Sunday, 16 October 2016

NGOMA MPYA: RAYVANNY & NEYLEE- RUDI

Kitu kipya kwa mashabiki kinaitwa Rudi toka kwa  Rayvanny na Neylee
Kudownload Bonyeza hapa

UCHAGUZI MAREKANI: TRUMP ATAKA CLINTON "AFANYIWE UKAGUZI WA DAWA"


Mgombea wa Republican, Bw. Donald Trump
Mgombea kiti cha Urais kwa tiketi ya chama cha Republican nchini Marekani, Donald Trump, amemshutumu mpinzani wake Bi Hillary Clinton kwa kutumia aina fulani ya dawa, wakati wa mjadala wao uliopita wa moja kwa moja wa runinga.

Anasema kuwa alikuwa na haiba mwanzo mwanzo wa mjadala huo.
Sasa anapendekeza kuwa wafanyiwe majaribio ya matumizi ya dawa, kabla ya kufanyika kwa mjadala wao wa mwisho hapo siku ya Jumatano ya wiki hii.
Katika mkutano wake wa hivi punde uliofanyika New Hampshire, Bwana Trump kwa mara nyingine, amedai kuwa kuna njama za kumuibia kura.
Timu ya kampeini ya Bi Clinton, imesema kwamba wapigaji kura, sasa wameona bayana kile anachokiita juhudi za aibu za Bwana Trump za kutaka kuhujumu shughuli za upigaji kura.
Trump, anazidi kudidimia katika majimbo mengi, huku akikabiliwa na madai ya udhalilishaji wanawake kingono.


Chanzo: BBC Swahili

MAGAZETI YA LEO HAYA HAPA UNAWEZA UKAYAPITIA

Front Pages za Magazeti ya leo Oktoba 16, 2016 yapo tayari hapa.


SHIRIKA LA NDEGE LA LA KENYE LAAHIRISHA SAFARI KISA WAFANYAKAZI HAWAJATOKEA KAZINI



Shirika la ndege la Kenya Airways limeahirisha safari zake tano za kwenda ndani na nje ya nchi leo October 16 2016 kutokana na upungufu wa Wahudumu wa ndege kazini.
Taarifa inasema sababu hasa ya kuahirisha safari hizo tano za MombasaKilimanjaro,JubaMaputoHarare na Lusaka ni kutofika kazini kwa Wahudumu wa ndege ambao wamepangiwa zamu kwa wakati huo.
Imeelezwa kuwa baadhi ya Wafanyakazi wa shirika hilo hawajaripoti kazini toka Ijumaa iliyopita ambapo shirika linaendelea kufatilia kujua chanzo ni nini na jinsi ya kutatua tatizo na Mwajiri.
Kwa utaratibu ndege za abiria huwa na masharti yake kwenye kila safari ikiwa ni pamoja na kuwa na namba flani ya idadi ya Wahudumu ndani ya ndege ambayo ni lazima itimie, sasa kutokana na Wahudumu wa Kenya Airways kuwa wachache imebidi ndege nyingine zisisafiri.

Chanzo: Millardayo



DIAMOND, HARMONIZE NA DJ DOMMY WACHUKUA TUZO ZA AFRIMMA 2016

Watanzania Diamond, Harmonize na dj Dommy wameshinda tuzo Afrimma(African Music Magazine Awards) 2016 ambapo mwanamuziki Diamond ameshinda tuzo hiyo katika kipengele cha msanii bora wa kiume kwa upande wa Afrika Mashariki.  Vilevile Harmonize ambaye amesainiwa WCB nae ameshinda tuzo ya msanii bora chipukizi barani Afrika. Kwa upande wa Dj dommy  ameshinda tuzo ya Dj bora Afrika. Mdada  Akothee kutoka Kenya ameshinda tuzo ya msanii mora wa mike  Afrika Mashariki. SautiSol kutoka Kenya wameshinda tuzo ya Kundi Bora Afrika. Kwa upande wa Afrika Magharibi mwanadada Efya wa Ghana ameshinda kipengele cha msanii bora wa kike Afrika Magharibi alichokuwa akishindana na wakali kama  Yemi Alade(Nigeria) na Tiwa Savage(Nigeria).

LIST NZIMA YA WASHINDI WA AFRIMMA 2016 HII HAPA:
Best Male West Africa  Olamide (Nigeria)
Best Female West Africa  Efya
Best Male North Africa – Amr Diab
Best Female North Africa – Ibtissam
Best African DJ USA – Dj Dee Money
Best Male Central Africa – C4 Pedro
AFRIMMA Video of the year – Brother brother Bisa Kdei
Best Female Central Africa – Daphne
Music Producer of the year – Masterkraft
Best male South Africa  AKA
Best African Dancer – Brenda Derry ( Cameroon)
Best Female Southern Africa  Chikune
Best Rap Act – Phyno (Nigeria)
Best African Group – Sauti Sol (Kenya)
Best collaboration – Reggae blues ( Harrysong, Kcee) Nigeria
Crossing boundaries with Music – Wizkid (Nigeria)
Song of the year – Tecno Duro (Nigeria)
Best Gospel Act – Willy Paul (Kenya)
Best Male East Africa – Diamond Platnumz ( Tanzania)
Artist of the year – Flavour ( Nigeria)
Best Newcomer – Harmonize (Tanzania)
Best Dancehall Act – Shatta Wale
Best Video Director – Patrick Elis
Carribean Artist of the year – Machel Montano.


Saturday, 15 October 2016

MSHINDI WA GRAMMY ASHTAKIWA KWA UMILIKI WA SILAHA

Rapper Coolio
Mshindi wa tuzo ya Grammy katika muziki wa Rap Coolio ameshtakiwa kwa kumiliki bunduki haramu.
Waendesha mashtaka nchini Marekani wanasema kuwa bunduki hiyo aina ya handgun ilipatikana katika mzigo wake wakati wa ukaguzi katika uwanja wa ndege wa LAX mwezi uliopita.
Coolio mwenye umri wa miaka 53 huenda akahukumiwa kifungo cha hadi miaka 3 katika jela ya jimbo la Carlifornia iwapo atapatikana na hatia.
Coolio ni maarufu kwa wimbo wake Gansta Paradise ambao ulitolewa mwaka 1995. Ameshtakiwa chini ya jina lake Artis Leon Ivey.
Waendesha mashtaka wanasema ilikuwa kinyume cha sheria kwa msanii huyo kubeba bunduki baada ya kupatikana na hatia mwaka 2001 kwa kubeba bunduki ndani ya gari na mwaka 2009 kwa kumiliki dawa ya kulevya aina ya Cocaine.
Nyota huyo alitarajiwa kuwasili katika mahakama ya Los Angeles siku ya Alhamisi lakini kusikizwa kwa kesi yake kukaahirishwa hadi Oktoba 26.
Mawakili wa Coolio walimwambia Jaji kwamba msanii huyo alikuwa anawatumbuiza mashabiki wke nje ya jimbo la California na hivyobasi hawezi kuwa katika mahakama hiyo.



UJENZI WA RELI MPYA TANZANIA KUHARAKISHWA

Rais wa Tanzania Dkt. John Magufuli akiagana na Waziri wa Biashara toka China, Bw. Qian Keming baada ya mazungumzo, Ikulu jijini Dar Es Salaam

Mradi wa ujenzi wa reli ya kati nchini Tanzania unatarajiwa kuharakishwa kufuatia mazungumzo kati ya Rais John Magufuli na Naibu Waziri wa Biashara wa China Qian Keming.
Reli hiyo ya kati ni ya kutoka Dar es Salaam, Mwanza, Kigoma na inatarajiwa kuunganisha Tanzania na nchi za Rwanda na Burundi
Wakati wa mazungumzo ikulu Dar es Salaam Rais Magufuli alisema serikali inataka kuona mambo yakifanyika na kutoa matokeo bila kupoteza muda, kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu.
Serikali ya Tanzania imetenga shilingi trilioni moja kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi katika bajeti ya sasa.
"Sisi tumeamua kuanza ujenzi na tayari Wakandarasi 32 wamejitokeza kuomba kujenga reli ya kati kuanzia Dar es Salaam hadi Morogoro umbali wa kilomita 200 za mwanzo na tutatumia fedha zetu wenyewe," alisema Dkt Magufuli kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu.
"Kazi hii tunataka ianze mwaka huu wa fedha, kwa sababu upembuzi yakinifu na usanifu umeshafanyika, kwa hiyo na nyie ongezeni kasi ili mradi huu wote ukamilike, nataka uwe umekamilika kabla sijaondoka madarakani."
Dkt Magufuli alisema mradi huo una manufaa makubwa kwa Tanzania na nchi nyingine nane zinazotegemea bandari ya Dar es Salaam na kwamba kukamilika kwake kutatoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa Tanzania ambayo inataka kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
Kwa mujibu wa taarifa ya ikulu, Bw Qian aliahidi kuwa Serikali ya China itaongeza msukumo katika uharakishaji wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa reli hiyo ya kati.
"Mheshimiwa Rais Magufuli nimeielewa dhamira yako na kiu uliyonayo, naona kabisa kwamba dhamira ya kisiasa ipo ya kutosha, tunachotakiwa kukifanya ni kuwasukuma wataalamu wetu waongeze kasi," alisema.
„Na mimi nakuahidi kuwa tulikuwa tunakwenda kwa kasi ya kilometa 100 kwa saa, sasa tutaongeza na kwenda kilometa 200 kwa saa."





Chanzo: BBC Swahili




Unaweza toa comment yako hapo chini!