Monday 17 October 2016

VIDEO: MSANII KOFFI OLOMIDE AWAOMBA RADHI WAKENYA


Mwanamuziki wa Congo, Koffi Olomide ambaye Julai mwaka huu aliwasili  Nairobi Kenya  kwa ajili ya shoo na baadae kuripotiwa kukamatwa kwa tuhuma za kumshambulia “dancer” wake wa kike ni baada ya kusambaa kwa video iliyomuonyesha akifanya kitendo hicho. Baada ya kupita miezi kadhaa tangu kutokea kwa tukio hilo na Koffi Olomide kutowahi kujitokeza hadharani kulizungumzia, amejitokeza kupitia kipindi cha TV cha Churchill Show, baada ya kupita miezi mitatu amewaomba msamaha wakenya na mashabiki wake kwa ujumla n kunukuliwa akisema

’Kupitia Churchill show, nataka kusema na nyinyi na kutuma ujumbe wa upendo, heshima na urafiki, mimi nasikitika kwa kile kilichotokea na maombi yangu nisamehewe kwa kile kilichotokea, mimi ni mwanadamu tu licha kwa kuwa ni maarufu’:- Koffi Olomide



No comments:

Post a Comment