Sunday 2 October 2016

DAR DERBY SIO SEHEMU YA KUCHEZEA HISIA ZA WATU

Na
Gilbert Nchimbi, SJMC
+255 657 215 404

Mpira wa miguu ni mchezo unaopendwa na watu wengi sana duniani kwa hapa Tanzania, klabu kubwa za Simba na Yanga zina mashabiki wengi mno ndio maana uwanja unajaa sana zikikutana.

Hawa  watu wakikusanyika pale Uwanja wa taifa sio kama kuna sehemu wanalipwa, sio kama wanakodiwa mabasi kwenda kwenye ule mkusanyiko kama ambavyo tumezoea kuona kwenye mikutano ya siasa, mara huyu kapewa fulana huyu kapewa khanga,  huyu kapewa kofia,  huyu kakodiwa basi ili afike kwenye mkutano lakini kwenye mpira ni tofauti wale watu uliowaona pale uwanja wa taifa kushuhudia pambano la simba na yanga hawajakodiwa gari jumamosi ya jana  wala hawalipwi kufika kuona ile mechi cha zaidi wale ndio huwa wanalipa pesa zao kuingia pale uwanjani yaani kinachowapeleka pale ni mapenzi na hisia zao walizonazo juu ya timu zao watu wanazipenda hizi timu watu wanapoteza fahamu kwa ajili ya hizi timu watu wamepoteza maisha sababu ya Simba na Yanga.

Sasa mnavyoleta masihara na hisia za watu wale pale uwanjani kwa kutuwekea marefarii ambao wanashindwa kusimamia sheria kumi na saba za huu mchezo wa soka kuna hatarisha sana maisha ya wapenzi wa huu mchezo tuwe makini na waamuzi makosa yao yanapelekea amani kuvurugika uwanjani watu wanashindwa kuvumilia zingatieni sana huu mchezo mpira wa miguu ni zaidi ya mchezo,  mpira wa miguu ni maisha watu wanahitaji haki itendeke ili waishi kwa amani. Ni zaidi viti mia mbili kuharibiwa na baadhi ya watu kujeruhiwa hiyo jana.

Tusitake yanayotokeaga kwenye mechi za watani wa jadi kwenye nchi za wenzetu yatokee nchini kwetu ndo tuanze kulizingatia hili.

No comments:

Post a Comment