Hii
ni makala niliyokuwekea uisome hapa Oktoba 14, ila siku iliyofuata Oktoba 15,
2016 imepata nafasi kwenye gazeti la
TanzaniaDaima
Na
Peter C. Mmbaga
Peter C. Mmbaga
Ndiyo muda wangu wa kuingia “Giningi” na Wabasi wenzangu
ambao tunaamini kwenye mawazo ya chanya pasipo kupepesa macho,
safari ya Giningi inahitaji ufunge mkanda kweli kweli na leo nipo njiani
kuongea na kumpa pongezi za “kuondoka” zake mapema mbasi wangu
katika fikra Mwalimu mkuu, Baba Makongoro kwakuwa angebaki mpaka sasa
angekuwa anaduwaa kama mimi na vile hapendi kuonekana kwenye “maamuzi
ya umimi”, anakuwa mpole tu.
Kumbuka kipindi kile wakisema baadhi ya viongozi
waliokuwa wanafanya mambo tofauti, yeye alitoa tamko gani? Kwenye
kitabu chake cha “Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania” anabaki kama mshauri tu,
japo kutokana na hadhi yake ama “popularity” aliyokuwa nao asingesikilizwa na
wananchi kweli, katika kukataza?
Aliwaachia uhuru wajitathimini wenyewe, na uhuru ni mbaya
sana, walipoona mbasi wangu katika fikra chanya hajaja juu
wakaona sawa tu, mambo yanafanyika, anajifanya haoni. Kumbe “mbasi”
ulikuwa “unawachora” tu.
“Giningi yetu” ina raha yake huku yupo Baba wa maridhiano, mbasi
wangu katika fikra, Mandela yeye anatabasamu tu anasema “Real leaders must be
ready to sacrifice all for the freedom of their people“ kwa tafsiri isiyo
rasmi ni kuwa “ Vingozi wa kweli wanatakiwa wawe tayari kujitoa vilivyo
kwa uhuru wa wananchi”, naye namwangalia natabasamu kwa kuwa kazi
aliyoiamua Rais JPM ni ngumu sana kwakuwa wapiga vita
mfumo mzuri wapo na hasa watendaji, “We got a Long Way To Freedom”
ila kwa imani atawatumbua tu!
Baba Makongoro bwana ananifurahisha sana akasema “Siku
Wamarekani wakinisifia nimefanya kazi nzuri nitajiuliza kuwa nimekosea wapi?” ndiyo kitu nilichompendea hasa kwa
kauli hizi za kujiamini kwa nukuu nilyooina kwenye gazeti moja la kila siku
miaka mitatu nyuma, ni kauli ya Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM), chuo ambacho Mwalimu alikianzisha na mara kwa mara kufika hapo kwa
ajili ya mijadala na wanafunzi kuhusu uhuru na maendeleo ya Afrika na dunia kwa
ujumla, Bashiru Ally, anaamini Mwalimu anastahili kupewa tuzo
lakini ananyimwa kutokana na kuyaudhi mataifa ya magharibi wakati aliongoza
harakati za kudai haki za binadamu na uhuru wa mataifa ya Afrika. Huu ndiyo
ushujaa tunaouhitaji Rais JPM piga kazi kwa haki na kweli usihitaji kusifiwa na
watu wa nje ila tu angalia uhuru uwepo kama Baba Makongoro alivyoutoa. Mwalimu vijana wa leo sio wa kipindi
kile “pesa” inawanunua wanashindwa kutetea maslahi ya nchi, hasa
wasomi dira hawaileti , ukanijibu “pesa ni matokeo” kama ulivyoainisha kwenye
kitabu chako cha cha “Ujamaaa na Kujitegemea” lakini Mwalimu sasa sivyo,
nadhani wakati nao unabadilika, ila wanaamini, pesa ndilo lenye
nguvu!
Sasa hivi wasomi wanaonekana shujaa kwenye dimbwi la
mfumo huu wakuogopa kuhoji, vyuo vikuu vimepoa vimenyamaza, nahisi
huko ndiko ulipowasikia kwa mara ya kwanza kina ndugu Lowassa,
JK na wengineo, ila sasa wanaogopa kuitwa wasaliti ni
bora kuliko kuonekana mnyenyekevu kwao halafu kwenye jamii uonekane “Kamuzu”.
Wazee wetu ukiwauliza watakujibu enzi za kupigania uhuru
walimwita huyu mtu walimwitaje "aliyeolewa na wazungu"
aliwabania waafrika haki zao, ndiyo nyimbo iliyokuwa kwenye mchamchaka.
Kwanini nimesema hayo? Nakumbusha raia wote na
viongozi wasaliti kwa machinga, boda boda, mama ntilie , wasakatonge , wasio na
ajira ni bora uonekane umemsaliti rafiki yako anayetafuta “ujiko” kwa
njia ya “matukio” kuliko kuitwa "umeolewa nao" na jamii ni
mbaya sana, lakini Mwalimu hao watu tunao?
Wewe mwenyewe ukasema “Unyenyekevu ukizidi unazaa uoga, uoga
huzaa unafiki na kujipendekeza, mwisho wake mauti”
Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu J.K Nyerere |
Baba Makongoro kuna walimu wamekuwa ‘maarufu” kwa
kipindi hichi kubwa ni kumpiga mwanafunzi wa kidato cha tatu mwezi huu
uliotuaga, kuna kitu baba nimegundua Walimu wengi wanakwenda pasipo ‘passion”,
lengo ni kupata mkopo ambao miaka ya karibuni imekuwa kipaumbele kwa
walimu ili kusaidia changamoto za elimu yetu, japo wanafunzi wa siku hizi ni
watukutu kufikia hatua ya kuchanganywa na malezi na utandawazi ambao tumeupokea
“negative” sana kwenye matumizi yake.
Mtoto kupewa adhabu hatujakataa, ni moja ya kufunza baba,
kama wewe ulifanya pale Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam kwa mmoja wa viongozi wetu
kugoma akiwa Rais wa serikali ya wanafunzi-Daruso enzi zako
wakigomea kutopatiwa maziwa na siagi, kweli enzi zako “walikula
bata” mbasi wangu, leo hii wanasota watoto wanaoishi kwenye mazingira
magumu “no mkopo”, kipaumbele kimeharibu kila kitu na wengi wanakimbilia
huo ualimu, tasnia nyingine baada ya miaka kumi wasomi wengi watakuwa
kwenye tasnia moja halafu wasio na “passion” japo sio wote ama tasnia
zote lakini Je, hali itakuwaje?
Enzi zako mtu akisema mimi ni mwalimu hiyo heshima anayopewa
ni nzito lakini leo sielewi, thamani imepungua sijui kisa ni nini? Ndo
maana misongo ya mawazo inakuwa mingi sana hata kupiga wanafunzi.
Mimi kusema kula bata ni kweli kwasababu habari
hii niliwahi kuhadithiwa na “anko” wangu aliyesoma na ndugu
Rais mstaafu kijana wako, Jakaya Kikwete pale Shule ya Tanga
(Tanga School) enzi zako Mwalimu Mkuu wa fikra
yakini, juu ya elimu,chakula(asubuhi chai nzito), na usafiri
wa bure kwa gharama za Serikali. Ila nyakati zinabadilika!
Wakati tunaendelea na maongezi yetu ya Kibasi zaidi huko “Ginigi
yetu” kuna msomi enzi zake Mwalimu akaniuliza leo hii
madaftari yanauzwa kwa shilingi ngapi wanafunzi, vipi
madawati shuleni? Nikamwambia najua, wajua, akanijibu halafu tuna misitu
mikubwa nchini?
Baba Makongoro ulivyooondoka kuna mwana hip hop aliimba
“wasomi wanakimbilia siasa, Je, nchi itajengwa na nani? Hata mimi najiuliza
nchi itajengwa na nani? Sielewi!
Mwalimu alizidi
nitoa tongotongo katika kuandaa na maswala mengine yenye maslahi
kitaifa yasiyohitaji mgawanyiko wa itikadi na uchama kwa kile
waingereza wanachosema “number do not lie” wakimaanisha nambari
haidanganyi kwa kufanya mambo kwa “ tathmini onyeshi” moja ni moja
na nane si saba, kwakumshangaa Waziri mwenye dhamana ya Afya
kukinzana na Makamu wa Rais, kuhusu upungufu wa madawa kwenye
bohari ya Taifa!
Nakamwambia Mwalimu neno “siasa” ni mwiba kwa wananchi si
neno zuri kulizungumza japo Rais JPM anawapa matumaini kuwa
utendaji wake kwa kiasi chake kuna tija imeonekana Mwalimu, kabla
hatujaendelea zaidi nikatafakari kuwa ujasiri ni pale
unapojua "siasa" si tatizo bali tatizo ni picha na taswira
iliyojengeka mtu kuwa "mwanasiasa" ndani ya jamii na jibu tunalo kwa
utendaji mzuri wa viongozi wetu ili kugeuza neno "politics is dirty
game". Itabadilika tu hii hali, kama enzi zako Ualimu ulivyoheshimika leo
hii unaonekana taaluma ya kawaida! Sisi wenyewe hatupendi Mwalimu.
Nikamwona kifkra shujaa wa India, Mahatma Ghandi na falsafa yake
kuwa “I love your Christ but not your Christianity” nikimaanisha serikali
na vyama vya siasa ni sehemu salama na sera zenye weledi lakini walioko
ndani yake ndiyo kuna kila aina ya ubaya,udhalimu, na siasa chafu japo kuna wasafi na wenye kweli daima.
Naipenda sera weledi yenye utekelezaji, itikadi ninayo,na “imani”
kwa kiongozi na mwananchi mwenye misingi fanikishi ya kuileta
“Tanzania ninayoitamani”, si kauli za kutofautiana
za “makaisari” wetu na sio ushabiki wa chama. Haya
yakifanikiwa mbona “siasa nyeupe” itaonekana na tuishi ili kumuenzi Baba wa
Taifa na hilo ndilo kusudi lake, siku siku ya leo tutoe “speech” za kumsifia ila hizo
sifa zake ninyi kiuhalisia na kiutendaji mnaziishi kwenye vyombo vya
habari.
Watanzania ni wepesi wa kusahau kama zao la “kuamua”
litaleta watu makini, wazalendo,wenye dira elekevu, na misimamo
binafsi tutakuwa tumefikia kiwango kikubwa katika “mchakato”
wa kujitambua na kuutambua ukweli na ule mtazamo wa siasa ni mchezo mchafu
(politics is the dirty game) tukiishi ya Baba Makongoro na sio kuienzi siku
yake bila matendo sio maneno. Hata Baba Makongoro kwenye “mjadala”
wetu hapendi hilo swala.
Alichopenda ni “Argue, Don’t shout” na hichi ndicho serikali
inakinzana na vyama vya upinzani sana, kwasababu kila mmoja anatoa
kinachojipendelea ila tukumbuke tunajenga moja, Tanzania yetu katika siku hii
ya kumuenzi Baba wa Taifa sio kwa makelele na sifa kedekede bila kuishi
aliyoyaishi!
Pumzika kwa amani Mkuu, muda mwingine tutatembeleana!
Mawasiliano 0656 859045 au barua
pepe: petermmbaga29@gmail.com
Unaweza kuacha comment yako hapo chini kwa kile ulichokisoma!
Unaweza kuacha comment yako hapo chini kwa kile ulichokisoma!
IPO safi, nimeipenda hii makala.
ReplyDelete