Nchi za Marekani na Uchina ambazo kwa pamoja
huzalisha gesi chafu ya kaboni duniani kwa 40% - sasa zimeidhinisha mkataba wa
Paris wa mabadiliko hali ya hewa duniani.
Kupunguzwa kwa gesi aina ya CO2 ndilo lengo linalotegemewa
katika mabadiliko ya hali ya hewa.
Hatua kubwa kuelekea utekelezwaji wa makubaliano haya
ilifikiwa mwezi Disemba, ambapo mataifa hayo yalikubaliana kupunguza gesi chafu
kwa kiwango cha kuwezesha kupanda kwa joto la dunia kufikia chini ya nyuzi joto
2.
Mapema Jumamosi wajumbe wa kamati ya bunge la taifa la
kongresi la watu wa Uchina- China's National People's Congress waliidhinisha
"pendekezo la kuchunguza upya na kuidhinisha mapatano ya Paris "
Jumamosi asubuhi katika kilele cha wiki nzima cha vikao vya bunge.
Mkataba wa Paris ni mapatano ya kwanza kuwahi kuzingatiwa
zaidi miongoni mwa makubaliano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa duniani.
Utekelezwaji wake utakubalika rasmi kisheria baada
yakuidhinishwa na nchi 55 zinazozalisha 55% ya hewa ya Kaboni duniani.
Chanzo:BBC Swahili
No comments:
Post a Comment