Sunday 4 September 2016

MOURINH0 KAMGEUKA SCHWEINSTEIGER

Ilionekana kama mvumilivu hula mbivu kwa  kiungo Bastian Schweinsteiger baada ya kocha wa Man U, Jose Mourinho  kuonyesha kutomhitaji  ila kiungo  alikaza na kuonekana shujaa mbele ya “special one”  siku chache baada ya jina lake kujumuishwa kwenye kikosi cha Man United kwenye msimu wa ligi wa 2016-17,  ila balaa limekuja baada ya Bastian Schweinsteiger kugeuziwa kibao na kocha wake Mourinho baada ya jina lake kutojumuisha katika kikosi kitakachoshiriki Ligi ya Europa. Schweinsteiger ambaye huko nyuma alicheza kwa mafanikio makubwa kunako klabu ya Bayern Munich ameichezea Ujerumani michezo 121.
Kiungo huyo mkongwe amestaafu soka la kimataifa  baada ya Jumatano  iliyopita kufanyiwa sherehe ya kuagwa kwenye Timu ya Taifa ya Ujerumani maarufu kama Die Manschaft kufutiwa kufanyika mchezo maalum dhidi ya Finland na kushinda mabao 2-0.
Katika kikosi hicho, viungo 10 wametajwa huku jina la Schweisteiger likipigwa panga.
Kikosi kizima kipo hivi:
Makipa: David De Gea, Sergio Romero, Sam Johnstone
Mabeki: Eric Bailly, Phil Jones, Marcus Rojo, Daley Blind, Chris Smalling, Luke Shaw, Timothy Fosu-Mensah, Antonio Valencia, Matteo Darmian, Axel Tuanzebe
Viungo: Paul Pogba, Juan Mata, Jesse Lingard, Michael Carrick, Ashley Young, Ander Herrera, Henrikh Mkhitaryan, Marouane Fellaini, Morgan Schneiderlin, Memphis Depay
Washambuliaji: Wayne Rooney, Zlatan Ibrahimovic, Anthony Martial, Marcus Rashford.


No comments:

Post a Comment