Mgombea wa Democratic, Donald Trump |
Akizungumza mjini Fort Myers katika jimbo la Florida nchini Marekani Bwana Donald Trump amesema kuwa hatua ya serikali ya nchi hiyo inayoongozwa na chama cha Democratic kumpatia matibabu ya kisasa mshukiwa wa ugaidi ni ishara ya dhahiri kuwa kuna udhaifu mkubwa ndani ya idara ya usalama wa taifa ya nchi hiyo, Bwana Trump alisema ‘’Sasa tumemfanyia ukarimu wa ajabu sana, ametibiwa na miongoni mwa madaktari bora duniani, amepelekwa kwenye hospitali ya kisasa na amepewa chumba cha kisasa hospitalini hapo na huenda atapokea huduma zote akiwa humo, ukizingatia jinsi nchi hii ilivyo’’.
Bwana Ahmad Khan Rahami wenye umri wa miaka 28 ambaye ni mzaliwa wa Afghanistan anatuhumiwa kufanya mashambulizi ya kigaidi katika miji ya New York na New Jersey nchini Marekani jumamosi iliyopita ambapo tayari amefunguliwa mashtaka matano ya kujaribu kutekeleza mauaji.
Mshukiwa wa mlipuko miwili mfufulizo New York na New Jersey, Ahmad Rahmani Khan |
Mgombea urais wa Republican nchini Marekani Bwana Donald Trump ameelezea masikitiko yake kuhusu namna serikali ya nchi hiyo ilivyomkarimu mshukiwa wa vitendo vya kigaidi katika jiji la New York jumamosi iliyopita Bwana Ahmad Khan Rahami ambapo maofisa wa serikali wanadaiwa kumpatia matibabu mshukiwa huyo na kisha kumpatia wakili atakayemtetea wakati atakapopandishwa kizimbani kwa tuhuma za ugaidi.
No comments:
Post a Comment