Monday 5 September 2016

WASANII WAMEPOKEA VIBAYA STORI YA LIL WAYNE KUACHA MUZIKI


Mpaka sasa wasanii na mashabiki kibao wamepokea stori hizo kwa huzuni wakiwemo  Missy Elliott, Lupe Fiasco, Chevy Woods,  Flying Lotus, na wengineo, Mkali Liltunechi ameamua hilo baada ya kuona muziki wake umeandamwa na matatizo kibao.
Aliandika kwenye Twitter: "Sasa sijiwezi tena, sipo poa kiakili, na naondoka kwa staha na nashukuru mashabiki wangu."

Hata hivyo, hajafafanua iwapo ataacha sekta ya uimbaji kabisa, au ataacha tu uimbaji wa muziki wa kufoka. Mwanamuziki huyo wa umri wa miaka 33 hata hivyo amesema hataki "kuonewa huruma".
Lil Wayne amekuwa akigonga vichwa vya habari hivi karibuni kwa visa mbalimbali,  huku rapa Rick Ross akionekana kujibu maneno ya shabiki  aliyehitaji Tunechi kusainiwa Maybach Music Group(MMG) kwa kuandika “Muunganishe Birdman kwenye simu”

Amekuwa na mzozo wa muda mrefu na  lebo ya Cash Money Records inayomilikiwa na babaye kimuziki Birdman, kuhusiana kucheleweshwa kwa albamu yake ya 11, ambayo imepewa jina Tha Carter V. Alishutumu kampuni hiyo siku mbili zilizopita akitumbuiza na Drake mjini Miami.
Polisi Miami walifika nyumbani kwake kisiwa cha La Gorce baada ya mtu kupiga simu 911 akisema kulikuwa na ufyatuaji risasi. Habari hizo hazikuwa za kweli.


Hii ndio “tweet”  ya Lil Wayne;
 Lil Wayne WEEZY FVerified account‏@LilTunechi
I AM NOW DEFENSELESS AND mentally DEFEATED & I leave gracefully and thankful I luh my fanz but I'm dun

Hawa ni kati ya wasanii walioguswa;

 Missy Elliott ‏@MissyElliott  @LilTunechi Prayers up 4 whatever u may be enduring right now this to will pass & may u find PEACE  I will always be a fan of your work


Chris Clemons ‏@chrisclemons91
@LilTunechi       The game will never be the same!!! Long live the  of my generation.


No comments:

Post a Comment