Showing posts with label JAMII. Show all posts
Showing posts with label JAMII. Show all posts

Friday, 14 October 2016

“Argue, Don't Shout" Ya Mwalimu Nyerere Tuiishi Kwa Vitendo

Hii ni makala niliyokuwekea uisome hapa Oktoba 14, ila siku iliyofuata Oktoba 15, 2016  imepata nafasi kwenye gazeti la TanzaniaDaima
   
   
Na 
Peter C. Mmbaga

Ndiyo muda wangu wa kuingia “Giningi” na Wabasi  wenzangu ambao tunaamini kwenye mawazo ya  chanya pasipo kupepesa  macho, safari ya Giningi inahitaji ufunge mkanda kweli kweli na leo nipo njiani kuongea na  kumpa pongezi za  “kuondoka” zake mapema mbasi wangu katika fikra Mwalimu mkuu, Baba Makongoro  kwakuwa angebaki mpaka sasa angekuwa anaduwaa kama mimi na vile hapendi  kuonekana  kwenye   “maamuzi  ya umimi”,  anakuwa mpole tu.
Kumbuka kipindi kile wakisema  baadhi ya viongozi   waliokuwa wanafanya mambo  tofauti, yeye alitoa tamko gani? Kwenye kitabu chake cha “Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania” anabaki kama mshauri tu, japo kutokana na hadhi yake ama “popularity” aliyokuwa nao asingesikilizwa na wananchi kweli, katika kukataza?
Aliwaachia uhuru wajitathimini  wenyewe, na uhuru ni mbaya sana, walipoona   mbasi wangu katika fikra  chanya hajaja juu wakaona sawa tu, mambo yanafanyika,  anajifanya haoni. Kumbe “mbasi” ulikuwa “unawachora” tu.
“Giningi yetu” ina raha yake huku yupo Baba wa maridhiano, mbasi wangu katika fikra, Mandela yeye anatabasamu tu anasema “Real leaders must be ready to sacrifice  all for the freedom of their people“ kwa tafsiri isiyo rasmi ni kuwa “ Vingozi wa kweli wanatakiwa wawe tayari kujitoa vilivyo kwa  uhuru wa wananchi”, naye namwangalia natabasamu  kwa kuwa kazi aliyoiamua  Rais JPM ni ngumu  sana kwakuwa  wapiga vita mfumo  mzuri wapo  na hasa watendaji, “We got a Long Way To Freedom” ila kwa imani atawatumbua tu!
Baba Makongoro bwana ananifurahisha sana akasema “Siku Wamarekani wakinisifia nimefanya kazi nzuri nitajiuliza kuwa nimekosea wapi?”  ndiyo kitu nilichompendea hasa kwa kauli hizi za kujiamini kwa nukuu nilyooina kwenye gazeti moja la kila siku miaka mitatu nyuma, ni kauli ya Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), chuo ambacho Mwalimu alikianzisha na mara kwa mara kufika hapo kwa ajili ya mijadala na wanafunzi kuhusu uhuru na maendeleo ya Afrika na dunia kwa ujumla, Bashiru Ally, anaamini Mwalimu anastahili  kupewa tuzo  lakini ananyimwa kutokana na kuyaudhi mataifa ya magharibi wakati aliongoza harakati za kudai haki za binadamu na uhuru wa mataifa ya Afrika. Huu ndiyo ushujaa tunaouhitaji Rais JPM piga kazi kwa haki na kweli usihitaji kusifiwa na watu wa nje ila tu angalia uhuru uwepo kama Baba Makongoro alivyoutoa. Mwalimu vijana wa leo sio wa kipindi kile  “pesa” inawanunua wanashindwa kutetea maslahi ya nchi,  hasa wasomi dira hawaileti , ukanijibu “pesa ni matokeo” kama ulivyoainisha kwenye kitabu chako cha cha “Ujamaaa na Kujitegemea” lakini Mwalimu sasa sivyo, nadhani wakati nao unabadilika, ila  wanaamini,  pesa ndilo lenye nguvu!
Sasa hivi wasomi wanaonekana shujaa  kwenye dimbwi la mfumo  huu wakuogopa kuhoji, vyuo vikuu vimepoa  vimenyamaza, nahisi huko ndiko ulipowasikia kwa mara ya kwanza   kina ndugu Lowassa, JK  na wengineo,   ila sasa wanaogopa  kuitwa wasaliti ni bora kuliko kuonekana mnyenyekevu kwao halafu kwenye jamii uonekane “Kamuzu”. Wazee wetu  ukiwauliza watakujibu enzi za kupigania uhuru walimwita   huyu mtu walimwitaje  "aliyeolewa na wazungu" aliwabania waafrika haki zao, ndiyo nyimbo iliyokuwa kwenye mchamchaka.
Kwanini nimesema hayo?  Nakumbusha raia wote  na viongozi wasaliti kwa machinga, boda boda, mama ntilie , wasakatonge , wasio na ajira ni bora uonekane umemsaliti rafiki yako anayetafuta  “ujiko” kwa njia ya  “matukio” kuliko kuitwa "umeolewa nao" na jamii ni mbaya sana,  lakini Mwalimu hao watu tunao?
Wewe mwenyewe ukasema “Unyenyekevu ukizidi unazaa uoga, uoga huzaa unafiki na kujipendekeza, mwisho wake mauti”
Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu J.K Nyerere

Baba Makongoro kuna walimu  wamekuwa  ‘maarufu” kwa kipindi hichi kubwa ni kumpiga mwanafunzi  wa kidato cha tatu mwezi huu uliotuaga, kuna kitu baba nimegundua Walimu wengi wanakwenda pasipo ‘passion”, lengo ni kupata mkopo ambao miaka ya karibuni imekuwa  kipaumbele kwa walimu ili kusaidia changamoto za elimu yetu, japo wanafunzi wa siku hizi ni watukutu kufikia hatua ya kuchanganywa na malezi na utandawazi ambao tumeupokea “negative” sana kwenye matumizi yake.
Mtoto  kupewa adhabu hatujakataa, ni moja ya kufunza baba, kama wewe ulifanya pale Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam kwa mmoja wa viongozi wetu kugoma akiwa  Rais wa serikali ya wanafunzi-Daruso  enzi zako  wakigomea kutopatiwa maziwa na siagi, kweli enzi zako “walikula bata”  mbasi wangu, leo hii wanasota watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu  “no mkopo”, kipaumbele kimeharibu kila kitu na wengi wanakimbilia huo ualimu,  tasnia nyingine baada ya miaka kumi wasomi wengi watakuwa kwenye  tasnia moja halafu wasio na “passion” japo sio wote ama tasnia zote lakini Je, hali itakuwaje?
Enzi zako mtu akisema mimi ni mwalimu hiyo heshima anayopewa  ni nzito lakini leo sielewi, thamani imepungua sijui kisa ni nini? Ndo maana misongo ya mawazo  inakuwa mingi sana hata kupiga wanafunzi.
Mimi kusema kula bata ni kweli kwasababu   habari  hii niliwahi  kuhadithiwa na “anko” wangu aliyesoma na ndugu Rais  mstaafu kijana wako, Jakaya  Kikwete pale Shule ya Tanga (Tanga  School) enzi zako  Mwalimu Mkuu wa fikra yakini,  juu ya elimu,chakula(asubuhi chai nzito), na usafiri wa  bure kwa gharama za Serikali.  Ila nyakati zinabadilika!
Wakati tunaendelea na maongezi yetu ya Kibasi zaidi huko “Ginigi yetu”  kuna  msomi  enzi zake Mwalimu  akaniuliza leo hii madaftari  yanauzwa  kwa shilingi ngapi  wanafunzi, vipi madawati shuleni?  Nikamwambia najua, wajua, akanijibu halafu tuna misitu mikubwa nchini?
 Baba Makongoro ulivyooondoka kuna mwana hip hop aliimba “wasomi wanakimbilia siasa, Je, nchi itajengwa na nani? Hata mimi najiuliza nchi itajengwa na nani? Sielewi!

Mwalimu alizidi  nitoa tongotongo katika kuandaa  na maswala mengine yenye maslahi kitaifa yasiyohitaji mgawanyiko wa itikadi na uchama  kwa kile  waingereza wanachosema “number do not lie” wakimaanisha  nambari haidanganyi kwa kufanya mambo kwa  “ tathmini onyeshi” moja ni moja na nane si saba, kwakumshangaa  Waziri mwenye dhamana ya Afya  kukinzana na  Makamu wa Rais, kuhusu upungufu  wa madawa kwenye bohari ya Taifa!
Nakamwambia Mwalimu neno “siasa” ni mwiba kwa wananchi si neno  zuri kulizungumza  japo Rais JPM anawapa matumaini kuwa utendaji wake kwa kiasi chake kuna tija imeonekana Mwalimu,  kabla hatujaendelea zaidi   nikatafakari kuwa  ujasiri ni pale unapojua "siasa" si tatizo bali tatizo ni picha na taswira iliyojengeka mtu kuwa "mwanasiasa" ndani ya jamii na jibu tunalo kwa utendaji mzuri wa viongozi wetu  ili kugeuza neno "politics is dirty game". Itabadilika tu hii hali, kama enzi zako Ualimu ulivyoheshimika leo hii unaonekana taaluma ya kawaida! Sisi wenyewe hatupendi Mwalimu.
Nikamwona kifkra shujaa wa India, Mahatma Ghandi na falsafa yake kuwa “I love your Christ but not your Christianity” nikimaanisha  serikali na vyama vya siasa  ni sehemu salama na sera zenye weledi lakini  walioko ndani yake ndiyo kuna kila aina ya ubaya,udhalimu, na siasa chafu japo kuna wasafi na wenye kweli daima. Naipenda sera weledi yenye utekelezaji, itikadi ninayo,na “imani” kwa  kiongozi na mwananchi  mwenye misingi fanikishi ya kuileta “Tanzania ninayoitamani”, si kauli za kutofautiana  za  “makaisari” wetu na sio  ushabiki wa chama. Haya yakifanikiwa mbona “siasa nyeupe” itaonekana na tuishi ili kumuenzi Baba wa Taifa na hilo ndilo kusudi lake, siku siku ya leo tutoe  “speech” za kumsifia ila  hizo  sifa zake ninyi kiuhalisia na kiutendaji  mnaziishi kwenye vyombo vya habari.
Watanzania ni wepesi wa kusahau kama  zao la “kuamua” litaleta watu makini, wazalendo,wenye dira elekevu, na misimamo binafsi   tutakuwa tumefikia kiwango kikubwa katika “mchakato” wa kujitambua na kuutambua ukweli na ule mtazamo wa siasa ni mchezo mchafu (politics is the dirty game) tukiishi ya Baba Makongoro na sio kuienzi siku yake bila matendo sio maneno. Hata  Baba Makongoro kwenye “mjadala” wetu hapendi hilo swala.
Alichopenda ni “Argue, Don’t shout” na hichi ndicho serikali inakinzana na vyama vya upinzani sana, kwasababu kila mmoja anatoa kinachojipendelea ila tukumbuke tunajenga moja, Tanzania yetu katika siku hii ya kumuenzi Baba wa Taifa sio kwa makelele na sifa kedekede bila kuishi aliyoyaishi!
Pumzika kwa amani Mkuu, muda mwingine tutatembeleana!

Description: https://ssl.gstatic.com/ui/v1/icons/mail/images/cleardot.gif

Wednesday, 12 October 2016

KANSELA MERKEL AZINDUA JUMBA LA MWALIMU NYERERE ADDIS ABABA


Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amezindua jumba jipya makao makuu ya Umoja wa Afrika ambalo limepewa jina la rais mwanzilishi wa taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere ambaye siku ya Oktoba 14, 2016 itakuwa kumbukumbuku ya kifo chake.
Jumba hilo ambalo jina lake kamili ni Jumba la Amani na Usalama la Julius Nyerere limejengwa kwa ufadhili kutoka Ujerumani.

Litakuwa makao ya idara ya Amani na Usalama ya AU na litatumiwa pia na maafisa wa kutoa tahadhari ya mapema kuhusu mizozo barani pamoja na kuratibu juhudi za kulinda amani za AU.
Ujenzi wa jumba hilo, ambalo ukubwa wake wa sakafu ni mita 13,500 mraba na linaweza kutumiwa na wafanyakazi 360, uligharimu euro 27 milioni.
Jumba hilo afisi za kufanyia kazi, vyumba vya mikutano vya kutumiwa na Baraza la Amani na Usalama, chumba cha kuratibia shughuli, maktaba na vyumba vya shughuli za pembeni.

Mwalimu Nyerere, ambaye alikuwa rais wa Tanzania hadi 1985, alikuwa mmoja wa viongozi waanzilishi wa Muungano wa Nchi za Afrika (OAU) ambao sasa ni Umoja wa Afrika (AU).
Alishiriki sana katika jitihada za kuendeleza bara la Afrika na kusaidia mataifa ambayo hayakuwa yamepata uhuru kujipatia uhuru wake.
Mwalimu Nyerere alipigania sana kumalizwa kwa ubabe wa Wazungu katika nchi za Rhodesia (sasa Zimbabwe), Afrika Kusini, na taifa la Kusini Magharibi mwa Afrika/Namibia (sasa Namibia).



Chanzo: BBC Swahili

10 HARSH “TRUTHS” NOT TO BE AVOIDED WHICH WILL MAKE YOU A BETTER


One medieval philosopher Saint Thomas Aquinas once said “There is no higher GOD than truth”, live truly who you and accepting truth whenever pour on you.
Medieval Philosopher, St.  Thomas Aquinas 
Life is a hard place and most of us can be forgiven for feeling we are on the losing end of it. The simple truth is no one has an easy ride; most of us have had some serious ups and downs along the way. Below are 10 harsh truths that will make you a better person;

1. Life isn’t fair
Of course life isn’t fair it never is. The challenge is to find someone who has had an easy life all the way through, they don’t exist. The sooner you except this fact the happier you’ll be.
2. The first step is the hardest
Well it may be. It is also good to reach outside our comfort zone from time to time. The problem with comfort zones is they get smaller and smaller with time. Reaching out, and doing something new, can revitalize us and make us more rounded people.

3. Good things don’t come quickly
There is the opposite adage that good things are worth waiting for. The reality is good things are happening all the time. Okay, you didn’t win the lottery this week, but the chances are lots of good things have happened to you, be they small and fleeting. Make a note of the good things that happen each week, you’ll be surprised.
 
4. Not everyone gives support
It would be very strange if they did because we are all made up of different personalities, values and have different points of view. It would be impossible to please everybody all the time, there will always be doubters. Never let these people stop you from going for your goals and passions. These are the very things that make you a better person.



5. You can’t always be in control
That’s the way the world is made up, there will always be things you have no control over. The boss has control over you; the Inland Revenue has control over you along with your wife or husband. This is life, live with it, but don’t let it stop you from reaching out for your aims.
6. You can only accomplish great things with taking risks
Risk taking is a part of life; any successful businessman will tell you this. If you’re not prepared to take risks you will have harder time accomplishing what you want in life.

7. You’ll be better off without people you currently care about
Yes that’s true. You’ll be better off because you won’t have to worry about a loved one, falling ill, dying, or falling out of love. However, would being on your own without all this responsibility make you happier? It seems unlikely as the precious things in life are people, not money or possessions.
8. Death is a part of life
Yes that is true. Live with it, and that is not supposed to be a pun. There’s things you can do to make losing a loved one a lot less distressing: make them a bigger part of your life right now. Little things like making that call or paying a flying visit to a friend you haven’t seen in a while. These things will make you a better person.



9. You are the only thing holding yourself back from greatness
Being negative will hold you back. Instead, focus on the positive things and be happy now.

10. Bad things happen to good people
That’s the nature of life, the good die young too. But the opposite is also true, the good have good things happen to them, and the good can live to ripe old age.






HISTORIA ILIOJEE: BIBI TITI MOHAMED

Bibi Titi Mohamed

 Ni HISTORIA ILIOJEE! mwanamke jasiri, shujaa na mwenye msimamo, moja ya barabara kuu ndani ya jiji la Dar es Salaam, jina lake limo kwa heshima ya mchango wake mkubwa wa  kuleta uhuru wa Tanganyika.
Si mwingine ni Bibi Titi Mohamed,  mwanamama, aliyekuwa kiongozi  mmojawapo katika  harakati za kudai uhuru wa Tanganyika, baadaye aliongoza Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT), chama cha wanawake katika chama cha Tanganyika African National Union (TANU), na baadaye akawa waziri wa wanawake na masuala ya kijamii katika serikali ya Mwalimu Nyerere.
Bi Titi  Mohamed alikuwa mwanamke wa Kiislamu aliyezaliwa jijini Dar es Salaam mnamo  mwaka 1926 na baba mfanyabiashara na mama mkulima. Alipata elimu ya shule za msingi pekee na alipofikisha  umri wa miaka 14 tu aliolewa na mume mzee.
Bi Titi Mohamed alipata nguvu  ya kuwa mwanaharakati   kupitia kipaji cha kuimba, enzi za ujana wake alikuwa mwimbaji mzuri wa kwasida na hivyo kuwa  kama mwimbaji kiongozi katika ngoma katika kikundi cha muziki na ngoma ambacho kilimwongozea uzoefu wa kuwa mbele ya umati.
Nguvu ya kushiriki katika majukumu ya uongozi na uhusiano ndani ya mitandao wanawake na mapambano ya kitaifa yallianza mwaka 1950, baada ya Vita Kuu ya II ya dunia, Tanganyika ikiwemo nchi  nyingine katika harakati za uzalendo zilikuwa zimeshika kasi. Mwaka 1954, TANU iliundwa chini ya uongozi wa mwalimu na  baadaye Rais Julius Nyerere. 
Bibi Titi na Mwalimu J.K Nyerere kwenye pozi enzi hizo
Muda si mrefu baadaye mwaka  1955, Bibi Titi alikasimishwa  kiti cha UWT, na ndani ya miezi mitatu ya uteuzi wake, walijiunga wanawake zaidi ya 5,000 kama wanachama wa TANU, na hivyo kwa mrengo huo wa  wanawake uliianzishwa na jukumu kubwa kwa mapambano ya uhuru na UWT kufanya kazi kubwa ya kukuza maadili  ya TANU kwa raia. Pia umoja wanawake ukapaza sauti moja katika mapambano dhidi ya ukoloni.
 Bibi Titi kupitia wanaharakati wanawake walikuwa na uwezo wa kutumia mitandao yao mbalimbali ya kijamii na kiuchumi kwa kuongeza fedha kwa kiasi kikubwa kwaajili ya chama cha  TANU. Zaidi ya hayo, Bibi Titi akiwa na kipawa cha  usemaji, yeye mwenyewe, alihamasisha wanawake kupitia makundi ngoma na kusimamia viongozi wao kuunda nafasi kwa ajili ya kushughulikia wanachama na kuwasaidia, pia  makundi hayo yalikuwa wazi kwa wanawake wote waliotaka kujiunga, na kuishia kuwa mitandao yenye nguvu  kisiasa ajili ya kubadilishana taarifa,  tangazo la mikutano ya kampeni na maandamano.

Mwishowe mafanikio yaliingia  mwaka 1961,  kwa Tanganyika kupata Uhuru. 
Bibi Titi Mohamed bahati mbaya kisiasa  ilimpata mwaka 1965 wakati alipopoteza kiti chake cha ubunge. Mwaka 1967, yeye alijiuzulu kutoka uwaziri .
Baadaye alipata masaibu ya kisiasa  kwa kiasi kikubwa ilifanya kutoweka katika maisha ya umma na  baadaye   mnamo   Novemba 5, 2000,  Bibi Titi Mohamed pumzi yake ilirejea ilipotoka katika  hospitali ya Net Care huko Afrika Kusini.
HISTORIA ILIOJEE inajivunia Bibi Titi, mwanamama wa shoka, malkia wa nguvu  atakumbukwa kwa mengi,  heshima yake  ipo kwenye kutoa mwanga wa harakati za wanawake dhidi ya mfumo  mibovu  kwenye kila nyanja ya maisha,  kwetu sisi  WAUNGWANA ni HISTORIA ILIOJEEE!




Unakaribishwa kuacha comment yako hapo chini!

JPM AWATAKA WATUMISHI KUREJESHA POSHO


Rais JPM amewataka Watumishi wa Umma walioalikwa katika kilele cha sherehe za Mwenge ambazo zitafanyika tarehe 14 Oktoba kutohudhuria na warudishe posho za safari walizolipwa. 
Viongozi waliotajwa kutakiwa kufuta safari zao za kwenda Bariadi ni pamoja na wakuu wote wa mikoa, wilaya, wakurugenzi wote wa  mamlaka za serikali za mitaa, mameya, na wenyeviti wote wa Halmashauri  za majiiji, manispaa, miji na wilaya pamoja na watumishi ambao huambatana nao wakiwemo madereva na wasaidizi wao ambao kwa idadi hufikia takribani 1,500.
Kwa kuwa sherehe za kilele cam bio za mwenge wa Uhuru huambatana na maandhimisho ya siku ya kumbukumbuku ya Baba wa Taifa, hayati, Mwalimu J.K  Nyerere aliyefariki miaka 17 iliyopita, agizo hilo limewataka viongozi wote wa mikoa na wilaya kubaki katika maeneo yao ya kazi na kujiwekea utaratibu wa jinsi ya kuienzi siku hiyo.

 Hii hapa ni “Press Release” ya taarifa hiyo.

Tuesday, 11 October 2016

HAPPY EARTHSRONG "SHUJAA" SIR BOB CHARLTON

Sir Bob Charlton enzi zake.
Leo bwana ndiyo “birthday”  ya shujaa Sir Robert "Bobby" Charlton alizaliwa  11 Oktoba  1937. Ni mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu wa Uingereza, Anajulikana kama mmojawapo wa viungo wa kati wenye uwezo wa hali ya juu wa muda wote. Nembo muhimu katika timu ya taifa ya Uingereza ambapo alishinda Kombe la Dunia na Ballon d'O r mwaka 1966. Yeye alicheza karibu muda wote katika klabu yake  ya Manchester United, ambapo alikuwa mashuhuri kwa uwezo wake wa kushambulia na kupiga mashuti yaliypachikwa jina "Long Lange Shot" yaliyopigwa toka umbali mrefu. Alionywa kwa kadi mara mbili tu katika maisha yake ya soka; mara moja dhidi ya Argentina mwaka 1966 katika Kombe la Dunia, na katika mechi ya ligi kuu dhidi ya Chelsea. Alizaliwa huko Ashington, Northumberland. Charlton alicheza mechi yake ya kwanza kwa Manchester United katika kikosi cha kwanza mwaka 1956, na zaidi ya misimu miwili alipata nafasi ya uhakika katika timu. Ni moja ya wachezaji walionusurika katika ajali ya anga mjini Munich mwaka 1958 baada ya kuokolewa na Harry Gregg, baada ya kuisaidia timu ya Mashetani Wekundu kushinda kombe la Football League mwaka 1965 pia alishinda Kombe la Dunia na medali katika timu ya taifa ya Uingereza mwaka 1966 na kombe la “Football League” akiwa na Mashetani Wekundu mwaka uliofuata. Mwaka 1968 akiwa nahodha wa Manchester United alishinda Kombe la Ulaya akifunga mabao mawili katika mechi ya fainali . Amefunga mabao zaidi kwa United (249) kuliko mchezaji mwingine yeyote na kutokea kuwa mfungaji bora England wa muda wote  wa timu ya Taifa kwa mabao 49  na Wayne  Rooney kumpiku juzi kati kwa goli 50 katika mechi 107 alizocheza.


Hivyo kuanzia Mei 1968 hadi Septemba 2015, kwa Rooney kuvunja rekodi hiyo ndani ya Uingereza. Bobby Charlton alikuwa na rekodi ya kucheza mechi nyingi kwa Manchester United (758), kabla ya kuzidiwa na Ryan Giggs. Aliichezea Uingereza mara nne katika Kombe la Dunia (1958, 1962, 1966, na 1970), na kuisaidia Uingereza kushinda shindano hilo mwaka 1966.
Sir Bob Charlton siku za karibuni
Wakati wa kustaafu kwake kutoka timu ya England mwaka 1970, alikuwa ameichezea timu ya Taifa mechi nyingi kuliko mchezaji yeyote (mara 106 katika ngazi ya juu) ila Wayne Rooney kaivunja kwa mechi 107, kwa aliyocheza  mwaka jana dhidi ya Uswisi. Rekodi hii tangu wakati huo ilikuwa kwa upande wa Bobby Moore na Peter Shilton. Aliondoka Manchester United na kuwa meneja wa Preston North End katika msimu wa 1973-1974. Ambapo alikuwa mchezaji-meneja na baadaye kuwa mkurugenzi wa Wigan Athletic, Msimu uliofuata akawa mwanachama wa bodi ya wakurugenzi Manchester United tangu mwaka 1984 mpaka sasa msimu wa 2016/17.


Huyu ndiye Sir Robert "Bobby" Charlton aliyeshikilia rekodi ya ufungaji wa mabao Uingereza kwa miaka 47, HAPPY BIRTHDAY LEGEND!



Unakaribishwa kuacha comment yako hapo chini!

Saturday, 8 October 2016

UKITAKA KUMFUGA CHATU, UANDAE UNGA WA KUMLISHA

Hii ni makala yangu  iliyotolewa leo Oktoba 8, 2016 kwenye gazeti la TanzaniaDaima, kama hukupata nakala yako na kwa kukujali msomaji wa petermmbaga.blogspot.com isome hapa kwa utulivu.



Na
PETER MMBAGA, UDSM(SJMC)

“Ukitaka kumfuga chatu, uandae unga wa kumlisha”  hiyo ni kauli ya “kijana wa zamani”   kwenye kijiwe kimoja nikiwa kwenye harakati za kumng’ojea mgeni  wangu kituo cha daladala  mida ya jioni baada ya jua  kunipiga vilivyo mchana wake, nikamuuliza “kijana wa zamani” unamaanisha nini?
Akanambia kijana huelewi nini? Mimi nina elimu ya mkoloni nayo inanipa nguvu kudadavuadavua  yaliyomo kidogo, Je, wewe vipi?
Nikamwambia nijibu basi  “mzee kijana” akasema “homu weki” hiyo, wakati natafakari kabla  mzee hajatoa hoja ya msingi juu ya maana ya msemo wake, ndipo stori kijiweni zikazidi kunoga, kuna mshikaji moja akazungumza kuhusu  UKUTA(akimaanisha operesheni ya  CHADEMA) aliyotakiwa kufanyika septemba mosi ikasogezwa tena oktoba mosi kisha kuahirishwa kwa mara nyingine.
Jamaa mmoja akadai hawa  maCHADEMA nao wamezidi kila kitu wanahisi wanaonewa, mwacheni  ndugu Magu(Rais John Magufuli) apige kazi bwana! Mzee tunayemwita “mzee wa busara”  akajibu hii ni kizungumkuti kila mtu anavutia kwake ila serikali iwe makini kwa kauli ya rais kusema hakuna siasa  mpaka 2020, sasa kazi ya vyama vya siasa ni nini?
Kuna mvutano wa CUF na Profesa Ibrahimu  Lipumba  nikawa nawaza kichwani mwangu wakati huohuo kuna mbasi akaja na akatusikilizisha sauti  ya Rais JPM juu ya kuhamia Dodoma. Kwa hisia kidogo akataja kuwa haiwezekani baba wa Taifa mwalimu Nyerere alisema makao makuu ni Dodoma hivyo kupinga”.
Mzee anayeuza kahawa akasema naona mmedakwa na kuhamia Dodoma, Yule mleta hadithi za Dodoma akasema “Bongo iliitwa Tanzania kila kitu kilipatikana hapa, get ready with dom” akatia na umombo  kwa mbwembwe kidogo, tukacheka sana!
Uchumi wa Tanzania, au uwepo wa Tanzania unahitaji kutegemeana ili kumvusha mama Tanzania kwenye lindi la umaskini, sasa wakati ninawaza hilo mulemule jamaa mmoja akasema “mgawanyiko wa kiuchumi na kiutendaji unabidi uguse nchi nzima”, serikali si inahama yote bwana!
Tukashindwa kuelewa anamaanisha nini? Akasema ule mlundikano wa wizara hapa Dar, au ukipita mtaa wa Magogoni unaona nini? Tukashangaa, nikamuuliza kwani tatizo ni nini?
Akanijibu “Mbasi nawe unaonekana huoni mbali, mimi naona tugawe wizara hata kimkoa  au kikanda hivi kama Arusha ndiyo kitivo cha utalii Tanzania, ni vema Wizara hata ikawa pale, haya maswala ya bandari na usafirishaji wa maji ukaa “centre” ya mikoa husika kama Dar, Tanga na Mtwara”
Mzee mkongwe akasema ni wazo zuri lakini mbona kwenye ofisi za mkoa ama wizara, ofisi ndogo za mkoa zipo hizo ofisi hata nchi zilizoendelea sidhani kama zina kitu kama hicho! Mbasi mmoja akasema hiyo haitoshi ila ili kuweka mgawanyo wa kiserikali, ili “decentralization” ya serikali za mitaa mpaka serikali kuu hawafiki vyema, hii ni sera ya kibunifu!

Mzee kijana akasema enzi hizo kwenye historia  ya utawala wa Mwingireza  kama vijana mnasoma,  Idara za serikali zilikuwa hazipo mikoani na wakuu wa Idara hawakutaka kuhama Dar, mchakato wa kupata sehemu tulivu ya mji mkuu mpaka kufika mwishoni mwa mwaka 1920, Idara ya kilimo na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mashariki zilihamia Morogoro, Idara ya mifugo ilikwenda Mpwapwa sasa je, kwa mgawanyo huo tu wa kipindi hicho wizara haziwezekani kweli? Tukajiumauma tukijibu “inawezekana mzee, eeh inawezakana mzee ila kwa mipango”
Kuna jamaa akatoa nje mada kidogo akadai “ving’ora viletavyo foleni vitapungua jijini bora waende dom”, tukamshangaa nikajiuliza hivi foleni Dar kumbe inachangiwa na misafara ya hawa waheshimiwa, nikacheka kidogo!
Wakati kahawa inaendelea kuchemshwa mzee wa kahawa akasema “nasikia wakuu wanaharakisha uboreshwaji wa hadhi ya kimataifa  hata kwa viwanja vya ndege Dodoma kurahisisha usafiri na hata mdege  umeshuka juzi toka Kanada”,  kuna mfanyakazi mmoja wa benki akadai mbona ukarabati wa  uwanja Dar unafanyika pia, hapo hakuna hoja labda useme fursa gani zimekwepo baada ya uwepo wa uwanja mkubwa wa Dar, ajira zimetoka na zitakazotoka kwa upanuzi unaoendelea.
Jamaa mmoja akanena “hapa Bongo hawajapaendeleza kivile, nadhani wangepaendeleza Dodoma vyema na nchi kiujumla hata kama wazo ni la tangu uhuru kuhusu kuhama, je, mikakati waliyoanza nayo kwa awamu zilizopita ikoje? Nikamjibu  jibu la swali kwa swali “kuhusu miundombinu kiujumla eeeh?”
Yule jamaa wa benki akamjibu “umefanya utafiti kuwa hawajajiandaa vyema, utafiti mbele ndipo ukosoe”, akabaki tunashangaa, asijue la kujibu!
Nikamuuliza mzee kahawa vipi? Akajibu piga domo kwanza, ndipo nikauliza hivi huo uchumi mnaozungumzia mipango miji inaridhishaje? Mzee wa kahawa akadakia akasema walicho “bugi” muda mrefu Dar haikuwa na mipango miji, na mimi nkamropokea “kazania kahawa wewe”
Mshikaji mmoja akajibu “mzee kaongea bonge la hoja wewe, mipango mikakati hamna jiulize wazo dogo la kujenga hata “hoteli” ya nyota kadhaa pale jirani na uwanja wa ndege wa J.K Nyerere  ili kupambana na ajira, pato la taifa, foleni  pamoja na muda kwa wasafiri  hilo haliwaziki kabisa, hii ndio Tanzania”
Aliposema foleni nikamkumbuka mbasi wangu mmoja aliyenieleza habari za semina moja aliyohudhuria katika hoteli ya Blue Pearl, moja kati ya wasemaji wa hiyo semina alizungumzia hali ya foleni ya Bongo aliyodai inavyosikitisha kwani haiwezekani atoke Afrika kusini kuja Tanzania kwa masaa matatu na kutoka uwanja wa ndege J.K Nyerere mpaka Blue Pearl kwa masaa hayohayo matatu, akastaajabu! Ila sisi hatukustaajabu ndio huku “kwetu” kulivyo!
Mzee wa busara akasema nasikitika  pale “nkulu” akimaanisha Ikulu, hata mashujaa wetu hawathaminiwi hata kwa kumbukumbu angalia, anwani ya nkulu wanaandika barabara ya “Barack Obama” hivi hata kuiita bararaba  ya  Mangi Marealle, Kinjekitie Ngwale au Mirambo. Kuna jamaa muuza chips jirani kwanye kibanda kilichoandikwa  “Hapa Kazi Tu chips” akasema  wakihamia kuna barabara inaweza kuitwa  barabara ya “George Bush”.  Nikamjibu kwa mbwembwe za kimombo “are you serious”. Akanijibu hapa Dar mbona imewezekana?
Kahawa ikawa tayari tukaanza kunywa uchungu wa kichangamsha mwili kile,  ndipo jamaa yetu wa bodaboda akatokea akisema  hii hela kutonekana mwisho wake ni nini?  “Mzee kijana”  akadakia akisema kila sehemu hakuna hela halafu eti majipu yametumbuliwa pesa iko wapi?
Yule jamaa wa benki akasema kwenye uchumi kuna kitu kinaitwa “economic paradoxes”, naona mnashangaa sana uongozi uliopita kulikuwa na ufisadi, na rushwa  na bado pesa ilikwepo lakini sasa hivi hela hamna mnasikia majipu yametumbuliwa mengi.



Mawasiliano kwa namba 0656 859045 au barua pepe petermmbaga29@gmail.com

Tuesday, 20 September 2016

MLIPUKO MFULULIZO MAREKANI HUENDA IKAWA NA SURA YA UGAIDI

Wakati wachunguzi wa shirika la kijasusi la Marekani  FBI, mjini New York wakifuatilia ushahidi  ili kubaini   chanzo  cha  bomu lililolipuka katika eneo la Chelsea huko Manhattan siku ya Jumamosi usiku na kifaa cha pili ambacho hakikulipuka kilichopatikana eneo hilo, shirika hilo  la FBI pia  limesema linachunguza bomu lingine lililopuka katika jimbo la New Jersey saa chache kabla yakutaka kuongea na waandishi wa habari.
Agenti maalum wa FBI, Richard Thornton.
Mlipuko huo ambao ulitokea saa chache kabla ya "agenti" maalum wa FBI kuhusu tukio hilo, Richard Thornton kuzungumza na waandishi wa habari, alidai “kwa sasa tunafanya uchunguzi wa awali kama ni gaidi, nasema uchunguzi wa awali kwasababu kuna vitu vingi hatufahamu, hatufahamu kama shambulio hili linahusisha kikundi gani cha ugaidi, hivyo ndivyo uchunguzi ulipofikia”

Katika tukio hilo lilotokea eneo la Chelsea watu 29 wamejeruhiwa na tayari watu hao wameruhusiwa kuondoka hospitalini baada ya matiba huku maofisa hao wa FBI wakisema kuwa wanachunguza madai ya kundi la Islamic State yakuwa mtu mmoja aliekuwa amevalia mavazi ya kiaskari mwenye asili ya Somalia na kuendesha shambulizi kwa kutumia kisu na kuwajeruhi watu nane ndani ya duka la Crossroads Center mall, jimbo la Minnesota nchini marekani siku ya hiyo hiyo ya Jumamosi ni mfuasi wao.


Monday, 5 September 2016

NDEGE ZILIZOBEBA MIRAA MARUFUKU SOMALIA

Serikali ya Somalia imesitisha kwa muda ndege zote zinazoingiza miraa kutoka taifa jirani la Kenya.
Biashara hiyo ina thamani ya mamia ya mamilioni ya madola kila mwaka.
Waziri wa maswala ya anga nchini Somalia Ali Ahmed Jama Jangali,amesema kuwa marufuku hiyo itaanza kutekelezwa siku ya Jumanne lakini hakutoa maelezo zaidi.
Miraa ni maarufu sana nchini Somalia ,ambapo hutafunwa kwa saa kadhaa na hutumika kusisimua mwili .
Miraa mingi katika sehemu ya kusini na katikati mwa Somalia hutoka nchini Kenya.
Haikuzwi nchini Somalia.
Miraa hutumika na imepigwa marufuku nchini  Tanzania, Marekani pamoja na mataifa kadhaa ya Ulaya.



Chanzo:BBC Swahili

Sunday, 4 September 2016

MAMA THERESA WA CALCUTTA ATANGAZWA KUWA MTAKATIFU

Maelfu ya watu wameshuhudia kwa pamoja ambapo Papa Francis amemtangaza mtawa Mama Teresa kuwa mtakatifu.
Mwanamama huyo wa Albania ambaye alifariki mwaka wa 1997 alianzisha shirika la hisani la kimishenari ili kuwasaidia wasionacho katika mtaa wa mabanda wa Calcutta nchini India.
Hivyo kuanzia sasa ataitwa mtakatifu Teresa wa Calcutta.
Waandishi na wataalamu wa mambo wanasema kuwa maisha yake yanaenda sambamba na maono ya Papa Francis kuhusu kanisa linalojikakamua kuwasaidai watu masikini.
Lakini wakosoaji wanasema kuwa Mama Teresa hakuwasaidia watu waliokuwa wagonjwa na alilaumiwa kwa kujaribu kuwabadilisha dini watu masikini wa kabila la Hindu nchini India kuwa Wakristo.
 Mama Theresa