Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila. |
Pamoja na mkutano wa upatanishi
ulioongozwa na aliyekuwa mwenyekiti wa
umoja wa Afrika Bwana Edem Kodjo
uliofanyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwanzoni
mwa mwezi Septemba mwaka huu kati ya wapinzani na
serikali ya nchi hiyo inayoongozwa na Rais Joseph Kabila. Tume ya
Uchaguzi ya Jamhuri ya Kidemokirasia ya Kongo
imesisitiza kuwa hakuna uwezekano
wa uchaguzi kufanyika nchini humo mwaka
huu kama ilivyoelezwa kwenye katiba ya nchi hiyo.
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya nchi hiyo ambayo
ilitarajiwa kuanza mchakato wake wa kufanyika kwa uchaguzi kuanza jumatatu ya
wiki hii, Bwana Corneille Nangaa amesema suala hilo kwa sasa haliwezekani na
badala yake anashauri uchaguzi ufanyike mwaka ujao.
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, Corneille Nangaa. |
Kufuatia tamko hilo
hali si shwari ndani ya miji mikubwa
ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
ambapo makundi ya upinzani yamefanya
mkaandamano makubwa katika miji ya nchi
hiyo ikiwemo Kinshasa na Kivu pamoja
na maeneo mengine ili kuishinikiza tume
ya uchaguzi ya nchi hiyo itengue
uamuzi huo na kuruhusu uchaguzi ufanyike
mwaka huu kwa mujibu wa katiba
No comments:
Post a Comment