Monday 19 September 2016

YAANI..... ZIDANE KAMA GUARDIOLA!

Zidane(kushoto) na Guardiola.
Ni tukio la kihistoria kwa mchezaji wa zamani na sasa kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane kwa mechi iliyopigwa usiku wa jumapili(Sunday Night Football)  ambapo Madrid waliibuka mpaka Espanyol pasipo nyota wao Christiano Ronaldo na Gareth Bale na kushind goli 2-0. Ushindi huo uliowafanya kuwa juu kwa pinti tatu dhidi ya mahasimu wa Barca kwa michezo mitano katika msimu mpya, na zaidi kuwafanya Los Blancos kuwa na historia ya kushinda mechi mwanzoni mwa ligi.
Ishu ni kuwa mpaka mechi ya jana Madrid walishacheza michezo 16 mfufulizo bila kufungwa hivyo kuwa historia kwa bosi wao, Zidane na hivyo kutarajia kuvunja rekodi  ya mkatalunya Pep  aliyeko Man City kwa sasa  kwenye mechi yao ya jumatano dhidi ya Villareal ndani ya dimba la Santiago Bernabeu.
Mpaka mechi ya jana Zizzou alifikia rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Pep Guardiola.
Rekodi ilikuwa hivi;
Guardiola alikuwa anaongoza kwa mechi 16 bila kufungwa ndani ya ligi ya Spain(La Liga) mpaka anaondoka na kutimkia Bayern na hivi sasa Man City.
Madrid wamefunga magoli 51 na  kushindwa  mara 12 katika kipindi cha  ushindi mfufulizo, ambapo wanaKatalunya wamefunga magoli 60 na kushindwa mara 6 katika uongozi wao wa msimu wa 2010-2011.
Zidane enzi akiwa mchezaji Madrid

No comments:

Post a Comment