelezwaji wake utakubalika rasmi kisheria baada yakuidhinishwa na nchi 55 zinazozalisha 55% ya hewa ya Kaboni duniani.

Chanzo:BBC Swahili