Hilo limetokea baada ya Donald Trump kuanza kuamini Obama amezaliwa Marekani ambapo mgombea huyo kwa mara nyingine
alisisitiza kwamba hayuko tayari kuamini kwamba Bw Obama alizaliwa Marekani.
Akihojiwa na gazeti la Washington Post, Bw Trumo alikataa kusema Bw Obama
alizaliwa Marekani na badala yake akasema hangejibu swali hilo.
Ofisi ya kampeni ya mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani
Donald Trump imetoa taarifa ikisema sasa anaamini Rais Obama alizaliwa nchini
Marekani.
Trump huchukuliwa
mwanzilishi wa kundi lijulikanalo kama "birther movement", ambalo
huamini Rais Barack Obama hakuzaliwa katika jimbo la Hawaii, na kwa hivyo
hakufaa kuhudumu kama rais wa Marekani.
Anasema taarifa hiyo
iliyotiwa saini na mshauri mkuu wa Trump, Jason Miller hata hivyo si kwamba
anakubali makosa.
Badala yake, Miller
aliweka lawama kwa Hillary Clinton na kundi lake la kampeni la mwaka 2008,
ambapo Bi Clinton alikuwa anashindania tiketi ya chama cha Democratic na Obama.
Hakuna ushahidi wa
kumhusisha Bi Clinton na kundi la Birther. Akijibu, Bi Clinton alisema kupitia
Twitter kwamba mrithi wa Rais Obama "hawezi kuwa mtu aliyeongoza kundi la
ubaguzi wa rangi la Birther".
Wanaopinga kwamba Obama
alizaliwa Marekani wamekuwa wakisema alizaliwa Kenya (babake Obama alikuwa
Mkenya).
Taarifa katika
magazeti kadha ya Marekani zinaashiria uvumi huo ulienezwa mwaka 2008 na
wafuasi sugu wa Bi Clinton ilipoanza kudhihirika kwamba mwanamke huyo
hangeshinda uteuzi wa chama cha Democratic.
Madai hayo baadaye
yalifufuliwa na wafuasi wa mgombea wa Republican John McCain alipoanza kuachwa
nyuma na Obama kwenye kura za maoni, tovuti ya Fact Check imeripoti.
Obama
Trump alianza
kujihusisha na suala hilo kabla ya uchaguzi mkuu wa 2012.
Aprili 2011, Trump alimtaka Obama kuonyesha hadharani cheti
chake cha kuzaliwa, wito ambao uliungwa mkono na wanasiasa wengi wa Republican
akiwemo aliyekuwa gavana wa Alaska Sarah Palin.
Mwaka 2012 mgombea wa
wakati huo wa Republican Mitt Romney alirejelea madai hayo kwenye mkutano wa
kampeni Agosti mwaka huo.
Chanzo:BBC Swahili
No comments:
Post a Comment